Bwana Zero/Bi Centi 50/Mzalendo halisi/Hasara/Halisi/Mtumwitu/Jemba Jemba/Mwana-CCM/Mama Lao/Bigman.
Ninaomba nikujibu kama ulivyoomba, ni kwamba serikali ya Muungwana haijamaliza hata mwaka, kwa hiyo kwangu kuisakama ni kwa yale tu yaliyojitokeza katika kipindi cha mwaka mmoja, na cha muhimu ni Richimond, pia ninamsakama kwa ajili ya kutowafikisha kwenye sheria waliohusika na mikataba ya IPTL na Radar, otherwise bado ninampa nafasi zaidi ya kutawala kwa angalau miaka mitano ndio nimpe hukumu yangu, lakini in the meantime nitaendelea kumsakama kwa yaliyofanyika katika mwaka wake mmoja wa madaraka, ndio maana nilizilalia macho data za Richmond na zote ninazo, na nilishazifikisha zinapotakiwa!
Now, ngoja niguse subject ambayo ninatakiwa sana na wananchi hapa, ya kichwa cha hii mada, ninaamini kuwa imeletwa hapa na Mzee MMJ, ikiwa ni hasira ya kuguswa kwa Mheshimiwa Freeman, na bwana Wooh, kwa sababu siku zote Malecela ni mmoja wa viongozi ambao huwa ninawatetea kuwa ni safi, na mfano bora kwa taifa letu, yaani waliolitumikia taifa letu kwa karibu maisha yao yote kwa jasho na damu, na taifa letu kwa kuheshimu hilo limeamua kisheria, kumtunza kwa hali na mali mpaka atakapoitwa na muuumbwa wake, hiyo ni heshima kubwa sana kwa taifa letu, kama alivyosema Dr. Kaunda alipokuja siku ya kumsimika urais Muungwana!
Sasa labda nijaribu kuwalinganisha Dr. Malecela na Mheshimiwa Freeman, mwenyekiti wa Chadema, kuanzia na CV zao, na mambo yote waliyoyafanyia taifa letu ili kuona kama kuna ukaribu wowote wa kuwahusisha kila anapoguswa Mheshimiwa Freeman, kwa kweli ningeomba msaada wako kuiweka CV ya Mheshimiwa Freeman, ambayo sina ila nitajitahidi kuitafuta, na pia za viongozi wote wa upinzani na nitaziweka hapa, ili tuone ukweli wa mambo, na baadaye tutahamia kwenye legacy zao kwa taifa letu kisiasa, na hasa kiuongozi, baada ya kumaliza hii post nitaanza kuyashughulikia hayo, na nitaendelea na hizo series, pole pole sina haraka, unajua niko vacation kwenye visiwa lakini inabidi niwatumikie wananchi hapa ambao huwa hawa-get enough of my political views na vigongo pia, maana sasa pm yangu huwa imejaa kila siku wakitaka more, sina noma nitawapatia tu wananchi!
Sasa kuhusu, chanzo cha hiii drama, DR. WHO amesema maneno yake au maoni yake kufuatia kauli ya Mheshimiwa Freeman, kuwa afadhali kuwa chini ya mokoloni kuliko kutawaliwa na serikali iliyochaguliwa kwa kura za wananchi Asilimia 80%, against Aslimia 9& za chama cha Freeman!
Sikubaliani na matusi yaliyoambatana na hoja za Wooh, lakini ninaheshimu msimamo wa kusimama mbele ya forum ya Chadema na Freeman, na kusema ukweli, in fact Wooh alitakiwa kuihoji kauli tu bila matusi, na wenye forum walitakiwa kuyafuta matusi na kuacha hoja ili zijibiwe kama zilivyotolewa na Wooh, na ndio kilichonivuta pamoja na kuwa kwenye mapumziko mazito huku kwenye bahari, kilichonitisha ni kutolewa kwa ile topic, mpaka leo bado sija-recover na ule mshituko, sikutegemea hata siku moja this forum itakuwa capable wa kufanya kitu cha ovyo kama kile, na sidhani kama nitakuja ku-recover tena na ule mshituko, na maneno yako Mzee Zero, lakini pia ninaheshimu sentesi yako moja kuwa "...nani aliyekuambia kuwa hii forum ni ya wananchi, au una haki na hii forum?.....", kwangu hayo maneno yalikuwa ni deep!
Kwako Mheshimiwa Freeman, ninaamini kiongozi wa siasa wa nafasi kama yako, huwa ana washauri wa kumshauri cha kusema katika siasa hasa hadharani, kwa kweli ningekuomba uwafukuze kazi hao washauri wako ndugu yangu, kweli wabongo sisi ni wajinga kisiasa, lakini sio mpaka kwenye line za kutokujua faida na hasara za kutawaliwa na mkoloni, au wananchi wenzetu ambao huwa tunawachagua kwa ridhaa zetu wenyewe tukiwa huru bila ya kutishiwa bunduki!
......Itaendelea..........