Malalamiko: Tigo Tanzania

tafakari kali

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
211
195
Tarehe 27/11/2014 niliweka vocha ya sh 3500 kwenye simu na kisha kujiunga na kifurushi cha wiki cha 3500 lakini paka leo hawajanipa huduma hiyo nimewapigia mara 2 wakiniambia subiri kidogo wanakata simu baada ya hapo napiga simu nasubiliwa kuunganishwa kwa muda wa dk 19 na sek 38 na bila kuunganishwa. Nawashahuri wadau kuweni makin na mtandao huu. Ila hii pesa lazima warudishe hata kama itanigharimu zaidi
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,095
2,000

bado makampuni ya simu, wanatuescrow kushoto kulia mungu tu ndio anajua. sijui tutampataje kafulila kwa ajili ya simu!
 
Mauja

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
509
250
Ni kweli kabisa hata juzi ya 28th walitukosesha mawasiliano ya enter net then wakaja na sty ya kuomba samahani lkn unapewa mb za 24hrs but chaajabu ukikubali unaambiwa we can charge from your tigo account
 
tafakari kali

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
211
195
Ndugu zangu wana jamii f.Tarehe 27/11/2014 niliweka vocha ya sh 3500 kwenye simu na kisha kujiunga na kifurushi cha wiki cha 3500 lakini paka leo hawajanipa huduma hiyo nimewapigia mara 2 wakiniambia subiri kidogo wanakata simu baada ya hapo napiga simu nasubiliwa kuunganishwa kwa muda wa dk 19 na sek 38 na bila kuunganishwae.Nahisi hawa jamaa wa tigo kuna kamchezo wanacheza kawizi wizi,nilishawahi kusikia tabia yao hii kwa mtu mwingine sasa imenitokea mwenyewe,sisemi muache kutumia tigo la hasha ila Nawashahuri wadau kuweni makin na mtandao huu. hii pesa lazima warudishe hata kama itanigharimu zaidi
 
KISHINDO

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
1,747
2,000
Tigo ni wezi kabisa.
Serikali ipo inaangalia hivi vimitandao mchwala.
Leo wamenitumia 220 kama mkopo na kuniambia eti mtarejesha 250 nikiweka salio wakati hata sijaomba huo mkopo wao.

Hii nchi imejaa escrow kila kona.

Ila kuna siku haya yote yatakuwa historia maana wananchi wameshachoka.

Mtandao wenye kuaminika hapa tanzania ni airtel tu, hayo mengine ni uchafu tu.
 
Mngendalyasota

Senior Member
Jan 22, 2011
171
0
Unachoongea ni sahihi kabisa. Mimi nilinunua kifurushi cha internet cha mwezi 20,000/=GB 35 lakini internet yao imekuwa low au hakuna kabisa. Sehemu nilipo ni Mabibo hostel wengi wanasema maybe kwa kuwa watumiaji ni wengi. Sasa kama kampuni wanatakiwa wajue spatio-problems ya huduma zao!
 
Daniel Myl

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
536
225
Eti mimi naambiwa siwezi kujiunga na kifurushi cha Gb 20 eti kisa namba yangu hijateuliwa, yaaani huduma niitake mie halafu uniambie mpaka hapo nitakapo subiri uteue namba yangu nimeshawahama siku nyingi sana
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,302
2,000
Ha! Ha! Haaaa!!! Yaani ni kama kuuziwa mche wa sabuni ukidhani twanga pepeta , pole sana kijana .
 
mwabakuki

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
266
195
naomba mods,,muiache hii,,ili itumike kusolicit maoni ya wananchi kuhusu huduma za tigo..mimi binafsi ni muhanga wa vitendo hivi vya wizi kupitia mtandao wa tigo..miezi miwili iliyopita sikunmoja niliweka vocha ya shilingi elfu 10 kupitia maxmalipo...hapo hapo baada ya vocha kuingia nikakatwa shilingi elfu tano,,zikabaki elfu tano,,nikaamua kuunfa kifurushi cha wiki,,kabla sijaoiga nikatumiwa meseji kwamva kifurushi changu kimeisha,,nikapeleka lalamikoblangu oale tigo ktk ofis zilizoko palm residency pale ocean road...nikarecord malalamiko yangu,,kwa bahati nzuri nina copy ta malalamiko hayo,,lkn hadi leo hiyo pesa yangu haijawahi kurudi..

naamini mauza uza haya ya kipuuzi na kijinai hayatukuta sisi peke yetu...mamilioni ya pesa yanaibwa kila siku kuputia mitandao ya dimu...

ni wakati muafaka sasa kwa bunge kuingilia suala hili..wasiwasi wangu,,inawezekana kuna syndicate kubwa ambayo inawezekana inawahusisha wafanyakazi umma na mamlaka wanazifanyia kazi, wanasiasa nk...ajbayo inafacilitate upigaji wa pesa kupitia mitandao..

tuliombe bunge lianzishe uchunguzi,,kinyume chake tunatengeneza utamaduni wa watu kufanya wizi tena mkubwa bila kuwajibika
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,805
2,000
mmeshindwa kukomaa kuhusu mabilioni ya escrow mnakuja kudai elfu 3000 kama vipi mpigie simu ruge au chenge akupunguzie.tuanze na ishu kubwakubwa hawa wadogo tutawamudu wats 3500 mbele ya 306 bilioni
 
Cosmo 1

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
460
500
Ni kweli hata mimi ni muhanga wa tatizo hili pia! Siku ya tarehe 28 nilinunua vocha ya buku, na nikajiunga, ila ndani ya dakika 1 tu oesa yote hakuna!
Nafikiri hawa jamaa system yao huwa wanrekebisha kuwaibia wateja wao kwa muda furani

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,462
2,000
Na internet ya tigo hapa Dodoma ni kero sana.Kwa mfano,ukiwa baadhi ya maeneo ya Kikuyu hasa St.John's university ndani ya chuo,net ya tigo ni ya hovyo mno ni kero kwakweli.

Mjirekebishe.
 
babacollins

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
878
195
Duh! Nchi hii sheria taratibu kanuni maadili na misamiati inayofanana na hiyo ilishanyofolewa kwenye kamusi.
 
asakuta same

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
14,843
0
Tigo ni wezi kabisa.
Serikali ipo inaangalia hivi vimitandao mchwala.
Leo wamenitumia 220 kama mkopo na kuniambia eti mtarejesha 250 nikiweka salio wakati hata sijaomba huo mkopo wao.

Hii nchi imejaa escrow kila kona.

Ila kuna siku haya yote yatakuwa historia maana wananchi wameshachoka.

Mtandao wenye kuaminika hapa tanzania ni airtel tu, hayo mengine ni uchafu tu.
Hamna mtandao wa kuaminika ndugu , yote wizi wizi na chenga tu.
 
asakuta same

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
14,843
0
naomba mods,,muiache hii,,ili itumike kusolicit maoni ya wananchi kuhusu huduma za tigo..mimi binafsi ni muhanga wa vitendo hivi vya wizi kupitia mtandao wa tigo..miezi miwili iliyopita sikunmoja niliweka vocha ya shilingi elfu 10 kupitia maxmalipo...hapo hapo baada ya vocha kuingia nikakatwa shilingi elfu tano,,zikabaki elfu tano,,nikaamua kuunfa kifurushi cha wiki,,kabla sijaoiga nikatumiwa meseji kwamva kifurushi changu kimeisha,,nikapeleka lalamikoblangu oale tigo ktk ofis zilizoko palm residency pale ocean road...nikarecord malalamiko yangu,,kwa bahati nzuri nina copy ta malalamiko hayo,,lkn hadi leo hiyo pesa yangu haijawahi kurudi..

naamini mauza uza haya ya kipuuzi na kijinai hayatukuta sisi peke yetu...mamilioni ya pesa yanaibwa kila siku kuputia mitandao ya dimu...

ni wakati muafaka sasa kwa bunge kuingilia suala hili..wasiwasi wangu,,inawezekana kuna syndicate kubwa ambayo inawezekana inawahusisha wafanyakazi umma na mamlaka wanazifanyia kazi, wanasiasa nk...ajbayo inafacilitate upigaji wa pesa kupitia mitandao..

tuliombe bunge lianzishe uchunguzi,,kinyume chake tunatengeneza utamaduni wa watu kufanya wizi tena mkubwa bila kuwajibika
Hapo itakuwa wanaccm wanatafuta mashiko wa kampeni.
 
manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
Ndugu zangu wana jamii f.Tarehe 27/11/2014 niliweka vocha ya sh 3500 kwenye simu na kisha kujiunga na kifurushi cha wiki cha 3500 lakini paka leo hawajanipa huduma hiyo nimewapigia mara 2 wakiniambia subiri kidogo wanakata simu baada ya hapo napiga simu nasubiliwa kuunganishwa kwa muda wa dk 19 na sek 38 na bila kuunganishwae.Nahisi hawa jamaa wa tigo kuna kamchezo wanacheza kawizi wizi,nilishawahi kusikia tabia yao hii kwa mtu mwingine sasa imenitokea mwenyewe,sisemi muache kutumia tigo la hasha ila Nawashahuri wadau kuweni makin na mtandao huu. hii pesa lazima warudishe hata kama itanigharimu zaidi
Kama unafikiri hawa wana kuibia jaribu Smart huone moto wake.Niliweka sh 10,000/ikakatwa elfu nane kwa mkupuo. nikarudia kuweka elfu kumi nikakatwa nne. Nikazila.Haya mambo ya ESCROW yamefanya niirudie baada ya mtandao niliokuwa natumia kusumbua. Nilipoweka elfu tano hapohapo nikachinjwa 2200. Nilipowauliza wakanambia nimetumia kwenye internet , ilibidi nicheke tu. Ila internet yao ni za fastest.
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,444
2,000
mmeshindwa kukomaa kuhusu mabilioni ya escrow mnakuja kudai elfu 3000 kama vipi mpigie simu ruge au chenge akupunguzie.tuanze na ishu kubwakubwa hawa wadogo tutawamudu wats 3500 mbele ya 306 bilioni
Kila tu na evel yake
acha sisi tunaoibiwa tulalamike, 2000 ni nyingi

tiGo ni wezi hasa mm nimeachana nao katika mtandao kwani nimeingiza zaidi ya hizo 2,000 na jana wakaniambia wamenipa 100Mb za bure nizitumie ndani ya masaa 24
Nilipojaribu kuingia tu nikajibiwa hakuna salio na hata mtandao hakuna kabisa
Tigo acheni wizi
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,603
2,000
Ndugu zangu wana jamii f.Tarehe 27/11/2014 niliweka vocha ya sh 3500 kwenye simu na kisha kujiunga na kifurushi cha wiki cha 3500 lakini paka leo hawajanipa huduma hiyo nimewapigia mara 2 wakiniambia subiri kidogo wanakata simu baada ya hapo napiga simu nasubiliwa kuunganishwa kwa muda wa dk 19 na sek 38 na bila kuunganishwae.Nahisi hawa jamaa wa tigo kuna kamchezo wanacheza kawizi wizi,nilishawahi kusikia tabia yao hii kwa mtu mwingine sasa imenitokea mwenyewe,sisemi muache kutumia tigo la hasha ila Nawashahuri wadau kuweni makin na mtandao huu. hii pesa lazima warudishe hata kama itanigharimu zaidi
Serikali hii yaanihHadi iwe escrow scandal ndo wanashughulikia tena kwa ubishi na kuitana tumbili.
 
jorojo

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
1,643
0
tigo wapuuzi kweli kweli ukiwa udom humanity university promotion haipatikani mtandao wa ovyo ovyo huu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom