Malawi waandamana kumpinga Rais Chakwera

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,554
Hatimaye taifa la Malawi lina rais mpya kutoka upande wa upinzani kufuatia uchaguzi wa marudio uliokumbwa na mbwembwe za kila aina kati ya rais anayeondoka na upinzani.

Lazarus Chakwera ambaye ni muhubiri wa zamani wa kanisa la Evangelisti aliibuka mshindi baada ya kumbwaga rais wa zamani kwa kwa asilimia 58.57 ya kura.

Lakini wiki chache baada ya kuapishwa kwake rais huyo aliyechaguliwa kwa misingi ya kuleta mabadiliko nchini humo amejipata mashakani baada ya raia wa taifa hilo kuanza maandamano dhidi yake.

Mbali na hayo rais huyo mpya alikuwa akimkosoa mtangulizi wake kwa madai ya kupendelea jamii yake na kwamba aliwapatia watu wa eneo analotoka nyadhfa katika baraza la mawaziri.

Je ni nini kilichosababisha maandamano hayo?

Muungano wa wanaharakati wa haki za kibinadamu ambao uliongoza maandamano dhidi ya uchaguzi wa 2019 uliodaiwa kuwa na udanganyifu nchini Malawi umesema kwamba kuna ''malalamisi chungu nzima''.

''Kwanza ni suala la kushirikishwa kwa watu wa familia moja ,katika baraza la mawaziri kama vile mume na mkewe na dada na kakake'', Luke Tembo alinukuliwa na aljazeera akiambia chombo cha habari cha AFP huku suala la pili likiwa majimbo, alisema.

''Tumegundua kwamba asilimia 70 ya mawaziri wanatoka katika jimbo la kati na kwamba Lilongwe pekee ina mawaziri tisa na tunajua kwamba rais anatoka Lilongwe'', alisema.

Mwanaharakati wa masuala ya kijamii Mkotama Katenge-Kaunda alisema kwamba hatua hiyo ilikuwa inakera kwa kuwa rais mpya alikuwa ameahidi kwamba Malawi mpya itakabiliana na upendeleo na ukiritimba.

Bahati ya kisiasa ya Lazarus Chakwera ilimuangukia baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana

''Raia wa Malawi wanahisi kwamba nyadhfa hizi za baraza la mawaziri hazipatiwi watu kulingana na elimu na uzoefu wao, bali kulingana na kiwango cha fedha walichoupatia muungano wa upinzani wakati wa kampeni'', alisema.

Chakwera pia anadaiwa kumteuwa afisa mkuu mpya wa polisi, gavana mpya wa benki kuu na mkuu mpya wa shirika la utozaji kodi nchini humo.

Kiongozi huyo ambaye ni muhubiri wa zamani aliahidi kukabiliana na ufisadi wakati wa kampeni zake.

Ijapokuwa ni mapema mno kuukosoa na kuukashifu uongozi wa Chakwera Swali ni je alikuwa akiwahadaa wapiga kura kwa lengo la kuwavutia wamuunge mkono katika uchaguzi huo?

Msemaji wa Chakwera Sean Kampondeni hatahivyo amesema kwamba Rais Chakwera binafsi atalihutubia taifa kuhusu malalamishi hayo.

Jinsi ushindi wa Chakwera ulivyoweka historia Afrika

Mwezi Februari, Mahakama ya katiba nchini Malawi ilifutilia mbali ushindi wa Mutharika katika uchaguzi wa Mei 2019, kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.

Wakati huo taifa hilo liligawanyika vikali wiki kadhaa kuelekea uchaguzi wa marudio.

Malawi ni nchi ya kwanza Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuandaa duru ya pili ambayo upinzani uliibuka mshinda.

Kama ilivyotokea Malawi, nchini Kenya upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka 2017 na kushinda mahakamani.

Hata hivyo mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia duru ya pili ya uchaguzi.

Baada ya matokeo rasmi kutangazwa bwana Chakwera alisema ushindi wake ni "ushindi wa demokrasia na haki" na kuongeze kusema: "Roho yangu imejaa furaha."

Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Lilongwe, kushangilia ushindi wao baadhi wakipiga honi za magari na wengine wakipiga fataki.

Lakini Baada ya hatua hiyo Bw. Mutharika alikimbia katika mahakama ya rufaa kupinga uamuzi huo lakini majaji walisimama kidete kutoa uamuzi usioegemea upande wowote.

Source BBC Swahili.
 
Nasubiri upinzani humu waliokuwa wanaserebuka huyu jamaa kushinda uchaguzi.

Wanasiasa waafrika ni pasua kichwa. Ni mjinga tu ndo yuko tayari kuhangaikia wanasiasa wetu hawa.
Tena na wapumbavu wengine wanajidai wako tayari kumwaga damu. Shenzi type kabisa.

Binadamu kwa asili ni mbinafsi, watu kama Nyerere ni nadra.
 
Hatimaye taifa la Malawi lina rais mpya kutoka upande wa upinzani kufuatia uchaguzi wa marudio uliokumbwa na mbwembwe za kila aina kati ya rais anayeondoka na upinzani.

Lazarus Chakwera ambaye ni muhubiri wa zamani wa kanisa la Evangelisti aliibuka mshindi baada ya kumbwaga rais wa zamani kwa kwa asilimia 58.57 ya kura.
Lakini wiki chache baada ya kuapishwa kwake rais huyo aliyechaguliwa kwa misingi ya kuleta mabadiliko nchini humo amejipata mashakani baada ya raia wa taifa hilo kuanza maandamano dhidi yake.

Mbali na hayo rais huyo mpya alikuwa akimkosoa mtangulizi wake kwa madai ya kupendelea jamii yake na kwamba aliwapatia watu wa eneo analotoka nyadhfa katika baraza la mawaziri.

Je ni nini kilichosababisha maandamano hayo?
Muungano wa wanaharakati wa haki za kibinadamu ambao uliongoza maandamano dhidi ya uchaguzi wa 2019 uliodaiwa kuwa na udanganyifu nchini Malawi umesema kwamba kuna ''malalamisi chungu nzima''.

''Kwanza ni suala la kushirikishwa kwa watu wa familia moja ,katika baraza la mawaziri kama vile mume na mkewe na dada na kakake'', Luke Tembo alinukuliwa na aljazeera akiambia chombo cha habari cha AFP huku suala la pili likiwa majimbo, alisema.

''Tumegundua kwamba asilimia 70 ya mawaziri wanatoka katika jimbo la kati na kwamba Lilongwe pekee ina mawaziri tisa na tunajua kwamba rais anatoka Lilongwe'', alisema.
Mwanaharakati wa masuala ya kijamii Mkotama Katenge-Kaunda alisema kwamba hatua hiyo ilikuwa inakera kwa kuwa rais mpya alikuwa ameahidi kwamba Malawi mpya itakabiliana na upendeleo na ukiritimba.
Lazarus Chakwera

Bahati ya kisiasa ya Lazarus Chakwera ilimuangukia baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana
''Raia wa Malawi wanahisi kwamba nyadhfa hizi za baraza la mawaziri hazipatiwi watu kulingana na elimu na uzoefu wao, bali kulingana na kiwango cha fedha walichoupatia muungano wa upinzani wakati wa kampeni'', alisema.

Chakwera pia anadaiwa kumteuwa afisa mkuu mpya wa polisi, gavana mpya wa benki kuu na mkuu mpya wa shirika la utozaji kodi nchini humo.
Kiongozi huyo ambaye ni muhubiri wa zamani aliahidi kukabiliana na ufisadi wakati wa kampeni zake.

Ijapokuwa ni mapema mno kuukosoa na kuukashifu uongozi wa Chakwera Swali ni je alikuwa akiwahadaa wapiga kura kwa lengo la kuwavutia wamuunge mkono katika uchaguzi huo?

Msemaji wa Chakwera Sean Kampondeni hatahivyo amesema kwamba Rais Chakwera binafsi atalihutubia taifa kuhusu malalamishi hayo.

Jinsi ushindi wa Chakwera ulivyoweka historia Afrika
Mwezi Februari, Mahakama ya katiba nchini Malawi ilifutilia mbali ushindi wa Mutharika katika uchaguzi wa Mei 2019, kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.
Wakati huo taifa hilo liligawanyika vikali wiki kadhaa kuelekea uchaguzi wa marudio.

Malawi ni nchi ya kwanza Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuandaa duru ya pili ambayo upinzani uliibuka mshinda.
Kama ilivyotokea Malawi, nchini Kenya upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka 2017 na kushinda mahakamani.
Hata hivyo mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia duru ya pili ya uchaguzi.

Baada ya matokeo rasmi kutangazwa bwana Chakwera alisema ushindi wake ni "ushindi wa demokrasia na haki" na kuongeze kusema: "Roho yangu imejaa furaha."
Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Lilongwe, kushangilia ushindi wao baadhi wakipiga honi za magari na wengine wakipiga fataki.

Lakini Baada ya hatua hiyo Bw. Mutharika alikimbia katika mahakama ya rufaa kupinga uamuzi huo lakini majaji walisimama kidete kutoa uamuzi usioegemea upande wowote.
 
Chama cha lazarus ndio chama cha ukombozo, kilitolewa na sasa kimerudi kwa mbwembwe.
Juzi si ndo nyie mkaandika maneno kibao ya kukebehi kila kitu kilichofanywa na Raisi aliyepita

Uongozi buana, ukibahatika kupita Uraisi na ukashinda, hata kama ulikuwa hutaki kuzitambua kazi zilizofanywa na Uongozi uliopita, usilipize, samehe na kusonga mbele kufanya kile ambacho Mungu amekupa cha ziada, vinginevyo, hakuna malaika hapa duniani
 
Back
Top Bottom