Malaika kaponzwa na weupe wake

Malaika kaponzwa na weupe wake

Uliposema malaikaa mweupeee kitu kimekurupuka huku kunako boxer sasa kinasoma signal sasa Mkuu umeshindwa kutuletea kapicha ka malaika we kweli Emoji
 
MALAIKA KAPONZWA NA WEUPE WAKE

Rafiki yangu Yohana ni baba wa familia, ana watoto kadhaa. Jina la utani Yohana huwa tunamwita Ngosha kwa sababu anatokea kule kwetu. Vilevile Ngosha Yohana huwa tunamwita Mong'o maana sura yake anatabasamu kwa nadra!

Ngosha Yohana huwa tunamwita bichwa mchongoko au vichwa pacha, maana kichwa chake kina nyongeza fulani, ukikiangalia vizuri unaweza kuhesabu vichwa viwili.

Anyways, sifa za sura na kichwa cha mshkaji wangu siyo ishu sana. Lipo jambo Ngosha kalizua. Anaye dada wa kazi, ukimwita housegirl utakuwa hujakosea. Jina la huyo housegirl ni Malaika ila wenyewe humwita kwa Kizungu, Angel.

Ngosha alifanya jambo moja la kupongezwa sana. Alitoa ajira kwa Malaika pamoja na mume wake anayeitwa Mbili. Hata hivyo aliwatenganisha maeneo ya kazi.

Wakati Malaika kazini kwake ni nyumbani kwa Ngosha, Mikocheni, jirani na Hospitali ya Kairuki, Mbili yeye ofisini kwake ni shambani. Mbili anaishi kwenye shamba la Ngosha lililipo Chunya, Mbeya. Hurudi Dar na kukutana na mkewe nyakati za likizo.

Juzi nikaitwa na shemeji, yaani mke wa Ngosha. Nikafika Mikocheni, jirani na Hospitali ya Kairuki. Shem akanilalamikia kuwa mume wake kafanya jambo la hovyo sana.

"Wewe fikiria shem, huyu Angel ni mke wa mtu, halafu Yohana akawa anataka Mbili akae sana Chunya, kumbe aliwatenganisha ili amfaidi mke wa mwenzake," shem alilalamika kisha akaongeza:

"Kinachoniuma zaidi amempa na mimba. Yohana wewe ni wa kutembea na Angel mpaka unampa mimba? Unafahamu wewe ni baba wa familia na Angel ni mke wa mfanyakazi wako!"

Nikasitisha mazungumzo kwa kumwambia shem aniitie huyo Angel nimuone. Angel akaitwa. Mtoto mweupeeee peeeee! Peeee yaani! Mpaka hapo nikawa nimeshapata jibu.

Nikamuuliza Angel: "Jina lako ni Angel?"

Angel akanijibu: "Hapana, jina langu Malaika, ila tangu nimefika hapa, baba na mama huwa wananiita Angel."

Shem akadakia: "Kwani hujui Malaika ni Kiswahili na Kiingereza ni Angel? Sikupendi wewe Angel kuniingilia ndoa yangu. Tena wewe siyo Malaika ni Shetani. Wewe ni Devil siyo Angel."

Basi ikabidi nimtulize shem, nikamwambia Malaika aondoke pale sebuleni. Alipoondoka nikamgeukia Yohana, nikamwambia: "Mshkaji umeniangusha sana."

Shem akadakia tena: "Kakuangusha kwani vidogo? Limwanaume limejaa tamaa tu."

Nikamgeukia shem nikamwambia: "Ila na wewe ulichemka. Umemuona Malaika alivyo mweupe? Na si unajua sisi akina Ngosha tunavyopenda wanawake weupe? Halafu wewe ukaruhusu aingie ndani ya nyumba kwa jina la dada wa kazi, kweli kabisa ulitegemea mbuzi aone majani asile?"

Shem akajibu: "Lakini kweli." Ngosha akaendelea kuwa kimya.

Nikamwambia shemeji yangu: "Msamehe Malaika, hana kosa, ameponzwa na weupe wake."

Shem akajibu tena: "Lakini kweli."

Ugomvi nikausuluhisha kwa mtindo huo. Hata nikikutana na mume wa Malaika nitamwambia amsamehe mkewe, maana ameponzwa na weupe wake.

Ndimi Luqman MALOTO
Naona fasihi katika ubora wake
 
Aiyaaaa, baba ubaya kaharibu tena? Ina maana yule shombe wa kihaya ashajazwa mimba teyari?
 
narudi mambo hatari sana haya


baba yohana alikuw anafanya ubatizo wa karne
 
Back
Top Bottom