Malalamiko ya watalii Arusha Airport: Ni malalamiko ya kimaslahi ya madereva waliolalamikiwa na wageni, ila sio malalamiko ya wageni dhidi ya mamlaka

waBasila

Senior Member
Jun 27, 2013
168
37
Na mimi ngoja nisipepese macho. Wala nisifiche jina kwani ukweli haufichwi. Nijuavyo mimi kama niliyekuwepo kiwanja hapo na niliyeshiriki wakati malalamiko yanatolewa na wageni, ni kweli kikundi kipo kama kulivyo na kikundi cha wakata majani, madreva, na cha vijana wa kazi. Ila kikundi hiki cha wabeba mizigo kimepotoshwa kwa asilimia 98 ya yote yaliyoelezea.

Ukweli ni kwamba huyu mpotoshaji ni dreva na anatetea maslahi yake na sio ya mtalii.

Tokea ukarabati wa kiwanja umeanza, kumekuwa na mvutano baina ya madreva taxi na dreva tours kwa upande mmoja, dhidi ya kikundi hiki kwa upande mwingine.

Nashukuru stroke na wengine wamegusia upande wapili wahoja mi nachofanya naweka ushahidi tu.

Kwa sasa sipo. Ila nimewahi fanya kazi Arusha airport kwa muda, na mleta post anajua namna utendaji wa viongozi wa TAA Arusha umekuwa intact na matarajio ya wageni. Namini aliyetoa post hii ananifaham, nakuwa nachoeleza ndicho ukweli hata nikiandika jina moja tu, Basila

Iko hivi....

Kiwanja cha ndege cha arusha kimekuwa ktk matengenezo, na wakati kikundi hiki kinaanzishwa manager alipokea malalamiko ya muda mrefu toka kwa wadau na watalii kuwa kutokana na matengenezo hayo yaliyopelekea baadhi ya mageti kutotumika, wageni wanatembea umbali mrefu na mabegi, kitendo kinachopelekea madreva taxi na tours wanawadai kiasi kikubwa cha pesa za kubeba mizigo kwa beg moja nje ya bajeti zao kwani waliwadai hadi dola 5 kwa beg.

Baada ya malalamiko kuwa mengi, meneja aliwaita wadau wote, mamlaka zote na vikundi vyote. Wakatoa maoni kuwa nikweli wageni wanalalamika kuwa umbali wakubeba mabeg umekuwa mkubwa na wanadaiwa ela kubwa ya kubeba mabeg na madreva wanao waleta.

Ikapeneekezwa wawepo kikundi maalum, kisichozidi watu 5 wapewe reflectors na vitambulisho vya muda, wasaidie wagen kutatua kero hiyo kwa mgeni atakaye taka kubebewa mzigo, na wasimdai mgeni zaidi ya dola moja. Na kwakuwa madreva ndio waliolalamikiwa, basi dreva anapomshusha mgeni haruhusiwi kumbebea mizigo yake. Ktk kikao hicho hata baadhi ya watumishi waliokuwa wakibeba mabegi walipigwa marufuki kali, na hawakurudia.

Uamuzi huu haukuwafurahisha madreva na siku zote waliwachukulia vijana hawa kama wamewanyanganya tonge mdomoni, lakini siku zote wakawa ndio wanaolalamika kwa security na sio wageni kama walivyotumiwa ktk post.

Uongozi uliendelea kuwasisitiza kuwa kwakuwa vijana hao wapo kwa muda kipindi kiwanja kinakarabatiwa wajaribu kuwa wavumilivu, uongozi ufanyie kazi malalamiko ya wageni na sio malalamiko ya madreva wanaoona wamepotezewa kipato. Baada ya ukarabati kukamilika, na umbali wa kubeba beg kupungua, hali itarudi kama ilivyokuwa awali, au kama kitakuwa na mabadiriko mapyayakiwemo kuondoa kabisa mgeni kubebewa mzigo, basi wataelezwa.

Madreva hawa wanafaham kuwa kikundi hicho ni chamuda ndomana wamesubiri ukarabati sasa unaelekea ukingoni ndipo wametoa post hii kama ku pre empty, lakini c kweli kuna kitu kama malalamiko ya wagen isipokuwa yaliyoletwa dhidi yao madreva.

Madreva hawa wanaweza kuwa sawa kama shida yao nikuhitaji hali irudi kama awali sawasawa na majibu ya uongozi wa kiwanja. Ila wanakosea kuchafua uongozi uliopanbana kuhakikisha hali ipo kama ilivyo sasa, na ikizingatiwa kuwa hawa a uhakika kama wataruhusiwa nao kubeba bizigo iwapo ukarabati ukakamilika.

Kama utaratibu haujabadirika, meneja wanaye msema vibaya, wamesahau kuwa ameyavumilia pia malalamiko ya wadau kuwa madreva wanazuia mwenye taxi mwingine asilete gari yake airport kujipatia rizki zaidi ya wao? Je, nao kawaweka meneja huyu?

Tetea chako ila usiharibu wala kuchafua sifa njema ya aliye msafi kwa maslahi yako. Kwa kipindi nimekuwepo, sikuwahi ona meneja mskivu, mchapa kazi, na mkarimu, na lilikuwa kipindi ambacho kiwanja hicho kinapambaniwa kipate iso identification, na kikafanikiwa chini yake. Alikuwa mstari wa mbele kuyafikisha mafanikio ya kiwanja kwaniaba ya dg na mamlaka. Acheni kuendekeza njaa kuchafua watu.

Nijuavyo mimi, tokea ukarabati umeanza na wageni kulalamikia madreva, kikao kikafanyika pale arrival, madreva hawakupenda mazimio, ni kuwa haya malalamiko c ya wageni, ni ya kimaslahi baina ya madreva waliokuwa wanadai dola 5 kwa beg na vijana hawa wanao dai dola moja kwa mgeni bila kujali anamabegi mangapi. Mwenye akili, achuje. Mwenye ukweli zaidi ya huo alete na asifiche identification kama kweli hajalenga kupotosha umma, viongozi na serikali.

Basila M.
 
Dreva guide amdai mgeni pesa ya kubeba begi? Even dreva taxi mgeni atakupa tip na si kulazimishwa hata kama umbali ni kisongo kia ...kampuni iliyo mhost mgeni si inatambuwa hiyo scenario....for dreva taxi inaweza kuwa tatizo
 
hii nchi watu wana tamaa za kipuuzi mpaka aibu kabisa, maeneo yote ya utalii utakutana na wahuni kama hao. Ni Aibu kabisa.
 
Back
Top Bottom