Makusanyo ya TRA ya Julai - September 2018/2019 yapanda maradufu: Yakusanya 3,840,000,000,000/-

Daimler

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
556
973
Mamlaka ya Mapato nchini TRA, imetoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato yake ya quarter ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/2019, ambayo imeonyesha makusanyo ya shilingi Trilioni 3.84, sawa na asilimia 5.3% ya mwaka 2017/2018 ambako makusanyo yalikuwa ni trilioni 3.65.

TRA imewashukuru walipakodi wote ambao wameendelea kulipa kodi zao kwa hiari na kwa wakati na kuwahimiza wale ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo kwa wakati.

TRA imewataka wenye changamoto mbalimbali kufika katika Ofisi za TRA mikoani na wilayani kuonana na mameneja wao.

IMG_9135.jpg
 
Mamlaka ya Mapato nchini TRA, imetoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato yake ya quarter ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/2019, ambayo imeonyesha makusanyo ya shilingi Trilioni 3.84, sawa na asilimia 5.3% ya mwaka 2017/2018 ambako makusanyo yalikuwa ni trilioni 3.65.
TRA imewashukuru walipakodi wote ambao wameendelea kulipa kodi zao kwa hiari na kwa wakati na kuwahimiza wale ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo kwa wakati. TRA imewataka wenye changamoto mbalimbali kufika katika Ofisi za TRA mikoani na wilayani kuonana na mameneja wao.

View attachment 891163
 
Yamepanda vipi maradufu ikiwa tuliambiwa kila mwezi TRA wanakusanya zaidi ya trilioni moja, sasa ukipiga hesabu kwa miezi mitatu mapato si ndio yale yale tu
Siyo miezi yote huwa zinafikia trilioni moja. Ndiyo maana quarter hii kwa kuwa ndiyo mwaka wa fedha unapoanza, huwa mapato ni makubwa. Kwenye kupongeza ni vyema tufanye hivyo kwani tutapata amani ya moyo. Kama unataka Serikali ifanikiwe kwenye ukusanyaji wa mapato ya kuleta maendeleo lazima utafurahi but kama hautaki Serikali ifanikiwe, hata ikusanye kiwango gani lazima utaponda tu.
 
Siamini kama mwanadamu amefikia hatua ya kufanana kifkra kiasi cha kushindwa kuhoji, kudadisi na kutafakari juu jambo lolote, ulikuta jamii inamfanano wa fikra ujue hiyo jamii imejaa wendawazimu watupu
 
Back
Top Bottom