Sheikh adai Los Angels maana yake Malaika waliopotea

Kinyungu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
22,576
Reaction score
45,477
Nilikuwa nasikiliza maelezo ya huyu Sheikh anaeleza maana ya Los Angels mji ulioko Pwani ya Magharibi ya Marekani katika jimbo la California.
  1. Sheikh anadai kuwa Los Angels maana yake ni Malaika waliopotea (#Lost Angels).
  2. Anasema Los Angels kuna jiwe kutoka mbinguni lina ukubwa wa kilometa 12. (#Ni ukubwa siyo urefu)
  3. Anasema ni jiwe aina ya Kimondo kama cha Mbeya (#Kimondo kipo Songwe siyo Mbeya)
  4. Anasema kazi ya vimondo Mungu kaieleza katika surat jin 72:13
  5. Kwamba kuna majini wachafu walikuwa wanaenda mbinguni kuchukua taarifa na kuwaletea watu duniani
  6. Ndipo mwenyezi mungu akaandaa malaika wanaotembea na vimondo au mawe yenye moto
  7. Mawe ama vimondo yanatoka katika ozone layer
  8. Wale majini wachafu wanapoenda kuchukua taarifa wale malaika huwarushia majini hao mawe ya moto. Mawe hayo yanatembea kwa speed zaidi ya umeme au sawa na jini ama mwale wa moto.
  9. Jini anaweza toka Marekani hadi Dar es Salaam kwa sekunde 2
  10. Lile jiwe kubwa la kimondo lililoko Los Angels lilitumika kuwapiga majini wawili waasi ambao walikuwa wakubwa. Kwa hiyo lile jiwe kubwa la km 12 liliwapiga na kuwakandamiza hadi leo hapo Los Anges na hivyo kupeleke mji huo kuitwa Los Angels au Malaika waliopotea😂😂😂
Msikilize Sheikh hapa chini kwenye video

========
Los Angles ni mji uliko pwani ya Kusini Magharibu ya USA. Neno "Los" ni la asili ya Spanish na ni sawa na article "The" katika lugha ya Kingereza. Hivyo kwa Kingereza Los Angles ingeandikwa The Angles ama Malaika kwa Kiswahili. Chanzo cha mji kuitwa Los Angels ni wahamiaji wa Kispanish ambao waliupa mji huu jina la "El Pueblo de Nuestra Señora la Reina de los Ángeles de Porciúncula,"

Kwa kifupi wanaita mji wao "Los Anges"

ama kwa Kingereza ingetamkwa

"The Town of Our Lady the Queen of Angels of Porciúncula."

Kwa Kiswahili tungeweza kutafsiri kama

"Mji wa Mama Yetu Malkia wa Malaika wa Porciúncula."

Mji huu hauna uhusiano na malaika waliopotea

Huyu Sheikh asirecord tena uongo wake kama alivyo ahidi maana ataonekana hamnazo

View: https://x.com/PolycarpMDM/status/1905553597313532369?t=50ACyzvtsdSdKKIIAUW6IA&s=19
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
1743693940766.jpg
 
Nilikuwa nasikiliza maelezo ya huyu Sheikh anaeleza maana ya Los Angels mji ulioko Pwani ya Magharibi ya Marekani katika jimbo la California.
  1. Sheikh anadai kuwa Los Angels maana yake ni Malaika waliopotea (#Lost Angels).
  2. Anasema Los Angels kuna jiwe kutoka mbinguni lina ukubwa wa kilometa 12. (#Ni ukubwa siyo urefu)
  3. Anasema ni jiwe aina ya Kimondo kama cha Mbeya (#Kimondo kipo Songwe siyo Mbeya)
  4. Anasema kazi ya vimondo mungu kaieleza katika surat jin 72:13
  5. Kwamba kuna majini wachafu walikuwa wanaenda mbinguni kuchukua taarifa na kuwaletea watu duniani
  6. Ndipo mwenyezi mungu akaandaa malaika wanaotembea na vimondo au mawe yenye moto
  7. Mawe ama vimondo yanatoka katika ozone layer
  8. Wale majini wachafu wanapoenda kuchukua taarifa wale malaika huwarushia majini hao mawe ya moto. Mawe hayo yanatembea kwa speed zaidi ya umeme au sawa na jini ama mwale wa moto.
  9. Jini anaweza toka Marekani hadi Dar es Salaam kwa sekunde 2
  10. Lile jiwe kubwa la kimondo lililoko Los Angels lilitumika kuwapiga majini wawili waasi ambao walikuwa wakubwa. Kwa hiyo lile jiwe kubwa la km 12 liliwapiga na kuwakandamiza hadi leo hapo Los Anges na hivyo kupeleke mji huo kuitwa Los Angels au Malaika waliopotea😂😂😂
Msikilize Sheikh hapa chini kwenye video
View attachment 3292204

View attachment 3292207

========
Los Angles ni mji uliko pwani ya Kusini Magharibu ya USA. Neno "Los" ni la asili ya Spanish na ni sawa na article "The" katika lugha ya Kingereza. Hivyo kwa Kingereza Los Angles ingeandikwa The Angles ama Malaika kwa Kiswahili. Chanzo cha mji kuitwa Los Angels ni wahamiaji wa Kispanish ambao waliupa mji huu jina la "El Pueblo de Nuestra Señora la Reina de los Ángeles de Porciúncula,"

ama kwa Kingereza ingetamkwa

"The Town of Our Lady the Queen of Angels of Porciúncula."
Kwa Kiswahili tungeweza kutafsiri kama
"Mji wa Mama Yetu Malkia wa Malaika wa Porciúncula."

Mji huu hauna uhusiano na malaika waliopotea

Huyu Sheikh asirecird tena uongo wake kama alivyo ahidi maana ataonekana hamnazo

View: https://x.com/PolycarpMDM/status/1905553597313532369?t=50ACyzvtsdSdKKIIAUW6IA&s=19

Umenikumbusha kuna picha fulani inaonyesha namna watu wanavyoiona dunia vs aliens wanavyoiona dunia.

Wanadamu wanaiona dunia ikiwa na mabara yake saba ila aliens wanaiona dunia ikiwa na nchi moja tuu ya USA 😂

Kwamba, hao malaika na majini waliiona USA tuu hapo Los Angeles Na Sio sehemu zingine 😂
 
Hako ka shehe ni kaongo kaongo na kakuda sana.

Hakuna utofauti na wale wazee wa Istiqama wazee wa "Devoshipa"

Kana ile dhana ya kujifanya ni moja ya prominent modern Muslim scholar hapa Tz.

Mara siku eti anamchambua nyuki kisayansi halafu anafanya na relate kwenye Quran na kuinasibu Quran kuwa iko mbele ya Sayansi.

Na waumini wanajaa.
 
Back
Top Bottom