Makusanyo ya TRA ya Julai - September 2018/2019 yapanda maradufu: Yakusanya 3,840,000,000,000/-

Wale wanaochukia jitihada za awamu ya tano nina uhakika watachukizwa na habari hii pia.

Wakwanza akiwa ni yule muheshimiwa mshirikina wa Kigoma Ujiji na Domo Kaya aliyepo kwenye matibabu Ubeligiji.
 

Ni tatizo la uwezo wa kujua kusoma namba na kuzitafsiri kwa maneno, pole ndg yangu rudi skuli upya na uwasikilize walimu wako uache tabia ya kupiga chabo wakati wa mitihani
 
Tatizo mmeweka Sheria za Twakimu zinabana kuchambua takwimu za serikali kukosa hizo Sheria Zitto angetuambia Ukweli.
 


Ambayo ni sawa na "zaidi" ya asilimia 5.3%. Tuzingatie, tuwe makini kutumia lugha sahihi. Tuna wataalamu wa kutosha.

"Zaidi" ni neno muhimu hapa. Otherwise the statement doesn't make any sense.
 
hata mkisema mmekisanya trillion 400, nani atabisha, say anything you like! trillion 1,000 zimekusanywa Salary Slip
 
Hawa TRA na BOT wangekuwa wanatoa detailed statistics kuliko hii final figure ingependeza.
Tunataka tupate indication ya growth kwenye kila sekta mfano kilimo, uvuvi, imports, exports, biashara za ndani, uzalishaji viwandani nk.
 
Mleta mada nawe umetia kachumbari hiyo taarifa ni kweli kuna ongezeko lakini kusema maradufu siyo kweli maana difference ni 0.19 kati ya 3.84 na 3.65 maradufu ingekuwa na sense kama tungekuwa na difference ya kuanzia at least 1.5 hivi

Ila bado wanapaswa kupongezwa japo hata kwa hicho kidogo walichofanikiwa ila sasa watafute namna kidogo hizo hela zirudi kwenye mzunguko ili kuchochea zaidi ukuaji wa uchumi na kuongeza purchasing power ya watu wakifanya hivyo mapato yataongezeka ila hii contractionary method yao ina athari sana maana hali zetu wananchi mbaya
 
Jifunze kwanza kuandika kiswahili...marafufu ndo nini wew jinga kubwa?Shida ni kukimbilia sit kushabikia mithili ya zombiz!!
 
sasa wanatuletea takwimu ili sisi tusemeje??
siku hiz ukisema waongo unawekwa jera. wanataka tuitikie kama tuko ibadani ! ujinga huu kuna kipindi tutakua tunaukwepa kama sio sisi waasisi
 
Tangu iwekwe ile sheria ya takwimu, ni vigumu sana kuamini usahihi wa taarifa za serikali na vyombo vyake. Hakuna anayeweza kuhoji wala kuhakikii.
 
Hii habari yote ni upuuzi mtupu.

Aliyesema kuwa mapato yameongezeka maradufu yaelekea hata kiswahili hajui. Mapato yaliyoongezeka ni kidogo sana ambayo wala hata hayaendani na ukuaji wa uchumi ambao tuliambiwa ni 7%. Kama uchumi unakuwa kwa 7%, inakuwaje mapato yaongezeke (revenue difference not revenue growth rate) kwa 5% tu? Na hiyo 5% ni ongezeko wala siyo ukuaji.

Kwa vyovyote, ina maana ukuaji wa makusanyo ya serikali ni chini ya 2.5%. Hapa lazima kuna eneo tunadanganywa. Haiwezekani ukuaji wa uchumi 7%, ukuaji wa makusanyo ya kodi chini ya 2.5%!

Kwa wasiojua maana ya maradufu:

Ufafanuzi wa maradufu katika Kiswahili

maradufu

KIVUMISHI1

mara mbili ya kitu kingine k.v. kwa ukubwa, ujazo, thamani, nguvu au idadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…