Malalamiko dhidi ya JF yatupwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,392
39,495
Baada ya sakata la Manumba na watu wake, kulifanyika jaribio jingine la chini la kuweza kunyang'anya jina la jamboforums na mengine yaliyoandikishwa pamoja nalo na hivyo kulazimisha kutafuta jina jingine. Malalamiko hayo yaliyotolewa kwenye "National Arbitration Forum". Muda si mrefu ulipita hatimaye tumejulishwa kuwa chombo hicho kimeyatupilia mbali malalamiko hayo "without prejudice". Hivyo kwa wakati huu tunaweza kupumua kidogo na tukitumaini kuwa Bw. Mushi hatojaribu tena kuingilia utendaji kazi na uendeshaji wa Jambo Forums.

dismissal.JPG

Na hivyo basi vyombo vingine vilivyokuwa vimeshikilia domains hizo vimepewa taarifa rasmi kuwa madai ya Bw. Mushi yametupwa na hivyo mambo yote yanaendelea kama kawaida.

---------- Forwarded message ----------
From: <domaindisputes@godaddy.com>
Date: Tue, Mar 11, 2008 at 9:08 PM
Subject: RE: ORDER- William Mushi v Great Thinkers aka Watu Kutu aka eMedia Interactive Inc- FA0802001153030
To: "Johnson,Alexandra Rosenbaum" <arosenbaum@adrforum.com>
Cc: disputes@opensrs.org, wmushi@gmail.com, watukutu@gmail.com, parkingpartners@emedia.comDear Parties,

This is to confirm that GoDaddy.com has received the Dismissal.

The Registrar-Lock has been removed from the domain names JAMBOVIDEO.COM, JAMBOTANZANIA.NET, GOTOTANZANIA.COM, JAMBOFORUMS.COM, JAMBOTEAM.ORG, JAMBONETWORK.COM, JAMBOVIDEOS.COM, JAKAYAKIKWETE.COM, JAMBOSEARCH.COM, and JAMBOTHINKTANK.COM. Please feel free to contact us with any questions.

Kind Regards,

Diane E. Whiting
Domain Services
GoDaddy.com, Inc.
 
Baada ya sakata la Manumba na watu wake, kulifanyika jaribio jingine la chini la kuweza kunyang'anya jina la jamboforums na mengine yaliyoandikishwa pamoja nalo na hivyo kulazimisha kutafuta jina jingine. Malalamiko hayo yaliyotolewa kwenye "National Arbitration Forum". Muda si mrefu ulipita hatimaye tumejulishwa kuwa chombo hicho kimeyatupilia mbali malalamiko hayo "without prejudice". Hivyo kwa wakati huu tunaweza kupumua kidogo na tukitumaini kuwa Bw. Mushi hatojaribu tena kuingilia utendaji kazi na uendeshaji wa Jambo Forums.

dismissal.JPG

Na hivyo basi vyombo vingine vilivyokuwa vimeshikilia domains hizo vimepewa taarifa rasmi kuwa madai ya Bw. Mushi yametupwa na hivyo mambo yote yanaendelea kama kawaida.

ok !!..................
 
Nakuambia watetezi wa ufisadi kina kama huyo hapo juu wamepata kihoro sana kuiona hii maana walitaka kabisa kuona JF ikipotea milele.

Naona mwaka huu kuna watu watajinyonga maana kila kampeni walizoanzisha zimeakufa kifo cha mende.... miguu juu.. pwaaaa
 
If the freedom of speech is taken away then dumb and silent we may be led, like sheep to the slaughter.
George Washington
 
wewe mwafrika wa kike si useme tu kwamba unamtaja KadaMpinzani, unaogopa nini ?? FEEL FREE !!

sasa ona utakavyogonga ukuta nitakapokupuuzia !

nani anayetaka JF ipotee ?? nimekuja hapa kabla yako, umenikuta ! huwezi kusema unachosema with justification UNLESS unasema kufurahisha baraza na nafsi yako !

Naona post zako nyingi sana 85% ni udaku, umbea, na mengineyo mengi unayoyajua.....well to make it clear, you are free to say whatever and however you want, LAKINI SUALA LA KUSEMA NATAKA JF IPOTEE....IS REALLY SILLY !
 
Naona kuna haja ya kusikiliza tena ule wimbo wa Jaydee wa...... na kuwawekea some guys hapa JF! Kampeni zote dhidi ya JF zimefeli na wameinama weeeeeeeee sasa wameinuka na watarudisha vilio vyao JF kama kawaida yao.

JF is here to stay guys na hakuna mtakachofanya kwa sasa so kula nyembe or something.
 
wewe mwafrika wa kike si useme tu kwamba unamtaja KadaMpinzani, unaogopa nini ?? FEEL FREE !!

sasa ona utakavyogonga ukuta nitakapokupuuzia !

nani anayetaka JF ipotee ?? nimekuja hapa kabla yako, umenikuta ! huwezi kusema unachosema with justification UNLESS unasema kufurahisha baraza na nafsi yako !

Naona post zako nyingi sana 85% ni udaku, umbea, na mengineyo mengi unayoyajua.....well to make it clear, you are free to say whatever and however you want, LAKINI SUALA LA KUSEMA NATAKA JF IPOTEE....IS REALLY SILLY !

...Du beef nyingine bwana..Kada sikilizia mtu wangu sisi wote ni wamoja
 
"Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu" - Author unknown

Naam, sauti ya wengi tusio wanachama wa chama chochote cha siasa Tanzania, wana ccm wenye mapenzi ya kweli na Tanzania akina FMES na masatu, wanachadema, wanacuf, wanatpl kwa kifupi watanzania waliochoshwa na ufisadi ni SAUTI YA MUNGU!
 
I expected this verdict.

Kuna baadhi ya watu wanaamini kabisa kuwa pesa ndiyo jibu la tamaa zao bila kuangalia ukweli wa mambo. Nilitamani Bwana Mushi awe ameweka at least dola laki mbili kwenye hii kesi ili aone jinsi ambavyo zingeyeyuka kirahisi vile.
 
huu ni ukumbi wetu sote wana CCM na Wana CHADEMa na wengine waq vyama vyengine au wasio na vyama.

wana dini na wasio na dini na hata wale wenye kupenda mambo ya kikubwa na kitoto pia.

hatupendi kuona malumbano ya kipuuzi na kijinga hapa ni no ndo tu bila ya kulala

JF ni uwanja unaounganisha watanzania wote ili tupambane kwa hoja bila ya kutukanana au kuvunjiana heshima.

kwa hio hakuna mshindi wala mshindwa ktk hili
 
Ama kweli kuna ufisadi hata dhidi ya JF. "Vox Populi, Vox Dei" Hata IGP Mwema anaipenda JF tatizo taratibu za kuwaridhisha Mafisadi zilipelekea kuwe na huo mchakato wa kuipora Jamboforums na hao vibaka wachache, hatimaye tunasema "Deogratias".
 
Baada ya sakata la Manumba na watu wake, kulifanyika jaribio jingine la chini la kuweza kunyang'anya jina la jamboforums na mengine yaliyoandikishwa pamoja nalo na hivyo kulazimisha kutafuta jina jingine.

Ningekuwa mimi manumba ningekaa mbali na hawa watu wa JF manake naamini wanajua uchafu na ufisadi wangu fika.Hivyo wakianza kuuanika hapa patakuwa hapakaliki pale ofisi.Naamini wanajua sana issue zangu na aliyekuwa mkuu wa Upelelezi Wilaya Singida ndg Shilogile na sasa ni mkuu wa Polisi wilaya ya Muleba.Haya manumba sijui manumbi
 
Mimi haya wee!!!!!!!! Sasa Kaka Majita yaweke peupe hayo ya Manumba, ili yeye mwenyewe aamini kwamba JF ni zaidi.
 
M.M.M, Invi..., na wote mnaofanya kazi kubwa na yenye baraka ya kuuweka mtandao wetu wa "Watu Kutu" (I like this one) uendelee kupeta katika anga zote, chafu na safi.......Naomba niwape pongezi kubwa na kuwaatakia mema yote!!!

WanaJambo, hongereni sana kwa kazi kubwa, wembe ni ulele ikiwezekana tuunoe zaidi................
 
mwaka mbaya kwa mafisad huu!
wanapokwenda wamebanwa.....na ufisadi wa aina yoyote una bounce! kazi kweli kweli.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom