Malecela: Kingunge hana shukrani

Malecela: Kingunge hana shukrani

manizzle

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2015
Posts
3,421
Reaction score
4,323
Malecela.jpg
Mwanasiasa mkongwe wa CCM mzee John Malecela amemshangaa mzee Kingunge na kumuita Yuda na msaliti, ndumilakuwili na mchochezi na hana shukrani hakumbuki alichofanyiwa na serikali ya Kikwete huyu Kingunge.

Anakusanya ushuru stendi ya Ubungo na maeneo mengine ya mji hela anazokusanya kila siku anampa nani au aliwashawahi kutoa msaada wowote kwenye kituo cha kulea watoto yatima? Mzee Malecela amesema Kingunge aache kabisa kuwachagulia mtu anayefaa kuwa Rais kazi hiyo ipo mikononi mwa CCM kwenye mkutano mkuu hata CHADEMA, CUF hufanya hivyo kwenye vikao vyao maalumu.

Mzee Malecela amesema kura ya veto iliyomtoa manyoya yeye wakati anagombea Urais ndio itakayotumika kuangalia mgombea mwenye Sifa zote zinazohitajika kwa Tanzania ya sasa na nyingine pia awe msafi, mpole, mchana Mungu mwenye maadili.

Malecela amesema Rais hawezi kupatikana kwa kelele za watu, porojo na maigizo; muda ukifika kila Mgombea atabeba msalaba wake.

Kwa matendo waliyoyafanya kugawa watu kwa kuwanunua kwa uchu wa madaraka, mbegu hiyo ni mbaya sana kwa Taifa kwani kuna uwezekano Taifa lilitagawanyika tusipokuwa makini na wasaka urais kwa nguvu.
 
amesema hayo akiwa wapi? tuseme wao watapigana UKAWA watapita katikati
 
Huyu mzee ameshajifia, hata darasa la saba likamwangusha. Time will tell na kura ya VETO tuone kama inaweza zuhia mafuriko
 
Huyu kamshindwa Lusinde yule kichaa atawezana na Lowassa kweli kwa mziki tuliouona jana! Hii ngoma ya magamba lazima ipasuke mwaka huu. Naona karata pekee waliyonayo wapambe wa Membe ni kumkata jina Lowassa kabla hajafika mbali, sidhani kama atakubali kwa nilivyoona jana
 
Teeeeh,teeeeh,teeeeh,vita yapanzi faraja ya kunguru kwani hujipatia msosi ki ulaini,hivyo ukawa wawe tayari kukabidhiwa injhiii
 
Back
Top Bottom