Malecela: kuweka mihula kwa wabunge ni kukiuka Demokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela: kuweka mihula kwa wabunge ni kukiuka Demokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 29, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  27/01/2010

  [​IMG]

  Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa siku nyingi John Malecela amesema mjadala wa kuweka ukomo kwa wabunge wa Tanzania, waachiwe wananchi ambao ndio wanajua nani anastahili kuwawakilisha.


  Malecela ambaye ni miongoni mwa wabunge waliokaa kwa muda mrefu katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema kwa ufahamu wake wa siasa za kimataifa hakuna nchi duniani inayoweka ukomo kwa wabunge kukaa madarakani akitolea mfano wa Marekani, Uingereza, Urusi na China.

  Malecela amesema katika bunge la sasa la Tanzania karibu asilimia 80 ya wabunge ni vijana na haelewi kauli zinazotolewa kuwa wabunge wengi ni wazee zinatoka wapi.

  Aliwataka wananchi wanaozungumza hivyo kufanya utafiti wa kina badala ya kuropoka kwenye vyombo vya habari.


  Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wadau mbali mbali nchini Tanzania wakitaka kuwepo na ukomo wa kipindi cha ubunge nchini humo, ili kutoa fursa ya mawazo mapya katika bunge hilo, na hasa baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mizengo Pinda, kusema kuwa yeye anaona kuna umuhimu wa kuwa na ukomo wa mbunge kukaa bungeni.

  http://www.voanews.com/swahili/2010-01-27-voa2.cfm
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  I agree with him 100%. Let the people kick out the wabunges who they are not satisfied with.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini Rais ameweka kikomo? Je si ukiukwaji wa demokrasia huo?
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Ukomo ni muhimu.Kwani kauli ya wabunge wakongwe kupenda kungangania kwa kauli ya jimbo langu zinatia mashaka.Je rais angesema hiki ni kiti changu ingekuwaje? Come on!!!!!! fungua macho.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mambo haya ya kudai ukomo yanatokana na chaguzi zetu kutokuwa/kutoonekana kuwa HURU na HAKI. Mapesa ya ajabuajabu yanatumika kwenye kampeni, wakishachaguliwa wabunge wakapata nafasi za uwaziri wanaitafuna nchi kwelikweli, utawaondoaje hawa bila kuweka ukomo?
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ingawa mimi sio muumini wa siasa, lakini statement yako imeweka msingi mzuri wa ku-reason hii hoja. Kama kuna ukomo kwa URAIS, kwa nini kusiwepo na UKOMO ktk nafasi nyingine za kisiasa?? Au kinyume chake??

  Jibu nadhani mnalo nyie mnaoamini ktk hii version ya 'siasa' za kibongo.
   
 7. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Malecela hana pointi kabisa, swala la nchi zingine kutokuwa na ukomo halina maana, au sisi watanzania hatupaswi kubuni, yaani tunacopi na kupaste tu? Mtu akiingia bungeni anavuna pesa zitakazomhakikishia kurudi baadaye na kutamka "JIMBO LANGU"! Je, iwapo mbunge anatoka tu kwa hiari yake, au kwa kifo, lini maovu yake yataonekana na kuchukuliwa hatua? Tena ningependekeza kuwa na kikomo hicho, lakini sio kikomo cha kuchukuliwa hatua kwa wizi na maovu aliyofanya akiwa madarakani.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nitaenda mbele zaidi.. kwanini tumeweka umri wa kustaafu tena tunatumia neno "kwa lazima"..?
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hi mifano siku zote huwa mizuri when they work for but when they work against hawa wakuu huwa hawakawii kuruka na kusema ooh! hapa sio Marekani au UK, we are still a young democracy, we have to do things on our way etc. etc.

  Sasa on this hata kama hakuna sehemu nyingine zinafanya hivyo kwa nini sisi tusiwe wa kwanza????? Ili na wengine wajifunze kwetu????????
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Angalau sio kwenye siasa. Ni namna tunavyochaguana tu ndio inaleta taabu na mbaya zaidi tunavyoenenda baada ya "kuchaguliwa".
   
 11. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Bunge ni chombo cha watu wengi,kunatakiwa kuwe na mchanganyiko wa vijana na wazee. Ila vijana wanatakiwa wawe wengi zaidi kuliko wazee. Lakini sulala la ukomo wa umri ni muhimu. Wazee waliostaafu kazi zao kwa kufikisha miaka 60 hawatakiwi kuwa wabunge kwani ile siyo sehemu ya kupumzikia ni sehemu ya kuchapa kazi kama sehemu nyingine.

  Ni mtazamo tu wanaJF msijenge chuki
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  N.Y.C. Mayor Bloomberg's run for third term approved by Justice Department

  By Carly Rothman/The Star-Ledger

  March 17, 2009, 12:55PM

  [​IMG]

  AP Photo/Henny Ray Abrams

  New York Mayor Michael Bloomberg has been given approval by the Justice Department to seek a third term.

  NEW YORK -- The federal government has approved Mayor Michael Bloomberg's change to city term-limits law, clearing the final hurdle for the billionaire to run again this year. Under the Voting Rights Act, the Justice Department must approve changes to voting rules in New York City.


  Last fall Bloomberg got the City Council to approve an extension to the city's term-limits law so that he could run for a third consecutive four-year term.


  The Justice Department's ruling was the final obstacle.


  - Demokrasia ni wananchi na sheria, sio political desparations za wananchi wasiojua tatizo lao liko wapi kiuongozi kama sisi, ifike mahali tukubali tu kwamba we have no clue nini maana ya kiongozi anayefaa na asiyefaa,


  - As the results, toka tupate uhuru tumekubali kuwapa viongozi wasio na uwezo sio tu kutuongoza, bali kuwaruhusu kujifunza uongozi wakiwa kazini, hili taifa tumekwama sio kwa sababu yoyote nyingine ila uwezo wetu mdogo wananchi wa uelewa wa siasa, demokrasia tunayo lakini tumeshindwa kuitumia kwa faida yetu wananchi, sasa tumebaki kunyooosheana vidole tu!  Respect.

  FMEs!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unajua.. FMES right on the money.. ukifiria sana tatizo wala siyo ukomo au muda mrefu tatizo ni sisi wananchi tunataka au hatutaki? Meya Bloomberg angeshindwa ndiyo ingekuwa hivyo.. nadhani at the end of the day it all rest with the voters.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Tizama wanaojua maana ya demokrasia hapa chini, hakuna cha Obama wala nini, anapewa ujumbe mzito mapema sana kwamba jirekebishe ama sivyo ni rais wa term moja tu, kwa kupitia kwenye kura, sio matusi na kelele zisizo na anything ndani yake kwa masilahi ya taifa:-
  Republican Brown beats Coakley in special Senate election in Massachusetts

  [​IMG]

  Brown's win deals blow to Democrats


  Republican Scott Brown is now the Senator-elect from Massachusetts, winning the seat once held by the late Sen. Ted Kennedy. Brown's victory over Martha Coakley puts the fate of many Democratic initiatives up in the air.
  [​IMG]


  [​IMG]
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani kuna maswali hatujiulizi hapa.

  Je, majukumu ya 'mwanasiasa' mathalan mbunge ni yepi??

  Je, majukumu hayo yana mahitaji gani kuanzia elimu, uwezo wa kimwili na kiakili etc??

  Kama tukiweza kuyajibu haya maswali kwa ukamilifu tunaweza ifunga hii mada kwa wepesi zaidi.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Hapa chini ni namna ya upinzani na wananchi kutumia demokrasia ili kushinda uchaguzi, sio maneno mengi ya hewa na siasa za majina:-   
 17. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani naomba tuache kuchanganya mada hapa, ishu sio ujana wala uzee mheshimiwa WM Pinda amesema kuwepo na ukomo wa vipindi vya kukaa bungeni akimaanisha kuwa kama wewe una miaka 33 ama miaka 55 ukishatumikia vipindi vyako 3 then unaachia wengine simple and clear!!

  Amani.
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Baadhi ya maeneo hapa Tz wameanza kutambua nini maana ya uchaguzi na nani anawafaa kuwaongoza.Maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro, wilaya kama Tarime, Karatu,... huwezi kutumia pesa kununua uongozi. Wamefikaje hapo? Kwa nini majimbo kama ya Dar yako hivi yalivyo?
   
 19. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Pamoja na kuwa sikubaliani na utaratibu wa kufanya mambo kwa kuwa tu nchi nyingine hufanya hivyo, nakubaliana sana na haja ya kuachia wananchi waamue mwakilishi anaewafaa.

  Nakubaliana na haja ya kufanya hivyo kwa kuwa, Wabunge si watendaji, bali ni wawakilishi wa wananchi. Hivyo wananchi wanatakiwa waachiwe uhuru wa kuamua nani awawakilishe katika kutoa maoni, mahitaji na mapendekezo yao kwa serikali.

  Vile vile, Wabunge wa JMT wako zaidi ya 300. Kwa mtazamo wangu nafasi hizo ni nyingi kutosha kila mwenye kutaka kupata nafasi (kama anaonekana kufaa) ya kuwa mwakilishi wa wananchi atakaochagua kuwawakilisha. Hakuna uhaba wa majimbo ya kuwakilisha, hivyo hakuna haja ya kusita kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge.

  Kwa upande mwingine, nafasi ya Urais haifanani kabisa kiutendaji na nafasi ya Ubunge, hata katika ngazi hizo tofauti. Mamlaka ya Rais, majukumu yake na uwezo wa Rais ku-affect maisha ya waTanzania ni mkubwa sana kuliko wa Mbunge, au hata wabunge wote kwa pamoja. Nafasi ya Urais ni moja, nyeti, kubwa na yenye maslahi makubwa kwa Taifa. Inatakiwa iwe na vipimo na vikomo zaidi hata ya ilivyonavyo sasa.
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hana lolote anaona aibu kwani ameongoza mika mingi halafu bado anaendelea kutaka kuongoza....demokrasia ina Principles na mipaka yake...
   
Loading...