Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Jumapili iliyopita nilihudhuria kwenye msiba wa ndugu wa rafiki yangu, Miongoni mwa waombolezaji alikua dada mmoja mwenye miaka kama 26-30, alikuwa na mwanae wa kama miaka minne hivi

Sijui ilikuaje lakini mara yule dogo akaanza kulia na kisha kumvurumishia ngumi na mateke mama yake. Mama mtu akabakia kusema tu " Brian stooop banaa". Mpaka mama mmoja alipokuja akamwambia hiyo ni aibu mwanao hata kama ni mdogo unamuachia akupige hivyo hebu ingieni kule chumbani mkabembelezane

Watoto wote wadogo sio ajabu kuwa na utundu lakini utundu mwingine nahisi kama ni wa kukosa adabu na unaendekezwa na wazazi hasa wakike.

Nimewahi kushuhudia mtoto wa chini ya miaka mitano akiipasua simu ya mama yake kwa makusudi kwa kuibamiza chini na mama mtu anasema "mmmh leo sijui kakasirika nini huyu!" halafu akaanza kumbembeleza!

Kuna mtoto wa shangazi yangu aliwahi kumtupia usoni mfuko wa chips mama yake baada ya kugundua alicholetewa sio alichomuagiza wakati anaenda kazini!

Hapo kwenye msiba baada ya tukio la huyo mama na mtoto watu walisema mengi sana kuhusu dosari za kimalezi za wazazi wa kike wa siku hizi. Kuna mzee mmoja akawa anasema dunia inavokwenda huko baadae hayo mapenzi ya mama na mwana yanaweza kufikia hatua ya aibu zaidi hata mama "kumuonjesha" mwanae atakapo balehe

Sina hakika kama haya mambo ya kudekeza watoto kiasi hiki yalikuwepo zamani ila nahisi mengine ni kuwapotosha watoto kwa kuwapa malezi yasiyofaa.
Malezi ya kwenye tv...kujifanya wenyewe ndio wana uchungu zaidi kuliko mama zao. ..
 
so you actually believe it's dady that have to play the bigger role in co-parenting?
Nikufundishe, mtoto akiwa less than 5 years mama ni muhimu sana ila baba unatakiwa kuanza kukaonesha kuwa huna utani hasa kakikosea. Baada ya hapo hasa katika kuvunja ungo uwepo wako ni muhimu. Maana anamuona mama kama mwanamke mwenzie na anataka kuwa na opposite sex. Hapo ndipo mibaba mipuuzi inaweza kutenda upuuzi. Na mtoto wakike kama hajaanza kujamiiana utamuona alivyo free na baba ila akipata boyfriend anakuwa mita 500 na baba. Uzoefu muhimu
 
Wazazi wa kike wanachangia sana malezi mabovu kwa watoto. Tutamlaumu baba mtu ila kuna kipindi akiingilia kati ataambulia kauli "leba nilikua mwenyewe na manesi usinitesee mtoto" "haukunisaidia kupush" "huujui uchungu na maumivu ya kujifungua"

Akina mama wa siku hizi wanadekeza vibaya. Na zile kiss za mdomo uchafu mtupu
Utasema uzazi ulianza kwao...wengine hatukuzaliwa tuliokotwa..
 
Nakazia hapa..... Kuna jirani yangu ana mtoto hapa wa miaka kama mitano hivi toto halielewi lile jamani anamtukana mama yake mama nae anacheka tu, akimtuma kitu hataki yaani anamjibu mamake atakavyo.... Ukiona mtoto huyo anachapwa basi na babake sio mamake


Nilimuuliza siku moja ( mama nonino) malezi gani haya unampa mtoto? Anajichekesha tu hana cha kujibu... Kwakweli wamama ndio wanaoweza kunyoosha watoto au kulemaza watoto sababu Muda mwingi wanashinda nao wao....
Umenena kweli...
 
Nakazia hapa..... Kuna jirani yangu ana mtoto hapa wa miaka kama mitano hivi toto halielewi lile jamani anamtukana mama yake mama nae anacheka tu, akimtuma kitu hataki yaani anamjibu mamake atakavyo.... Ukiona mtoto huyo anachapwa basi na babake sio mamake


Nilimuuliza siku moja ( mama nonino) malezi gani haya unampa mtoto? Anajichekesha tu hana cha kujibu... Kwakweli wamama ndio wanaoweza kunyoosha watoto au kulemaza watoto sababu Muda mwingi wanashinda nao wao....
HAPA JIRANI ZANGU...KUNA WADADA WAWILI MTU NA DADA YAKE...MMOJA KAOLEWA NA ANA WATOTO WAWILI...MDOGO MTU HAJAOLEWA NI SINGLE MOTHER...SASA KILA MMOJA ANADEKEZA TOTO LAKE...

HUYU ANAMUONA MWENZAKE ANADEKEZA...UKIGUSA WA MWENZAKO ANAKWAMBIA MGUSE WAKO...KWAHIYO WANAANGALIANA TU...

KATOTO KAMOJA KALINISONYA NIKAKAFINYAAA...NIKAONA NIMENYANG'ANYWA MTOTO KWA HASIRA...NIKAAPA SIGUSI TOTO LA MTU...

HATA AKISEMA NINI NALIANGALIA TU...
 
Ukweli ni ukweli, na Nisiupindishe ukweli.

Single Mama wengi hawana malezi kabisa kwa watoto ..na sitoshangaa kama huyo mtoto ni wa single mama.


NI WACHACHE SANA SANA. NA HAWA WACHACHE NI LZIMA WAWE WENYE DINI KWA MAANA DINI INASTAHARISHA MTU.



Kwa ufupi.... Kama mama na baba HAWAMJUI MUNGU.....wala HAWAJAPANDIKIZA MBEGU YA MUNGU MOYONI MWA WATOTO WAO.



mtalalamika sana tu..na mtoto atabebwa nakila aina ya Dunia .


Baba Chapombe + kurudi home saa mbili au tano usiku+ kusali ni sifuri.

Mama kusali ni sifuri+ chapombe.


Nyie??? Mnafanya masihara kwa Dunia hii tuliyonayo??? Dunia ambayo Ukijichanganya kidogo tu imekula kwako???.
Umenena mazito aisee...
 
mara nyingi hiyo ni kawaida ya kina mama mfano mdogo ni kwenye kula unakuta mtoto akilishwa na mama yake ataruka ruka na kumwaga chakula wanacheka cheka naye ila mzee akipewa amlishe anakula kama kawaida
HILO LIPO KWA MWANANGU MDOGO...AKIWA ANALISHWA NA MAMA YAKE ANASUMBUA KWELI...OOOH MARA HATAKI KULA NIKAWAAMBIA HUO UJINGA SITAKI KUUSIKIA...LETA BAKULI YA UJI LETA...TUNAKABANA NA VIBAO JUU...KULA ANAKULA NA KUSAZA...
 
mtoto anapokuwa mdogo ni wa mama, kwa maana ya kwamba 80% ya malezi yake ya udogoni yanabebwa na mama. Na ndio maana hata sheria inatuambia kwa wazazi wanaoishi mbali mbali baba anaruhisiwa kuishi na mtoto akiwa tayari ana umri wa 6+.

Hivyo mtoto yeyote akiwa na mitabia ya ajabu obvious lawama nyingi zinaenda kwa mama kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake vizuri.
Wanawake hawa wanapenda sana kukimbia kuwajibika kwa mambo ambayo ni wazi kabisa ni juu yao...

Huyo dada umuulize...sawa malezi ni kwa baba...tuzae alafu nimchukue mwanangu akiwa mdogo nikamlee mwenyewe...utajisikiaje...?
 
wazazi wa siku hizi priority kwao ni kuona mtoto anakua huku akiongea kingereza kwa ufasaha, suala la nidhamu kwao sio issue kabisa.

Kwenye hizi day care centers matoto mengi yana vichwa vigumu kweli hayasikii ukiyakataza kitu, halafu yakiguswa tu na kiboko kesho yake mama mtu huyu hapa anakuja kulalamika.
Tumezitupa mkono chekechea zetu...
 
kwamba uwepo wa baba kwa mtoto mdogo ambae ndio anaanza kukua ni muhimu kuliko hata uwepo wa mama..!! nashawishika kuamini haya maneno yanatoka kwa mwanamke mvivua anayejua kuzaa tu na sio kulea.
Umeonaeeeh...haka kabibie hakana mtoto wala hakajaolewa...hebu katupishe kwnz...haka ndo katakuja kutuletea akina bob junior
 
HAPA JIRANI ZANGU...KUNA WADADA WAWILI MTU NA DADA YAKE...MMOJA KAOLEWA NA ANA WATOTO WAWILI...MDOGO MTU HAJAOLEWA NI SINGLE MOTHER...SASA KILA MMOJA ANADEKEZA TOTO LAKE...

HUYU ANAMUONA MWENZAKE ANADEKEZA...UKIGUSA WA MWENZAKO ANAKWAMBIA MGUSE WAKO...KWAHIYO WANAANGALIANA TU...

KATOTO KAMOJA KALINISONYA NIKAKAFINYAAA...NIKAONA NIMENYANG'ANYWA MTOTO KWA HASIRA...NIKAAPA SIGUSI TOTO LA MTU...

HATA AKISEMA NINI NALIANGALIA TU...
Hahahaha hahahahahahahah kwenye kukafinya sasa jamani wewe...... Ila mtoto mwenye matusi jamani hapendezi lol..... Mtoto anamwambia mamake "pumbavu" mama mtu anakenua meno tu aiseeee... Yaani hapo namzibua domo lake na kofi moja hilo lazima aumwe homa...... Mimi huwa hawaniachii watoto kabisaaaaaaa sababu ni mwendo wa makofi tu hakuna kipya
 
Ila huu uzi umenikumbusha katoto ka Dada angu ..kale katoto kamelelewa ovyo kabisa..lilitokea tukio kama ilo la msiba tuko msibani katoto kanamwambia mama ake waondoke..mama ake anakaambia subiri tuzike tutaondoka mtoto acha acharuke anamvuta mama ake nguo yani ili mradi amkere wanyanyuke waondoke..yule dada baada ya kuona kero zimezidi akampiga kale katoto kofi .

Kakaanza kujiliza kanabembelezwa kanazidisha sauti mama ake akawa kama anamnon'goneza katoto si kakaropoka "toka hapa ndio maana baba anakupigaga"

Aibu niliona mimi
MWISHO WA SIKU LAZIMA HIYO ADHABU IKURUDIE WEWE...UKOSEFU WA KUMJENGA MTOTO KIMAADILI ADHABU LAZIMA IKURUDIE MWENYEWE...
 
Back
Top Bottom