Na kumbuka kuwa ufikiri wetu unaathiriwa kwa kiasi kikubwa na stereotyping. Ukiwa na mke anayezungukwa na malaya jua wazi watu watakuwa wanamwita mkeo malaya; hawana muda wa sijuhi kuchunguza ooh malaya ni rafiki zake tu yeye ni tofauti; stereotyping ina save muda wa kufanya research kama hizo; rafiki zako malaya na wewe malaya simple!
Hivi kama mke wangu ataitwa malaya, wakati hana tabia hiyo ya umalaya, kitakachoniuma ni kitu gani. Binafsi nitakasirika na labda kuchukua hatua kama anafanya jambo hilo, lakini kama hafanyi zaidi tu ya kuzungukwa na marafiki wanaoitwa malaya, mie hilo halinihusu, ili mradi tu ana amani na urafiki wao hauathiri ndoa yetu............... Katika maisha huwezi kuizuia jamiii kusema lolote juuu yetu au juu ya wenzetu, hilo haliwezekani, kwani mke anaweza kuwa na tabia njema na akawa hachangamani na watu hovyo na bado akazushiwa kuwa ni malaya, Je utafanya nini!?
Kwa upande wa watoto sawa wanaweza wakabadilishwa na marafiki zao, ila kwa mtu mzima sidhani kwakweli. Akiamua kubadilika basi jua hiyo ni tabia yake tu ila alikuwa hajapata washirika!!
Linapokuja suala la malezi, wazazi tuna jukumu la kuwalea watoto wetu kwa mujibu wa maadili mema ya jamii, hapo siwezi kupingana na yeyote. Tatizo linakuja pale wazazi wanapolea kwa HAPANA bila ya kueleza kwa nini. Ikiwa mtoto hukumweleza, kwa tabia ya utundu wa kitoto, huenda wakawafata hao unahisi wana tabia usizozitaka. Ndio maana mara nyingi, tunafikiria tumewalea vyema watoto wetu kumbe wanatoa picha njema mbele yetu, pembeni wanafanya yale uliyowakataza. Na ndio maana wazazi tunashangaa na kudai "mwanangu mimi? haiwezekani, mnamzulia, mimi sikumlea hivyo".Ukweli unabaki pale pale; mfano ukiwa kama mzazi makini; watoto wako wawe wa kike au wa kiume hutapenda waongozane na watoto walio na tabia usizo zipenda. Kwa nini utegemee maajabu ya Mungu na kuishi kwa hope kuwa mwanao si bendera badala ya kumuepusha na vishawishi???? What if ni bendera???
rafiki zako malaya na wewe malaya simple!
Kweli mkuu ulichokisema nina mifano mingi tu kwa jamaa zangu.......nahisi kwa watoto ni rahisi hata kuwarekebisha pindi wanapo adopt hizo tabia....kwa mtu mzima shughul hapo ndo ilipoKwa watoto wengi ni kweli kwa sababu wako impressionable kwa sababu ya umri na tajiriba ndogo ya maisha.
Ila pia wapo watu wazima ambao wako impressionable. Fungua tu macho na utazame vizuri, utawaona. Akikuona wewe unafanya au unapenda kitu fulani basi naye huyo, anaanza kukuiga. Sisemi kila tukio au kitu cha kuigwa na mtu mzima ni kwa sababu ya impressionability ila watu wazima wa hivyo wapo wengi tu.
Si kweli, kama akili yako ni ya 'shake well before use' ndio unaweza badilishwa na hao marafiki malaya vinginevyo waweza fanya hao malaya kuwa na mwenendo mzuri wa maisha yao.
Sitaki kabisa kukuona na wale wanawake. Utakuwaje na urafiki na Malaya wale. Sasa hivi watakuuza kirahisi kabisa. Ukitaka kuifanya ndoa yetu ianze vurugu, endelea kuwa na urafiki nao. Wanawake kibao hapa mjini wamekuwa Malaya na kuvunja ndoa zao kwa sababu ya kuwa na marafiki wasio na mpango.
Je wewe unakubaliana na dhana hii, kuwa mwanamke aliyeolewa kuwa na urafiki na wanawake wasio waaminifu au wanaoitwa Malaya, basi naye atashawishiwa hadi awe Malaya?
Waambie bana........................Hata Yesu alipoulizwa na Mafarisayo, kwa nini anakula na kunywa na wenye dhambi, aliwajibu kwamba, atawezaje kuwaokoa kama akiwatenga!
Hivi kweli mtu mzima ambaye ameolewa na anajua majukumu yake kama mke, ile kuwa na urafiki na wanawake wenye tabia hizo zinazoitwa za umalaya akubali tu kuuzwa na kuwa malaya! hivi hili linawezekana kweli?
Hivi hakuna malaya walio kwenye ndoa?
Hey blubber mouth why don't you stick to your token job and stop gloating blah blah prositute, some of them did not choose to do that and they are not happy doing it, ni tabu, shida na umasikini wetu, so shut your big mouth, just because you are getting your daily bread you think your smart you start abusing people calling them prositute, how do you feel if somebody refers that to your mama or sista, wewe wacha mdomo mkubwa na uwache kuita watu malaya...........God bless Tanzania
Kama una upako wa kushindana na nguvu za shetani hapo sitii neno; kama ni binadamu wa kawaida mwenye madhaifu; unajiingiza kwenye mitego maana badala ya kuwabadili hao marafiki utabadilishwa wewe.
Hivi kweli mtu mzima ambaye ameolewa na anajua majukumu yake kama mke, ile kuwa na urafiki na wanawake wenye tabia hizo zinazoitwa za umalaya akubali tu kuuzwa na kuwa malaya! hivi hili linawezekana kweli?
Sisi tunaoishi nyumba sa kupanga huku uswahilini basi tuna kazi, maana waweza kuta unaishi nyumba moja wauza Bar kadhaa, na wale wanajiuza wamo humo humo, na mkeo ni mama wa nyumbani. kama ujuavyo, kuna kuazimana vibao vya nazi, kuombana chumvi, na usisahau habari ya kusukana Mabutu, na kuchapa umbea............................. Kama ni hivyo, ndoa zetu zitasalimika kweli?
Hizi Bhangi za kujifunza ukubwani zina madhara yake................................