DOKEZO Maji ya bomba yanayotoka Sombetini (Arusha) ni machafu na yanatuathiri Wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sisi wakazi wa Sombetini Jijini Arusha tuna changamoto ya kupata maji yasiyo salama kutoka kwenye mabomba ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA).

Hii hali ilikuwepo miezi kadhaa nyuma na sasa naona imejirudia, ipo hivi maji ya bomba kuna muda yamekuwa yakitoka yakiwa na harufu kama ya kinyesi na mengine kuwa na uchafu ambao unaonekana na usioonekana.

Inavyosemekana kuna Mkandarasi wa Kichina alipewa tenda ya kutengeneza mifumo ya maji kwenye Kata ya Sombetini nadhani katika kuunga kuna namna alichanyanya njia ya mabomba ya maji safi na maji taka, matokeo yake ndio hayo.

Tulipeleka malalamiko kwenye viongozi wa ngazi mbalimbali, wakapiga kelele hali ikapoa nadhani kuna jambo walifanya, lakini imeanza kurejea kwa mara nyingine huku viongozi wenyewe wakiwa wamekaa kimya, sijui wamewekwa mfukoni?

Kuna watu ambao wanapata magonjwa ya tumbo na mengine kutokana na kutumia maji hayo, hili jambo linatakiwa lifanyiwe kazi haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Kibaya zaidi kuna baadhi ya maeneo watu wanalazimika kutoyatumia hayo maji kisha wananunua maji kwenye magari, sasa hapo inamuwa na maana gani ya kuendelea kulipa bili ya AUWSA

=== ===

Ufafanuzi wa Diwani wa Sombetini:
Diwani wa Kata ya Sombetini, Bakari Msangi ameongea kuhusu madai hayo akisema “Kulikuwa na changamoto ya aina hiyo miezi kadhaa iliyopita, kweli Wananchi walilalamika, tukazungumza na Mkandarasi ambaye ni kama alichanganya mambo kwenye mifumo ya maji kisha akarekebisha.

“Hiyo hali kwa sasa haipo na sijapata malalamiko ya aina hiyo, hata hizi mvua zilizonyesha hivi karibuni zimeweka mambo sawa kwa kuwa zimesafisha njia vizuri.”


Pia soma
 
Ahaa swala hili kwa wakazi wa arusha hasa ukanda wa chini murieti sombetini olasiti sinoni mkono siyo la kupuuzwa kwani tumekuwa tukinywa maji chumvi tunapatwa na homa za matumbo taiphody uti amweba na kadhalika kutokana na maji tumekuwa tukijiuliza maji haya yanatoka wapi tulishaenda idara ya maji kulalamika halijafanyiwa kazi
 
Back
Top Bottom