HONGERENI TIGO, HONGERENI VODA , HONGERENI PIA ZAIN NA ZANTEL NA MENGINEYO YALIYOPO. Mpokee hongera zangu za maksudi kabisa. Takriban wiki Moja sasa Bundle za Internet za Tiggo zimekuwa zikiyoyoma kwa speed ya jet. ukijiunga baada ya sekunde hamna kitu. si hilo tu bali pia wamekuwa wakikuingizia manyimbonyimbo ya mlio na wanakukata juu kwa juu hata hujui. logwa uandike sms wakati huna salio unafurumshiwa sms nyingi za huna salio hadi inbox inajaa. moja ya shughuli walizotuzawadia watu hawa ni kibarua cha kufuta ma sms taka mengi sana. njoo kwenye Tigopesa au m-pesa, waweza tuma laki ukakatwa 500tu na ukatuma elfu themanini ukakatwa elfu mia mbili. lakini mbali na ushenzzi wote huu bado nawapongeza kwa utu kwa sababu No body control them. Serikali kupitia TCRA Imechapazake usingizi, makampuni haya yanafanya yatakavyo. unaweza kuamini ukijisajili kwenye wimbo wa msanii unakatwa Tsh320, 70%(224) inaishia kwenye makampuni haya, 30%(Tsh96) inakwenda kwenye kampuni mfadhili wa msanii. kwenye kampuni hilo wanakomba 20%(Tsh64) na ten percent ya tsh320 ndo inakwenda kwa msanii yaani Tsh32. lakini bado haitoshi msanii haipati hiyo Tsh32 kamili inaundergoes makato hapo ya Vat,charges mbalimbali hadi mkononi msanii anaambulia Tsh23.5. Kazi za msanii zinapigwa roba ya kufa mtu na hapana anayesema, ashukuru hata kwa hicho kiduchu anacho ambulia wakiamua anaweza pata zero kabisa na nobody complain, nobody cares.
nchi hii mamlaka zenye dhamana na wananchi zimeshagoma kuwatetea watanzania. hongereni makampuni ya cm, lakini fanyeni tu ubinaadam ivoivo tuenedelee hadi tutapopata Rais kwenye nchi hii