Malecela and Dr. Salim - Into Oblivion?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
a. Sababu ya kwanza na ya msingi ni kuwa Mzee JM ni kiongozi aliyeshindwa. Hakuna kiongozi mwingine yeyote katika historia ya Jamhuri yetu ambaye ameshindwa kiuongozi kuliko Mzee JM. Katika muda wake wote wa uongozi akiwa ameshika nafasi nyingi sijui ni kitu gani alichokifanya (na watu wakakiona) na kuacha alama nzuri ya kukumbukwa. Hapa sizungumzii mambo yanayofanywa kwa siri au nyuma ya Pazia. Hivi ukimuuliza Mtanzania wa kawaida akuambie ni kitu gani alichokifanya Malecela ambacho Taifa litamkumbuka kwacho (zaidi ya nafasi za uongozi na kugombea nafasi Urais) ni nini atakutajia? Ukiwauliza watu hivi Mrema alifanya nini, Mwinyi alifanya nini? Warioba alifanya nini, au Kawawa, Salim etc kuna vitu kadha wa kadha ambavyo vitawajia kichwani. Labda wananchi wa Mtera wanaweza kutupa majibu

b. Alishindwa kuitetea Ilani ya CCM na sera ya CCM juu ya Muungano ilipoibuka mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kama kuna kitu ambacho kimetia doa kubwa la kiuongozi dhidi ya Bw. Malecela ni kushindwa kwake kuizuia hoja ya Tanganyika kujadiliwa Bungeni yeye akiwa ni Waziri Mkuu. Kama kuna kitu ambacho kitamfuata mpaka kaburini ni jinsi gani alishindwa kabisa kutetea msimamo wake huo dhidi ya mashambulizi yaliyoongozwa na Mwalimu. Kama ni mtu mwenye msimamo basi wakati ule ndipo angeonyesha uwezo wake wa kutetea hoja (kumbukua alikuwa na wabunge 55 nyuma yake). Hoja ya Mwalimu ilikuwa ni kama anayoitoa Mhe. Mzee Es hapa, kuwa ni lazima kufuata Katiba ya Chama na Ilani ya Chama, na kitu kingine nje ya hicho ni uzandiki na usaliti. Sera na Ilani ya CCM ni kuwa na Serikali Mbili. Kitendo cha Mhe. Malecela kuruhusu wabunge wa CCM kujadili serikali tatu kilikuwa kisichosameheka! Hayo yote yalisababishwa na kuthubutu kwa Zanzibar kujiunga na ile Jumuiya ya nchi za Kiislamu. Badala ya kuvunja hoja na kuweka msimamo wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Malecela akaungana na Wabunge wengine wa bara (kundi 55) kudai "Tanganyika yao".

c. Mzee JM hana jipya. Licha ya madai ya kuwa Mzee huyo anaheshimika sana ndani ya Chama, inaonekana bila ya shaka yoyote, mvuto na heshima hiyo ni hewa. Ameshindwa kujitetea kikamilifu au kujenga hoja zinazoonyesha msimamo wake zaidi ya kukaa chini na kuendelea kupigwa ngumi kulia na kushoto na watu ambao wanaendelea kuimba sifa zake lakini pembeni wanaendelea kumbomoa kisiasa. Baada ya varangati la IOC, Muungano, madai ya Mwalimu dhidi yake, kuenguliwa hatua za mwanzoni, Mzee JM anaendelea kuamini (au kuna watu wanamtaka aamini..) kuwa ana mvuto mkubwa na nguvu kubwa katika Chama. Ukweli ni kuwa Mzee JM hana nguvu hizo isipokuwa ana heshima ya kusikilizwa tu!

d. Amefanya kila aliloweza ndani ya ubinadamu wake kukitumikia chama na Taifa. Ni wakati umefika wa kumuachia mtu mwenye mawazo mapya na nguvu mpya kuungana na timu mpya ya Kikwete katika kutelekeleza majukumu ya chama. Ni kweli alitaka kujiengua huko nyuma lakini "akabembelezwa" akaamua kubakia. Kuna watu ambao wanamfanya aamini kuwa bila yeye CCM itayumba. CCM ni zaidi ya Malecela, Mkapa, RA, EL, EN etc. Itakuwa ni kitendo cha kimahiri na cha kisiasa kuachia umakamu kwani atakaa pembeni na kuona jinsi gani CCM itajaza nafasi hiyo. Sitaki Mzee JM awe kama mzee aliyezoea kusimamia watoto wake kwa kila kitu hadi wamekuwa na nyumba zao lakini bado anaendelea kuendesha maisha yao. Hadi siku mzee huyo anakaribia kufa anabakia kujiuliza kama aliwaandaa watoto kuishi pamoja vizuri. Mzee JM asije akabakia kujiuliza hivi kweli nikiondoka itakuwaje kwenye CCM. Atafanya kitendo cha Kimapinduzi akiamua kung'atuka na kuwaachia kizazi kipya (siyo lazima wawe vijana) kuanza kushika hatamu za uongozi wa Chama.

Ni kwa sababu hizo nne, ninasema kuwa, Mzee JM aamue kustaafu kwa manufaa yake binafsi na kwa ajili ya kukipa Chama nafasi ya kujaza nafasi hiyo kwa wakati mmoja na ile ya Uenyekiti. Atajifanyia mwenye fadhila na familia yake. Anaweza kuendelea kuwa Mbunge wa Mtera na kumaliza kipindi chake lakini hana sababu yoyote ya msingi ya kuendelea kuwa M/Mwenyekiti wa CCM (Bara). Aanze kupumzika kabla baiolojia haijamlazimisha.
 
You are right. Tatizo ni kuwa kuna CCM nyingi, na Mzee E.S. yupo katika moja tu ya ccm kibao zilizopo. Kwa hiyo hawezi kujua kila kitu katika CCM. Atayajua yale yaliyo kwenye CCM yake tu!
 
Kimsingi ni sababu moja tu inayompa Dr. Malecela uhuru wa kuendelea kuwa Makamu wamwenyekiti wa CCM mpaka mwaka 2007, nayo ni kuchaguliwa na asilimia 99.9% ya wanachama wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho mwaka 2002, kilichofanyika Dodoma. Kwa katiba za chama hicho cha siasa anatakiwa kuongoza hadi mwaka 2007,

Sasa gazeti au mtu yoyote yule anayeshauri tofauti ni mzandiki au antaka kutupotosha wananchi wengine wote kwamba hatuna akili ila yeye anazo nyingi zaidi, which is not true, Dr. Malecela ambaye pia ni Chancellor wa Dar Open Universty na mbunge wa Mtera, ni mtu mzima licha ya kuwa kiongozi na mwenye akili timamu ya kuweza kusema kama anataka kujiuzulu au hapana, hahitaji ushauri wa wanasiasa uchwara, au ushauri wa wanaomchukia bila sababu za msingi ila kwa sababu wana nafasi ya kuandika kwenye mtandao basi wameona ndio tiketi ya kumvunjia heshima kiongozi yoyote yule ili kupata umaarufu wa kwenye mtandao.

Yes hatimaye EL atakuwa makamu wa mwenyekiti, tayari mazungumzo na mikakati imeshapangwa, lakini mpaka mwaka mwaka 2007 sio sasa au June! Tujifunze kuheshimu Demokrasia, tunajua kuwa mzee huyu huko nyuma hakuwa mstaarabu na akina mama, sasa inaonekana kuna kati yetu ambao huenda mama zetu walipitiwa na huyu mzee bila "Ahsante", sasa tuvumilie tu maana ndio dunia lakini sio kumlazimisha kiongozi wa umma kujiuzulu, huo ni uzandiki na unafiki kwa wale wasio wanachama wa CCM, ni kiapo niliapa siku zote kuwa kiongozi bora hatatukanwa hata siku moja bila ya mimi kujibu unless awe kiongozi mwizi na mla rushwa kama BM!
 
Eeeeh mheshimiwa karibu!
Kulikoni?... kwani kuna watu wanaotaka Malecela ajiuzuru!... mbona hata sielewi hii picha! Malecela ajiuzuru kitu gani ambacho kinamkereketa mwananchi.
 
Ahsante Mzee Bob, na heshima kwa wazee wote wa bodi hii, Wazee kumradhi ninapita tu sio mhamiaji, lazima niwe mkweli hii forum kwangu ni baridi mno, ni forum kali na ya heshima no Question or butts about it ila bado ninasubiri itakapotokea, yaani yenye fimbo na mawe na mavitu, bwana Filga kudos, ila nitapita tu ikibidi otherwise heshima mbele wakuu! bado niko US, mpaka mwisho wa wiki hii ndio nitarudi bongo tena baada ya kama miezi miwili huku majuu kusafisha macho,

Mzee Filga heshima Mkuu tena, ila tu nitoe salaam kwa wakuu wote wanaonitumia message mbali mbali kuwa zimefika na heshima kwenu wote, hatuna kijiwe kwa sasa, lakini ninaamini kinakuja karibuni na guess what? yaani nina mavitu mpaka yanataka kuniangusha ninasubiri kuyamwaga!

Haya mzee Filga na wazee wote heshima mbele!
 
Mzee wa meli,

Punguza Munkari basi:) naona umekuwa mbogo. Kweli umevinjari mara ya mwisho kupata habari ulikuwa unaondoka uingereza.

Kijiwe kimeota majani, hatuelewi pa kuamini, mi sina imani na vijiwe vilivyopo kwa sasa, nimekuwa msomaji kuliko kuandika.

Njia ya kuwasiliana ni ile ile ya kwenye vijiwe hivi.

Keep well

FD
 
Mzee Es,

Kwa nini umethubutu kumtukana Mkapa lakini? Yeye ni Rais mstaafu, na kwa hali hiyo sio sawa hata kidogo kumtukana.

Mzee Malecela kazi kubwa aliyofanya CCM ni kusimamia chaguzi sehemu zilizoonekana ngumu (kama kwa Cheyo). Amebobea kwenye fani ya wizi wa kura.

Mzee Malecela alishawahi kuwaambia vijana wa CCM: mwana upinzani akikupiga kofi moja, wewe mrudishie mawili. Yaani ni mhamasishaji wa mapambano ya wenyewe kwa wenyewe. Hatari sana.

Anyway, unaweza kumpenda, lakini wacha kabisa kumtukana Mkapa. Tuko wengi ambao tuna macho na tumeona na kutambua jinsi Mzee Mkapa alivyojenga uchumi wa Tanzania. Amewapiku sana Musa (Mtumishi wa Mungu) na Mzee Ruksa.

Kuhusu kijiwe kinachowafaa akina sisi, nashauri tuhamie hapa na tupajenge sisi wenyewe. Tusisubiri mtu mwingine apapashe moto.

Tunasubiri kwa shauku michango mingi na yenye faida kwa taifa toka kwako.

Augustine Moshi
 
Mzee Moshi,

Heshima mkuu, Tatizo la nchi yangu ambalo ni nambari moja ni UMASIKINI, uliosababishwa in part na sisi wananchi lakini part kubwa ni viongozi waizi na walal rushwa, ndio wameiua nchi yangu mpaka leo ninapewa umeme kwa mgawo, kiongozi wa serikali ametoa wapi dola 650, 000 za kuweka nje ya nchi?

I have no beef na Mkapa, isipokuwa tu aliyoyafanya mwishoni ni aibu na ndio maana anaomba kuondoka CCM maana aliofanya nao rushwa wako madarakani ndio maana pia wanamdharau mno, hata hawezi kukaa nao meza moja kwa sababu ya aibu, Malecela hamkimbii mtu kwani hana sababu hajamwibia mtu, kuhusu wizi wakura sijui maana hebu uliza kama ni rahisi kumuibia mzee Mapesa kura katika jimbo lake, sina mapenzi na kiongozi yoyote bongo ila kati ya maraisi wote nina heshima na mzee Jakaya, kwa kuweza angalau kuwafukuza kazi baadhi ya viongozi wezi na ninasema bado afukuze wengine pia na awafunge akianzia na Mkapa, Kigoda, sumaye, Yona, Ngwilizi, Idd Simba, Mbilinyi, Mahalu, Makamba, Ditopile, Rita, Janguo, hawa wafunguliwe mashitaka na ikibidi wafungwe kama Nguza, bila huruma kwa kuturudisha nyuma kwa miaka zaidi ya 50 kutokana na wizi wao au kuwasaidia wezi,

Malecela ni mmoja tu viongozi watatu ambao CCM tumeamua kuwa watakuwa ni wa kudumu mpaka wanakufa, nao ni Mwalimu, Mzee Kawawa, na Malecela, hawa ni viongozi mpaka wanaenda kaburini kutokana na michango yao mizito ambayo sisi CCM tunaiheshimu Daima.

Nimeusikia wito wako lakini, as much as ningependa kuwemo humu lakini my soul inaniambia hapa sio penyewe, na hapo juu unaona mzee FD ameshaanza kulia kuwa nimekuja mkali mambo madogo tu, je yakianza makubwa,

anyway shukrani!!!! na CCM juu, Kikwete safi! Saaaaaaaaafi Saaaaaaana!
 
Mzee wa Meli,

Kati ya uliowataja hapo juu kidogo Idd Simba ni enterprenuer, anaweza hata akadanganya au akaeleza na ukakubali amepatajae fedha zake.

Ila hao wengine??!! Juzi nimeonyeshwa apartments za mama BWM baada ya kuvuka daraja ukitoka ubungo ukielekea Mwenge kama mita 150 kulia. Nikatingisha kichwa.... Mi nimechoka na ahaadi za JK, ni lazima waanikwe hadharani, hii ya kuwafuatilia kimya kimya sijaipenda, HAIWI MFANO KWA WENGINE WOTE WENYE KUIBA FEDHA ZETU WALAL HOI.
Halafu muulize Augustino Moshi Nyumba nyingi za Mikocheni zimejengwa lini na ni nani mmiliki? asilimia 60 zinamilikiwa na watumishi wa serikalini ambao mishahara yao ni take home ya 150,000tzs mpaka 1,200,000Tzs
Watoto wanasoma ulaya, wanalipa DSTV etc

Bwana Moshi Acha mzee acha tu!!

FD
 
Mzee Es,
Kweli ndugu yangu inabidi tuamini maneno yako maana mwenzetu soko lako kubwa sanaaaa! mshikaji endelea kipaji Mungu kakupa cha kuweza kuwa karibu na ardhi kuyasikia matukio yote yanayokuja na yakitopita.
Hiki kijiwe ni chetu...Tunamchukia sana Mkapa kuuza nchi lakini isiwe sababu ya kutuzuia kutoweka fedha zetu benki. Kwa maana hiyo mshikaji teremsha manyanga hapa itakuwa benki na faida yake itawakuta wanao na Wadanganyika wote... Thawabu unazizoa mwanangu kwa kusema yale yasiyotakiwa kusemwa eti siri - Na waswahili huita uongo, kesho hawatakuwa na pa kuuficha uso wao.
Mshikaji nawaita wote jamaa na marafiki Mzee karudi!
 
Mzee ES,

Kama Mkapa alifanya mambo ya rushwa na watu ambao unasema wako madarakani, basi itabidi na wenyewe waone aibu sana. Umetoa shutuma bila ushahidi. Hizo dola nusu milioni unazosema anazo benki sio ushahidi. Anaweza kuwa nazo kutokana na savings zake za miaka mingi, na zawadi. Mtu anayestaafu Urais anaweza kupewa zawadi ya hata dola milioni moja.

Unamtaja Mzee Kawawa kama ni mmoja wa watu ambao CCM mnataka awe madarakani mpaka afe. Mbona hayuko tena madarakani, na kufa ni bado kabisa? Sioni vibaya Malecela akiendelea kuwa kiongozi wa CCM, lakini naona vibaya CCM kuendelea kuongoza. Haina tena dira. Matatizo sugu yanayowaelemea Watanzania wa leo, yamelelewa na CCM kwa miaka mingi. Matatizo ya maji, umeme, rushwa, jeshi lenye wezi na lisilo na nidhamu, porojo badala ya kazi maofisini, yote yamelelewa, na yanaendelea kulelewa na CCM.

Napenda kusema hivi kwa wachangiaji wote: Tuache kuchukia mali, na tusiwaonee gere wenzetu wanaotegeneza pesa. Ukapa sio usafi. Kama Mama Mkapa amejenga apartments karibu na Chuo Kikuu, basi tufurahiye hayo maendeleo. Inawezekana amekopa benki au alikuwa na fedha zake. Sisi tufurahie kwamba kwa kujenga hizo apartments amejenga nchi. Huo ndio uzalishaji wenyewe; tusiwe wa kuatamia tu umasikini. Au tunapenda aparments zote nzuri zijengwe na wageni? Wasipojenga akina Mama Mkapa, atajenga nani?

Inawezekana kabisa mfanyakazi wa serikali akajenga jumba. Kwani ukiwa mfanyakazi huwezi kuzalisha mali nyakati ambazo huko kazini? Kuna kufanya biashara, kufuga na kufanya consultancies za nguvu. Sio lazima wafanyakazi wa serikali waatamie umasikini.

Niliwahi kusema kwamba zipo sehemu Tanzania mtu ukijenga nyumba ya bati basi kijiji chote kinakasirika, na washirikina wanajaribu kukuloga. Msiyalete hayo Dar. Mwenzio akijenga jumba au apatment block, au akawa na fedha nyingi benki, usinungu'nike. Mwache awe nazo; ni mwekezaji mzawa. Kigumu Chama cha Mapinduzi!

Augustine Moshi
 
Augustine,

Naomba nikubaliane na wewe, ila tatizo lilipo ni kuwa kufanya kazi na kupewa nafasi serikalini kwa muda wa miaka 10 ndio upate mikopo ya ma bilioni ya hela?! Sipendi kurudia yaliyokwisha semwa, ndio maana nimetolea mfano hizo za ubungo, maana nyingine nyingi tu zilishatajwa na wewe kama ninavyokufahamu ulisha zisoma.

Umeshatembea nje ya Tanzania, naamini hivyo. Kwa wenzetu ukiwa unafanya kazi ya Tzs 1 Mio kwa mwezi wanategemea uwe na nyumba ya mtu mwenye kipato hicho. Kama umekopa (ambayo ndio standard nchi za nje) poa, maana utakatwa kwenye mshahra wako!

Naomba hapa niongee kiuchumi kidogo, Umeongelea miradi nje ya kazi zako za kawaida, OK, can we reconcile the income earned from those miradi from Tanzania revenue authority offices?, tukiangalia kodi uliyolipa huko tunaweza kuona hizo consultancy na hiyo miradi? Maana umeongelea mirazi ya kujenga/kununua maghorofa Ilala na sehemu nyingine.

Bwana mzee, kama ni chuki binafsi mimi sina na kiongozi yeyote, so far Mwalimu (RIP) alitutunzia madini kwa miaka yote ya utawala wake, ni zuri hilo, Mwinyi aliweka soko huria ni zuri hilo Mkapa alikuza Uchumi ambao sasa JK anauporomosha!, kwa hiyo mzee kuwa makini unapoongelea miradi.

Tunachosema ni mali isiyoelezeka iliyopatikana ndani ya miaka kumi!

Samahani Moderator nimeandika gazeti.

FD
 
Hiyo nusu millioni sio ya Mkapa, yeye ana zaidi ya hizo mara kumi labda as for the rest mzee unaonekana kuwa naive mno na wanasiasa wa bongo,

Waliompa rushwa hawana shida naye tena maana walikuwa wanatafuta madaraka by any means necessary, the end justfies the means hiyo ndio hasa uti wa mgongo wa siasa za bongo, hiyo dola millioni moja waliyompa kuyaweka sawa matokeo Dodoma tayari wamesharudisha, lakini ukweli unabaki kuwa hawana tena shida naye si unajua kuwa Mafarisayo walipompa Yuda zile hela za rushwa ili awapatie Yesu baadaye walimfanya nini? walimfukuza! je kuna tofauti hapa na hawa jamaa sasa wanavyomfukuza Mkapa?

Kama ni gere ya majumba ya mkapa na mkewe, ambayo wameyapoata kwa mikopo benki, ni sawa mzee ninaona na sisi wabongo tukazane, ili tupatiwe mikopo kama hiyo ya akiona Mkapa na mkewe,

gazeti moja bongo linasema kuwa kuna kiongozi mdogo tu wa CCM aliyekutwa na dola 650,000 huko majuu I maen labda naye ni za mkopo Mzee Moshi ninajua kuwa una akili za kuona more than mikopo, na ninajua una heshimika katika hivi vijiwe, hiyo mikopo inapatikana wapi?

Ok ngoja nikimbie wazee,!
 
Mzee E.S.: Tunaomba pia utueleze chanzo cha utajiri wa waziri mkuu wetu ukianzia na utitiri wa majumba aliyonayo kuanzia Masaki na yale aliyomalizia kuyajenga hapa karibu na Rose Garden nwaka 2004.

Ahsante.
 
Mzee ES,

Usijaribu kutetea kushuka kwa ukusanyaji kodi kwa sabubu za ajabu. Ukweli ni kwamba ukusanyaji kodi umeshuka kutokana na serikali ya sasa kuwa ni serkali isiyoweza kumudu uchumi. Inauporomosha kwa kasi ya ajabu kabisa. Nimetoa takwimu kwenye mada ya "MV Kiwete Inazama?"

Unasema Mkapa alihongwa kuweka matokeo sawa Dodoma. Kama hivyo ndivyo, basi itakuwa JK na ajenti wake Rostam, ndio wahongaji. Kama tuna Rais aliyeingia madarakani kutokana na kumhonga aliyemtangulia, basi hali ni mbaya, na JK hastahili sifa unazompa.

Unauliza kwa nini Mwalimu alitoka bila mali baada ya kutawala miaka mingi. Mwalimu hakupenda kabisa mali binafsi. Alizipiga vita, na waliokuwa na mali wakati wake walikiona cha mtema kuni. Mwalimu alikuwa na asili ya utakatifu, na kumlinganisha na watu wa kawaida kama Mkapa na JK sio sahihi. Kuna wakati Mwalimu alijichimbia Dodoma akawajengea watu masikini nyumba kwa muda mrefu sana. Hiyo sio hatua ya mtu wa kawaida kama wewe na mimi au Mkapa. Morally, Mwalimu anafanana zaidi na Mother Teresa kuliko Mkapa au JK.

Nchi yetu iliwekeana mkataba na IPTL wakati JK akiwa Waziri wa Mambo ya Nje. Na kabla ya hapo kidogo alikuwa anahusika na nishati. Inasemekana ni JK alimshinikiza Mwinyi akubali huo mkataba. Anakana, lakini sio hoja kwani hana mazoea ya kusema kweli.

Unasema vile vile kwamba Tanzania ni masikini, na ni kweli. Unakosea pale unapotegemea Mkapa awe masikini kwa vile Tanzania ni masikini. Tukiwa masikini wote ni nani atawekeza ili kuinua nchi? Mtu aliyefanya kazi ndani na nje ya nchi kwa miaka mingi kama Mkapa halafu akabaki masikini ni goigoi. Mtu wa nafasi kama alizokuwa nazo Mkapa akiweka akiba na kuwekeza fedha zake anazopata kihalali, lazima atakuwa na mali nyingi.

Augustine Moshi
 
Mwansiasa,

Waziri mkuu wa sasa, alianza kulimbikiza mali enzi za Ruhksa na Mwalimu akiwepo na alijua njia zote alizozitumia kupata mali hizo, akanyamaza kimya mpak pale tu alipotaka urais ndipo akaondoa jina lake, na baadaye kumuita Msasani na kumkaripia kuwa ni mla rushwa, that is all! Mwalimu na usomi wote aliokuwa nao, na huruma yote aliyokuwa nayo juu ya masikini akaishia tu kumkarpia badala ya kusimamia sheria ipitie mkondo wake, all the power alizokuwa nazo angeweza kusimamia sheria mpaka mwisho, lakini kwa sababu tu alitaka kumpitisha Ben yakaishia hapo tu, sasa unashangaa kuwa leo PM ana majumba kila kona kama Mkapa? Are you serious kuwa unashangaa? Wakati baba wa taifa letu alimpa free pass ili mradi tu aondoe jina lake kwenye kugombea urais?

Unajua mimi ninafikia mahali ninasema hata kuongelea siasa za bongo at some point inakuwa ni waste of time, I mean siasa gani? Viongozi tuliowaamini toka mwanzoni hakuna aliyetusaidia kwa lolote, miaka 44 ya uhuru bado tunagawana umeme? Rais wa nchi yetu akisafiri hivi unajua kuwa watu wa protocol huwa wanasafiri naye kwa kutumia cash! yaani dola cash, inamaana huwa wanabeba sanduku zima la cash dola, I mean 44 years za uhuru we cannot do better than kumpa mtu sanduku la dola afuatane na rais wetu? Where is responsibility? Huyu mtu niambie ni responsible kwa nani na hizo hela? Akisema alitoka chumbani akakuta zimepungua nani atambishia?

Mzee Moshi,

Hata siku moja siwezi kutetea ujinga lakini, lakini at the same token siwezi kuwashambulia tu viongozi wapya bila sababu, ubaya na uchafu wao tunaujua lakini tukiangalia nyuma tulikotoka hakuna mfano wa kuigwa kwa hiyo tumekwama, yes umetoa namba nyingi ambazo kwa kweli hazimsaidiii kitu mtanzania wa kawaida, way bado ni ule ule tena unazidi kukaza, kukuhusu utajiri wa haraka haraka wa rais aliyepita ninaona nikukubalie kuwa ni wa halali kwa sababu ninajua kwa undani alivyoupata ndio maana kule Bcs niliposema kuhusu dola millioni moja alizopewa mwishoni, wazee wa usalama walikuja juu kweli hivi unaaamini walikuja juu kwa ajili ya uongo?

Rais wa sasa hana mali hiyo sio siri, sasa huo mkataba alisaini bila ya kupewa hela hata kidogo? Maana wakipitisha mikataba ya ujanja si wanapewa hela sasa mzee JK zikowapi? Au na yeye amezifukia anasubiri kama Mkapa dakika ya mwisho? Kigoda na mzee JK walulizwa wakati wa kampeni za urais juu ya mkataba wa umeme hewa, wote wakakataa kuwa hawakuhusika? Yakaisha! inamaana hata waandishi hawakuwa na ushaidi wa kutosha, I mean ninawapa pongezi wazee wa Bcs kwa kutoa angalau ushahidi mzito wa hii kesi kwenye dakika za mwisho mwisho za forum, no wonder haipo tena.

Nchi yetu ni masikini mno kwa sisi wananchi hata kujaribu kusifia kiongozi mmoja over mwingine, the matter of fact hata hizi namba za uchumi eti umekua na sasa unapungua ni hadithi tu za alinacha, jamani tuwatafute na tuwaseme wachawi walioturudisha nyuma miaka 50 zaidi ya tulipopaswa kuwa, ninamsifia Mzee JK kwa sababu moja tu nayo ni angalau kuwafukuza viongozi wachache waliolalamikiwa na wananchi, kitu ambacho katika miaka 44 ya uhuru wetu hakijawahi kutokea, the rest ni yale yale tu Mungu nisaidie hakuna cha Mkapa wala Mwinyi, Watanzania hatuwezi hata kutengeneza bomu la kuondoa mbu, huko Cuba na US huwa wanaenda kuangusha kabomu ka utatanishi kwenye bwawa au pori linalodhaniwa kuwa na mbu basi hawarudi tena, bongo ndio kwanza tunagawana umeme, halafu tunaamini kuna rais mmoja alikuwa bora kuliko mwingine!

Mungu aibariki bongo ili tubanane humo humo, na Dodoma haendi mtu!
 
Mzee ES,

Umesema mara kadhaa kwamba JK amefukuza viongozi wabaya kazi. Ni akina nani wamefukuzwa? Ni huyo Mahalu tu au wako wengine kama 10 hivi? Au unahesabau hata kumsimamsiha kazi mhandisi wa manispaa ni kuwafukuza viongozi kazi?

Itabidi JK afukuze kazi watu ambao sio marafik zake, ili apate nafasi za kuwaweka watu wake, kwani anao wengi mno. Amewapanga kwenye uwaziri, ukatibu mkuu, ukuu wa mikoa, lakini bado wapo marafiki zake wa karibu ambao hajapata pa kuwaweka.

Tangu lini kufukuza tu mtu, au hata watu kazi imekuwa kigezo kikubwa cha uongozi bora? Tuambie huo uongozi bora wa JK ni upi? Amefanya nini miaka mingi alipopkuwa waziri, au mienzi hii 4 ya Urais?

JK kutokuwa na kitu sio sifa. Miaka yote ya uwaziri fedha alitafuna zote? Kama angekuwa na akili ya kuwekeza, saa hizi angekuwa na kitu kidogo. Umasikini sio sifa. Kama domestic economics zimemshinda, hizi za nchi nzima ataziwezaje?

Augustine Moshi
 
Mzee Moshi,

(1). Wananchi walimlalamikia JK kuhusu Mahita, akampumzisha kabla ya wakati, Wakalalamika kuhusu mapolisi wakafukuzwa kazi na kutinga mahakamani yaani mapolisi 15, JK akapewa ripoto ya mabalozi yetu akakuta Mahalu ana matatizo, akampumzisha mara moja, sasa hivi NMB moto unawaka, I mean I am not anapologist wa Jk na serikali yake, but how can you ignore haya aliyoyafanya on the leadershipi side?

(2). Kuhusu uchumi sina uhakika what is goin' on, na sijui what went on kabla ya JK kuingia, kwani as far as I am concerned mambo ni yale yale tu, waya mkali bongo! Kwenda nchi za nje kuimba utandawazi na kusifiwa na wazungu wakati huku nyumbani hata maji wananchi hawana, tena mjini Dar, ni aibu na ufukara wa mawazo kwa rais wetu aliyepita. Mimi sijui uchumi, lakini kama kukua uchumi ni kwenda kununua radar UK, iliyotengenezwa maalumu kwa nchi kama Israeli na sisi wabongo tukaenda kujiweka mbele kuinunua tena kwa mapesa mengi mno wakati hata umeme wa kuindeshea hatuna, ninaomba unisadidie kuelewa kama ni u-genius?

(3). Umasikini sio tija au dhana ya kiongozi bora, so is utajiri wa haraka haraka! I mean binadamu unakuwa na moyo wa aina gani hapa duniani mpaka ukaweza kufanya ukusanyaji wa mali alioufanya rais wetu aliyepita bila hata huruma kwa wanyonge? Leo mkewe akisaidiwa na Makamba amechukua kila sehemu nzuri ili ajenge majumba ya kupanga, ni nani atakaye panga hayo majumba? Kule Msasani mfano ameuona mwenyewe lijumba hilo! wapangaji hakuna, kweli hawa wezi wamekwenda kuchukua fedha za serikali na kujenga bara bara ya lami mpaka kwenye nyumba hizo ili kuvutia wapangaji, bila hata aibu! Bila hata huruma! Watoto wanaumwa magonjwa ambayo wanahitaji kwenda India tu kutibiwa, serikali haina pesa!

Now hela za kujenga hayo majumba ni za wizi, halafu bado tena na hela za bara bara ni za wizi, yaani hela za wananchi halafu ni nani atakayekusanya kodi ya hizo nyumba? Mama Mkapa, shame on them na bwana Sumaye, ameingia u-PM akiwa masikini na elimu yake ya Diploma ya Kenya, leo mzee amekusanya mapesa sidhani hata kama anakumbuka mali zote alizonazo sasa hivi, maapologist wao mnasema huu ndio uongozi bora kwani kuwa kiongozi sio lazima uwe masikini, ni kweli mzee Moshi, huo ndio uongozi bora!

(4). JK ana marafiki wengi so is Mkapa, so far hatujasikia rafiki wa JK ambaye ni kiongozi kuhusishwa na matatizo, hebu tuambie ni viongozi wangapi enzi zile waliohusishwa na wizi na rushwa na Mkapa akakataa kabisa kusikia? Idd Simba, Mbilinyi, Ngasongwa, Yona, na wengineo wengi akagoma kabisaa mpaka anaondoka!

Now beside yote, unasema Mkapa alikuwa the best president ever sasa si yeye aliyetupatia JK? Sasa mti unakuwaje bora matunda yakawa mabaya? Tena in only six months? Sio Mkapa aliyewatukana kina JM na Salim, na Mwandosya na kumpalilia JK kuwa ni kiongozi bora na ndio maana alimuweka kwa miaka 10, sasa what hapenned now mzee Moshi?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom