Malengo 2024:mradi wa ufugaji nguruwe na mbuzi wa nyama

P-35

Member
Oct 17, 2022
22
21
Habari wapambanaji?
Mimi ni kijana mpambanaji,katika kilimo cha mahindi na alizeti,ila mwakan nataka nijikite zaid kwenye ufugaji wa nguruwe na mbuzi wa nyama,nimewajia hapa ili kupata experience pia ushauri,nina ekari mbili nataka 1½ nilime mahindi,alizeti na maboga at least gharama za ulishaji zipungue na sehem itakayobakia nijenge mabanda yao! mwenye mawazo ushaur karibu sana, Asante!
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    55.9 KB · Views: 27
Ni wazo zuri ila jitahid kuwekeza kwenye maarifa kwanza kabla ya kuanza mfano kufuatilia makala ya ufugaji mtandao na popote kujiunga na magroup ya Whatsapp ya wafugaj e g ya nguruwe kutembelea mashamba ya wafugaji waliofanikiwa kufanya utafit wa masomo

Hasa kwenye nguruwe Kuna vingi vya kijifunza kuanza aina ya mbegu ulishaji management ya magonjwa
Namna ya kutengeneza mabanda
 
UZOEFU WA UFUGAJI WA NGURUWE WENYE FAIDA

Natambua wapo watu wengi ambao imani zao zinaruhusu wanatamani kufanya mradi wa ufugaji nguruwe wenye faida.Labda wengine wamejaribu bila mafanikio.Kwa uzoefu wangu ( refer thread yangu Mbegu nzuri ya nguruwe sasa inapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers ndivyo waweza fanya kupata mfanikio.

1. Kwanza tambua hii ni agri-business,basi kama business nyingine inahitaji usimamizi wa kutosha. Watu hudhani ukianzisha mradi na kuweka kijana wa kuwalisha basi unangojea faida tu. Ni vema ukaelewa mahitaji ya hao wanyama (chakula,usafi,malazi,tiba na jinsi ya kuzuia magonjwa) na wewe sasa ndio uwe mwalimu wa herdman wako

2. Tambua faida inatokana na aina bora ya mbegu na malezi. Nia ni kuwalea wanyama wakue kufikia uzito wa soko kwa muda mfupi.Kwa kawaida nguruwe huuzwa kwa nyama akiwa na uzito kuanzia 50kg. Shambani kwangu huuzwa kuanzia miezi 5.

3. Waangalizi(herdmen) ni watu muhimu sana kwako.Ni lazima wafundishwe vizuri na maslahi yao yaangaliwe kwa makini.

4. Nguruwe akiugua atibiwe mara moja. Nguruwe ni mnyama ambae haugui kirahisi akilelewa vema unless kama kuna outbreak ya ugonjwa(kama swine fever). Mara mojamoja huugua inabidi herdman awe na uwezo wa kugundua mapema na mnyama apewe tiba mara moja. Ukiwalea vizuri muda mwingi wanahitaji chanjo tu za minyoo na ukurutu.

5. Nguruwe walishwe ration(balanced feed) sio pumba tu au masalia ya jikoni. Tambua mahitaji ya chakula ya nguruwe (protein,wanga,mafuta,madini,vitamin) na hakikisha mchanganyiko unaofaa kwa umri husika wa nguruwe.Shambani kwangu chakula kikuu ni mahindi/mtama,pumba za mahindi na mpunga,mashudu ya alizeti, ambayo tunalima hapo shamba.Pia huchanganya madini (nguruwe mix) na mifupa/chokaa

6. Tambua gharama kubwa ya ufugaji ipo kwenye chakula (atleast 70%). Kwa wastani nguruwe mkubwa anahitaji 2kg/siku. Kwa hiyo kumlea nguruwe mmoja hadi miezi 6 anahitaji 240kg(miezi 2 ya kwanza huwa ananyonya)

(a) ukininunua chakula ambacho tayari kimechanganywa gharama ni kama tshs 600/kg
(b) ukinunua vyakula na kuchanya mwenyewe gharama ni kama tshs.400/kg
(c) Ukilima vyakula na kuchanganya mwenyewe gharama ni kama tshs 150-250/kg

Hizo ni gharama za wastani kwa morogoro na Dar es salaam.Utaona kama waweza kulima mazao kwa ajili ya mifugo wako gharama inapungua sana. Nguruwe hula pia vyakula vingine kama mihogo,majani,viazi vitamu,maboga etc. Angalia vyakual rahisi kwa mazingira unayofuga. Faida yako ipo kwenye kuuza nguruwe wa nyama. Wanunuzi wa mbegu sio wengi na sio consistent. Kwa hiyo itakuchukua a minimum ya miezi 6 kuanza kupata faida kutoka kwenye mradi wako.Huu ndio ukweli. Lengo ni kuuza idadi fulani ya nguruwe Kila mwezi. Kwa mfano ingalau nguruwe 20 kila mwezi.Unadhani unahitaji nguruwe wangapi kwa wakati mmoja kufanikisha hilo???

8. Soko la nguruwe ni kubwa na linazidi kukua. Walaji wengi wapo Dar es salaam. Waweza kuuza live hapo shambani au ukapeleka mwenyewe machinjioni inategemeana na soko lipo mbali kiasi gani. Nguruwe wa miezi 6 anaweza kukuingizia tshs.200,000-300,000 kutegemea na namna ulivyouza na uzito 9.Unaanzaje kufuga kibiashara? Mfano.

(a) Faida ndani ya miezi 6,na kuuza nguruwe 20 kila mwezi.
Nunua nguruwe jike wenye mimba uzao wa 2 ; wa2 mimba miezi 3;wa2 miezi 2 na wa2 mimba mwezi1,wa2 ambao ndiowamepandwa na wa2 wenye umri wa miezi 6. Nunua kwa mfugaji mwenye mbegu inayoanza kuzaa mapema.

Ukinunua wa uzao wa kwanza namba inakuwa nguruwe 3 badala ya 2 kwa sababu uzao wa kwanza watoto ni wachache,6-9.Pia unahitaji dume mzuri mwenye umri wa miezi 8 au zaidi.Kwa namna hii kila mwezi nguruwe wa2(au 3) watazaa watoto sio chini ya 20. Utaanza kuuza mbegu ndani ya miezi

2.Na baada ya miezi 6 utauza nguruwe sio chini ya 20 kila mwezi kwa nyama
Nguruwe jike mwenye mimba waweza kumpata kwatshs350,000-400,000
Mauzo 4-6m kila mwezi. Neti profit itategemeana na gharamaza chakula kama nilivyo ainisha awali.

Shambani kwangu tunawaachisha watoto kunyonya wakiwa na week6 na jike hupata joto na kupandwa tena ndani ya siku 3-7. Hivyo nguruwe wetuhuzaa mara 2.5 kwa mwaka. Watoto huwauza wakiwa na miezi 2 kwa 45,000-60,000 kutegemeana uzito

(b) Kama utaanza kufuga nguruwe watoto wenye miezi 2?!
Ina maana utaanza kuuza nguruwe wa nyama baada ya miezi isiyopungua 14.

Pia utahitaji kuwafanya nguruwe wako wapate mimba kwa groups ambayo inahitaji uzoefu wako na herdman. Utahitaji pia dume lenye umri wa miezi12 au zaidi. Pia kwa mtu anaeanza ufugaji inasumbua kidogo. Lakini ni nafuu kidogo interms of upfront capital though gharama za ufugaji zinaWEZA kuwa kubwa. Utahitaji kuanza nao wengi pia ili kupata faida na utahitaji kufuga muda mrefu kama nilivyoeleza hapo juu.

Kama una mpango wa muda mrefu na mtaji wa kugharamia chakula na mengineyo kwa muda mrefu,hii ni namna nzuri pia.

Kwa mtu anaetaka kufuga kibiashara,mie humshauri option 8(a) hapo juu
Shambani kwangu Morogoro kwa sasa nguruwe wa 2 au 3 wanazaa kwa mwezi. Kuanzia November nguruwe 5-7watazaa kwa mwezi.

Hope hii itawasaidia watakaopenda kujaribu hii project. Ni muhimu kutembelea mfugaji halisi kupata uzoefu kabla ya kuanza ufugaji.

NYONGEZA1
Mojawapo ya vitu watu wanakosea wakati wa kuanza ufugaji wa nguruwe ni uchaguzi wa mbegu bora.Wengi anapotembelea mtu anaefuga na kukuta nguruwe wakubwa wanapata hamasa bila kuuliza maswali muhimu yatakayomsaidia kujua kama mbegu anayoona inafaa.

Mtu anaefuga kibiashara huwa na:majike na dume(au madume kutegemea na idadi ya majike).Lengo ni kuzalisha nguruwe wa kutosha watakaokua haraka na pia kuwa na nyama nzuri(isiyo na mafuta mengi) wakati wa kuuza akiwa na miezi 6 au 7.Ni vema basi ukjua sifa za jike na Dume!

Dume:iwe mbegu inayokua haraka na kuzalisha nyama nzuri.unapochagua asiwe na ulemavu wowote na awe na matiti 12 au zaidi. Large white,duroc,hampshire na crosses zake zinafaa.Ukiweza kupata first cross za duroc au hampshire ni wazuri zaidi kuwatumia kama terminal sire(dume wa kuzalishia nguruwe wako wa mauzo)

Jike:awe kutoka mbegu zinazozaa watoto wengi na pia uwezo mzuri wa kulea watoto.Awe na matiti 12 au zaidi.ni vema kutoka kwenye crosses za largewhite na landrace.Pia saddle back na crosses zake.

Kwa leo ni hayo.nitaendelea ku-update hii thread ninapokuwa na muda kwa topic mbalimbali.Ninatambua kuna breeds nzuri zaidi kama camborough,etc.nilizoelezea hapo ni breeds unazoweza kupata kirahisi humu nchini.

mawasiliano:0789412904,simu isipopokelewa andika msg ,utapigiwa

Pia angalia Mbegu nzuri ya nguruwe sasa inapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

HABARI ZA 2016.
NNA WATAKIA UFUGAJI WENYE MAFANIKIO WALE WOTE WALIONUFAIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA UZI HUU!2016 UWE MWAKA WA NEEMA KWENU!


Kuna huu Uzi nimeuforwad ni WA humu ni mzuri sana upitie
 
Njoo nikuuzie mbegu za nyasi za kulisha mbuzi wako
Juncao na Super napier

IMG_20230428_072832_072.jpg
IMG_20230426_175321_546.jpg
IMG_20230208_090717_957.jpg


Eka moja ukiitunza vizuri unaweza kuvuna 200 za majani mabichi kwa mwaka ambayo yanatosha kulisha mbuzi zaidi ya 50.

0756625286.
 

Attachments

  • IMG_20230428_072835_637.jpg
    IMG_20230428_072835_637.jpg
    121.5 KB · Views: 42
Habari wapambanaji?
Mimi ni kijana mpambanaji,katika kilimo cha mahindi na alizeti,ila mwakan nataka nijikite zaid kwenye ufugaji wa nguruwe na mbuzi wa nyama,nimewajia hapa ili kupata experience pia ushauri,nina ekari mbili nataka 1½ nilime mahindi,alizeti na maboga at least gharama za ulishaji zipungue na sehem itakayobakia nijenge mabanda yao! mwenye mawazo ushaur karibu sana, Asante!
Karibu 2023
Mapinduzi ya Ufugaji wa Nguruwe Tanzania.

Direct Whatsapp - Xiānshēng 大卫, 名尼亞 Muwekezaji / Entrepreneur / Investor

1. WhatsApp Group Mapinduzi ya Ufugaji wa Nguruwe Tanzania

2. WhatsApp Group Uza au Nunua Nyama ya Nguruwe Tu Hapa

3. Bei Facebook anmelden

4. Messenger

5. Messenger

6. Bei Facebook anmelden

7. Bei Facebook anmelden

8.

9. Wateja wa Nyama Ya Nguruwe

10. Wateja wa Watoto wa Nguruwe wa Kisasa wa Mbegu

Instagram - @Nyamayanguruwee
Facebook Account - Nyama Ya Nguruwe
Facebook page - nyamayanguruwe

1. Ninauza Watoto wa Nguruwe wa Kisasa wa Mbegu
Madume na Majike yanapatikana hapa
Bei ni Tshs 200,000/= - Tshs 2,000,000/=
Bei Inategemea na Mbegu au Umri wa Nguruwe utakayemuhitaji.

NB:- Ukinunua watoto wa Nguruwe Tenga la kuwaweka kwa ajili ya kuwabeba au kuwasafirisha utapata Bure kwa idadi yoyote ile ya watoto wa Nguruwe utakaonunua hapa shambani.

2. Ninauza Nyama ya Nguruwe kwa bei ya Jumla Kilo moja (Kg 1) ni Tshs 8,000/= - Tshs 8,500/=

NB:- NINAHITAJI Wateja wanaonunua nyama ya Nguruwe NA KULIPA hela Papo Hapo au CASH. Kuanzia Kilo 5, kilo 10, kilo 20, kilo 30, kilo 40, kilo 50, kilo 60, kilo 70, kilo 80, kilo 90, kilo 100, kilo 150, kilo 200, kilo 250 nakuendelea

👉🏽Nyama ya Nguruwe kwa bei ya Reja Reja Kilo moja (Kg 1) ni Tshs 9,000/= - Tshs 10,000/=

*SPECIAL ORDERS *
RIBS / Mbavu Tu Kg 1 - ni Tshs 12,000/= - Tshs 15,000/=
Stake Tupu / Steak Kg 1 - ni Tshs 12,000/= - Tshs 15,000/=
Maini Kg 1 - ni Tshs 10,000/=
Kichwa Kg 1 - ni Tshs 3,500/= - Tshs 4,000/=
Miguu Pair 1 - ni Tshs 4,000/= - Tshs 5,000/=
Matumbo Ndoo Kubwa - ni Tshs 15,000/= - Tshs 20,000/=
Mkia Kg 1 - ni Tshs 3,000/= - Tshs 4,000/=

3. Ninachukua Nguruwe wa kuchinja Dar es Salaam na Pwani. Kwa kila kilo moja (Kg 1) utalipwa Tshs 6,500/= mpaka Tshs 7,000/=

NB:- Popote Dar es Salaam na Pwani nitakuja kuwachukua Nguruwe BURE! - KAMA NGURUWE WAKO WAPO KARIBU NA MAHALI NILIPO.

4. Ninauza Mbolea ya Nguruwe
Ujazo wa Suzuki Carry Kg 350 ni Tshs 100,000/= Tu.

NB:- Kama ni Karibu na Shamba usafiri ni bure. Kama ni Mbali na shamba Dar es Salaam na Pwani usafiri upo kwa Gharama ya Mteja.

5. Nguruwe wenye mimba ni Tshs 2,000,000/=

KUMBUKA Kwa huduma yoyote ile utakayoihitaji hapa, Delivery Dar es Salaam na Pwani ipo kwa Gharama ya mteja.

Kwa Mawasiliano
Tel: +255716576827
Email: Nyamayanguruwe@gmail.com
Location: Dar es Salaam, Bunju B, Mabwe Pande, Manzese

Mapinduzi ya Ufugaji wa Nguruwe Tanzania.
#daressalaam #nguruwe #watotowanguruwe #watotowanguruwewakisasa #nguruwebiashara #piglet #piglets #pork #ham #swine #pigs #pig #delivery #tanzania #pigfarmer #pigfarmers #pigfarmerslife #mapinduziyaufugajiwanguruwetanzania #nyamayanguruwe
#porkrecipe #pigfood

Karibu tufanye Kazi.
2023
 
Back
Top Bottom