Makuruta walipogeuzwa asusa kwa kubakwa ndani ya jeshi la Marekani….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makuruta walipogeuzwa asusa kwa kubakwa ndani ya jeshi la Marekani….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 12, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Stafu Sajent Delmar Simpson.

  [​IMG]
  Kapteni Derrick Simpson
  [​IMG]

  [​IMG]
  Kwa jeshi la Marekani kashfa si jambo geni. Likiwa na idadi ya wanajeshi zaidi ya milioni moja, nusu wakiwa ni wanawake na nusu wanaume itakuwa ni vigumu kutarajia vinginevyo. Likiwa limekusudia kujenga taswira nzuri mbele ya jamii ya Wamarekani na dunia kwa ujumla, jeshi hilo limekuwa limejijengea utaratibu wa kusimamia lenyewe matatizo yao yanayohusiana na makosa mbalimbali yanayofanywa na wanajeshi ndani ya jeshi hilo.

  Hata hivyo pamoja na juhudi hizo, kuna wakati kuliibuka kashfa ya mapenzi ya wanajeshi wa kike kubakwa na maofisa wa ngazi za juu jambo ambalo kutokana na uzito wake, lilivuja na kuibukia katika vyombo vya habari nchini humo. Kashfa hiyo iliibukia katika kambi ya jeshi ya Aberdeen iliyoko katika jimbo la Maryland batalioni ya 143.

  Mnamo Novemba 7, 1997, afisa mmoja wa ngazi za juu katika batalioni hiyo aliibuka na kutangaza kwamba maofisa watatu wa jeshi hilo wameshitakiwa kwa makosa ya ubakaji, kutishia na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya makuruta wa kike ambao wako chini ya vikosi vyao na pia alibainisha kwamba kuna kesi 17 zinazofanana na hizo ambazo bado zinachunguzwa.

  Afisa huyo alisema kwamba hiyo ni kashfa kubwa kuikumba kambi hiyo tangu kutokea kwa kashfa katika kambi ya Tailhook iliyoko jimbo la Nevada katika mji wa Las Vegas hapo mnamo mwaka 1991, ambapo wanawake zaidi ya 100 waliokuwa katika kambi hiyo walilalamika kwamba walifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na askari wa majini katika kambi hiyo. Hata hivyo hakuna afisa yeyote aliyeshitakiwa kwa makosa hayo na kulikuwa juhudi za makusudi za kufichwa kwa tuhuma hizo ili kulisafisha jeshi hilo.

  Ili kuepuka makosa yaliyotokea katika kambi ya Tailhook, jeshi hilo lilitangaza kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na madai hayo ya unyanyasaji wa kijinsia sio tu katika kambi hiyo ya Aberdeen bali pia katika kambi zote za jeshi hilo nchini humo na kambi nyingine zilizoko nje ya nchi hiyo.Uongozi wa jeshi hilo uliahidi kwamba kila kesi itachunguzwa kwa makini na kitengo cha uchunguzi wa makosa mbalimbali katika jeshi hilo. Kwa taarifa hiyo, ikawa imevunja ule utaratibu wa jeshi hilo kufanya uchunguzi wa kashfa zinazoibuka ndani ya jeshi hilo kwa usiri mkubwa.

  Maofisa wa ngazi za juu katika jeshi hilo walishangazwa baada ya kupokea simu zaidi ya 4,000 ndani ya wiki mbili, nyingine zikielezea makosa ya unyanyasaji yaliyofanywa na wanajeshi wa jeshi hilo wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Zaidi ya simu 100 miongoni mwa simu hizo zilizopigwa zilitoka katika kambi hiyo ya Aberdeen.

  Hata hivyo simu nyingi kati ya zilizopigwa hazikuzungumzia kashfa ya vitisho kwa makuruta au ubakaji bali zilielezea kuhusu mahusiano ya kimapenzi kati ya maofisa wa ngazi za juu katika jeshi hilo na makuruta walioko katika vikosi vyao.

  Jeshi hilo lina sheria mahsusi inayokataza mahusiano ya kimapenzi kati ya askari wa ngazi ya juu na askari wa cheo cha chini ambao wako chini ya amri zao. Kwa kesi zinazohusiana na mahusiano ya kimapenzi kati ya maofisa wa vyeo vya juu wenyewe kwa wenyewe, jambo hilo linaweza kushughulikiwa, lakini bila kupewa uzito, lakini kama litahusisha askari wa cheo cha Sajenti na Kuruta ambaye yuko chini ya amri yake katika kikosi chake, jambo hilo litapewa uzito wa hali ya juu. Kwa mujibu wa sheria za jeshi hilo, kesi za namna hiyo huchukuliwa kama ni uvunjaji wa sheria katika jeshi hilo ambao hauvumiliki.

  Kashfa ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia katika kambi hiyo ya Aberdeen awali iliibuliwa na kuruta mmoja mzungu aliyetajwa kwa jina la Jessica Bleckley ambaye alimtuhumu Stafu Sajenti mmoja aitwae Nathaniel Beach. Alimtuhumu askari huyo kwamba alimnyanyasa kijinsia.Kitendo cha kuruta huyo kutoa malalamiko yake dhidi ya bosi wake kiliwashawishi makuruta wenzake ambao nao waliibuka na tuhuma mbalimbali za kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na maofisa wa jeshi hilo ambao wako chini ya amri zao.

  Jambo ambalo liliwashangaza maofisa wa jeshi hilo waliokuwa wakichunguza juu ya tuhuma hizo ni kugunda kwamba miongoni kwa tuhuma hizo, nyingi zilielekezwa kwa afisa mmoja Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyekuwa na umri wa miaka 30 Stafu Sajenti Delmar Simpson.

  Walipoulizwa ni kwa nini hawakuja mapema kutoa taarifa hizo, wengi wa makuruta hao walidai kwamba, Simpson aliwatisha kwamba, iwapo watatoa taarifa juu ya vitendo alivyowatendea, atawauwa.

  Baada ya uchunguzi, Simpson alikamatwa na kuwekwa ndani akisubiri kufikishwa katika mahakama ya kijeshi ya jeshi hilo. Alikuwa anakabiliwa na makosa mengi yakiwemo makosa nane ya ubakaji dhidi ya makuruta watatu na kesi nyingine sita za kulazimisha kulawiti.

  Mmoja wa makuruta hao alidai kwamba alibakwa na kunyanyaswa kijinsia na askari mwingine wa cheo cha juu ambaye alikuwa ni bosi wa Simpson aliyekuwa na cheo cha kapteni aitwae Derrick Robertson ambaye na yeye kama Simpson alikuwa ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika.

  Robertson alihojiwa na jopo la askari wa upelelezi katika jeshi hilo ambapo alikiri kuwa na uhusiano na Kuruta mmoja lakini alikanusha kumbaka kuruta huyo. Kapteni Robertson na yeye alitakiwa kufikishwa katika mahakama ya kijeshi na kama akikutwa na hatia yeye na Simpson wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela.

  Uamuzi wa jeshi hilo kutangaza kuhusu kukamatwa kwa askari hao hadharani kulikuwa kunakabiliwa na changamoto mbalimbali, lakini mbaya zaidi ilikuwa ni kuhusishwa kwa jeshi hilo na ubaguzi wa rangi kwa sababu asilimia 90 ya askari waliokamatwa na kuhusishwa na kashfa hizo ni weusi na asilimia hiyo hiyo 90 ya waathirika wa kufanyiwa vitendo hivyo ni mabinti wa kizungu.Hata hivyo Askari hao wa upelelezi wa jeshi hilo walisisitiza kwamba, wamebaini hakuna swala la ubaguzi wa rangi katika swala hilo na kueleza kuwa miongoni mwa watuhumiwa katika kashfa hiyo wengi wa Ma-Sajenti waliotuhumiwa katika kambi hiyo ya Aberdeen ni weusi.

  Wakati upelelezi wa kashfa hiyo ukiendelea ilibainika pia kwamba matukio hayo ya makosa ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa makuruta katika kambi hiyo ya Aberdeen na baadhi ya kambi nyingine za kijeshi nchini humu yamekuwepo kwa miaka kadhaa bila kuripotiwa.Hata hivyo vyombo vya habari nchini humo vilihoji, inawezekana vipi mambo hayo yatokee ndani ya jeshi hilo halafu maofisa wa ngazi za juu wasijue?

  Mwanamke mmoja ambaye ni afisa wa cheo cha juu katika jeshi hilo alikubaliana na maoni ya baadhi ya vyombo ya habari. "Ninaweza kuweka dau hata la dola milioni moja, baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wanafahamu kinachoendelea ndani ya jeshi hilo kwa muda mrefu tu. Inapotokea unafanyiwa vitendo vya unyanyasaji mara kadhaa, wengine wanashindwa kuvumilia na kutafuta namna nyingine."

  Mwanamke mwingine afisa wa cheo cha juu akiwa na miaka kumi ndani ya jeshi hilo alieleza jinsi alivyopata misukosuko kiasi cha kuhatarisha matarajio yake kitaaluma baada ya kutoa madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya afisa wa ngazi za juu katika jeshi hilo. "Tatizo ni kwamba, wale askari wanaochunguza kashfa za ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia jeshini nao ni wahusika wakuu wa vitendo hivyo." Alisema mwanamke huyo.

  Wakati wakihojiwa, askari wengi wa jeshi hilo walishtushwa na tuhuma hizo na waliogopa sana. Lakini kuhusu swala la mahusiano ya kimapenzi miongoni mwa wanajeshi, askari hao hawakushangazwa na tuhuma hizo, kwani jambo hilo halikuwa geni kwao.

  "Ni kweli jambo hilo lipo. Tunakula pamoja, tunalala na kufanya kazi pamoja, mvuto wa kimapenzi hauepukiki, sio swala la kujiuliza inakuwaje ni kwamba makuruta wanakuwa na mahusiano na mabosi wao ambao ni Ma-Sajenti ili kupata upendeleo maalum na afuweni ya suluba za jeshi." Alisema askari mmoja.

  Maofisa wa ngazi za juu katika jesho hilo waliweka wazi kwamba kutakuwa hakuna tena uvumilivu katika vitendo vya aina hiyo (Zero Tolerance) na watakaobainika watafukuzwa katika jeshi hilo. Hata hivyo hawakuishia hapo, walibainisha kwamba wameanzisha madarasa ya kufundisha makuruta namna ya kuzuia vitendo vya ubakaji.

  Mpaka kufikia Machi 1997, zaidi ya makuruta 50 walijitokeza na kutoa madai yao ya unyanyasaji wa kijinsia waliokuwa wakifanyiwa na mabosi wao katika kambi hiyo ya Aberdeen, zikiwemo tuhuma 27 za kubakwa. Ma-Sajenti 8 na afisa mmoja wa cheo cha juu walishitakiwa na wengine 20 walikuwa wakichunguzwa.

  Kwa kile kilichoonekana kama kulikuwa na tuhuma za kupikwa pia, makuruta watano wote wakiwa ni wazungu walibainisha kwamba walitoa madai ya uongo kuhusu kubakwa na Ma-mabosi wao wenye vyeo vya Sajenti wenye asili ya Afrika ambao ndio waliokuwa wakurufunzi wao. Walidai kwamba waliamuriwa na maofisa wa jeshi hilo waliokuwa wakichunguza kesi hizo ambapo waliwaahidi kuwapa kinga wasishitakiwe kwa kuwa na mahusiano na maofisa wa vyeo vya juu vya jeshi hilo……

  "Nilikubali kusema kile walichotaka kukisikia ili niweze kuepukana na kadhia hiyo." Alisema askari mmoja mwenye cheo cha Private aitwae Brandi Knewson. "Nilikuwa nataka kuachana na kazi hiyo na kutafuta ustaarabu mwingine wa maisha yangu." alibainisha mwanajeshi huyo.Maelezo hayo ya Brandi yalifanana na ya Kathryn Leming kuruta aliyeacha jeshi.

  Hata hivyo Luteni kanali Gabriel Riesco mkuu wa kambi hiyo ya jeshi ya Aberdeen alikanusha madai ya makuruta hao watano, kwamba walilazimishwa kutoa ushahidi wa uongo dhidi ya maafisa watano wenye asili ya Afrika. "Swala la ubaguzi wa rangi halikuwa ndio ajenda kuu katika uchunguzi wa kashfa hiyo, ulikuwa ni uchunguzi uliohusu dhambi na si rangi ya ngozi ya mtu," Alisema Luteni kanali Gabriel Riesco.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ijumaa hii kama kawaida nimekuja na kashfa hii ya ubakaji katika jeshi la Marekani. Naamini si Marekani tu na si kwa jeshi tu, hata hapa nchini kwetu, mambo haya yapo sana, kwa wale waliopitia JKT miaka ile ilipokuwa ni lazima kufanya hivyo baada ya kumaliza kidato cha sita watakuwa ni mashahidi wazuri wa jambo hili. Huko makazini nako pia sio salama, wanawake hupewa nafasi za upendeleo kutokana na rushwa ya ngono hata kama wanastahili.

  lakini pia wapo wasio na uwezo mahali pa kazi lakini kutokana na kuwashawishi wakubwa zao kwa kuwapa ngono huibuka kama uyoga kwa kupanda ngazi mfululizo hadi kufikia ngazi ya juu kabisa wakati uwezo wao kitaaluma ni wa kutiliwa mashaka. Vyuoni nako si salama pia, na ndio sababu ya kuibuka msemo maarufu wa Degree za chupi, kwamba baada a mwanamke kutoa rushwa ya ngono bila kujali kama ana uwezo wa darasani au la mwisho wa siku anaibuka kidedea kwa kufaulu vizuri na kujitwalia Degree yake bila jasho......
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Thanks Mtambuzi
  Mambo haya yapo sana kwa hawa wa jeshi.mh!

  Lakini saingine makuruta wenyewe wanajigonga kwa wakuu ili wapate favor za kijinga jinga
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Umesahau siku hizi kuna viti maalumu na chupi maalumu, bado kuna uDC n.k!
   
 5. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  HIZI THUMA NI NDIO YA SIO, INAWEZA KUWA SIO ILA NI NDIO KIUNDANI!!!! Tuangalie frm 3 points of view

  1. Binti Kilaza na Anategemewa kwao!!! Huyu kupata BCHELOR IN CHUPINIZATION nampongeza sana sababu hata asingefanya magumashi ya JASIRIAMWILI angeisoma namba, no cheti, no kazi, full kufulia, na kurudi kujasiriamwili kwa bei poa. Hapo kapata ji cheti, GPA Uppersecond, akienda ofisini ANAJASIRIA MWILI KWA GHALI SANAAAA!, ANAPATA JICHEO, NDO KESHATOKA KIMAISHAA HIVOOO! Mtasonyaje kimya kimya!!!!!

  2. Binti ana akili ila apenda sana vya bure, hivo anawachuna MAPROFF kwa kwenda mbele for MARKS N CASH!!! Huyu kusema kweli kwake MAJUTO NI MJUKUUU TU!!!!

  3. Binti mzuri, hagawi kidude, akili za kawaida! Huyu akimaliza GPA PASS AU LOWER SECOND!!! Kazi hatowahi kupata coz haoneshi ushirikiano kwa VIBOSILE, hata akipata kitengo cha jua kali, mshahara wa mawzo. HUYU ATAKULA KWA JASHO LAKE SANAAA! Atangoje sanaa KUTOKA KIMAISHA!

  Hahahaaaaaaaaaaaaa!
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mumie kauga wanaita vitu maalum!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. amu

  amu JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 7,979
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Hyo hata huku ipo ila kama utujuavyo
  halafu nilivyomaliza chuo mzee akaniambia niende uhamiaji au jeshini kisa yeye ni mjeshi
  loo namshukuru mama yangu akamchana live akamuambia unamtaka apewe miukimwi na vizee vya huko??
  Yani jeshini mhhh ila huku bongo ngono changanya na uchawi
  inasikitisha sana
  swali je na wavulana kweli hawapumuliwi kisogoni?
  Samahani kama umeliongelea hili maana sijaisoma yote
   
 8. mdida

  mdida JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  yapo sana, sio jeshin tu hata kwenye PRIVATE COMPANY ili binti apate kazi mpaka avue chu******p kwa kweli rushwa ya ngono imetawala, kuna mdada tunafanya nae office moja yaani yeye akichelewa kutuma report haulizwi wala hafokewi ila kama ni mwenzangu au mimi maana tuko watatu cha moto tutakona, unakutana na verbal warning na unakuta ujafanya maksudi may be network problem, achana na K ni noma naadhiri yangu siwezi kuwa na mahusiano na workmate maana no heshima.
   
 9. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Fikra angavu zimetoweka, watu siku izi tunafanya mambo holele holela, hata atujiulizi hili jambo matokeo yake ni yepi........ Bure aghali :spy:
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hii ndo dunia, uwanja wa fujo. Lakini kwa kesi ile ni kweni inajionesha ilikuwa ya kupika fulani.
  Wazungu wakija huku twatamani tuwalambe hadi nyayo za miguu, wakati waafrika wakienda ulaya wanatamani wawatupe jalalani wawe re cycled.
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Uzuri huko mbele kwa wenzetu mtu akianza kufunguka upelelezi utaanzishwa na kufuatilia suala zima.
   
 12. I

  IDDI SAIDI New Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ndio hali halisi iliopo katika maisha yetu duni ya kiuchumi ambayo huenda inasababiswa na ukoloni mambo leo.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ni tamaa tu inatuponza wanawake. I am so proud of my parents, kwa kunijengea msimamo kuwa i dont need anything material to be happy.
  Nilipomaliza chuo tu, nikiwa mdogo sana than peers, nilipata ajira kwenye taasisi ya serikali. Siku nasign mkataba, hr alinionya about boss wangu. Aliniambia wazi ni mroho wa mabinti, lakini kama ukiamua kuwa na msimamo he is diplomatic. Akikuonea kwa kazi uje tutakulinda manake tunamjua. Well, hakusita kuniambia hata yeye ananimezea mate.
  Nilifanya kazi hapo kwa shida. Mshahara mdogo sana na alihakikisha sipati safari hata moja! Isipokuwa akiwa na trip nje ya nchi alinishawishi 'nimsindikize'. Tulikuwa tunawekeana bets kuwa hatokaa anipate, na yeye ananiambia utanasa tu. Nilitafuta kazi nikahama. Recently tulikutana kwenye hotel moja kubwa. After my meal nikaenda kumsalimia, just to show him life went on well after all! He offered me a drink and i refused.
  Ukiachia wanawake wanaobakwa, na kwenye mazingira ambayo ni ya kushtukiza, wanawake tunaingia tamaa ya advantage. Niliteseka for 8 months, but i wasnt desperate at all. Mshahara ulitosha lunch tu na kuna gari ya ofisi ya bure. Alinishawishi nihamie kwake kuna servant quarter ya bure, nikagoma. Aliahidi kuniwekea some amount kila mwezi kwenye account yangu for no reason wala masharti (5x my salary) nikagoma. Looking back, kile kibabu hata ningetembea nacho kingeniharibia dira ya maisha yangu kwa senti chache tu. Nilipambana kuhakikisha nafanya long term plans na zimelipa kwa kweli.

  This is for all the young men and women mnaopata sexual harassment makazini na shuleni. I promise you, hailipiii! Fanya long term plans! Kama huna akili, soma hadi uloweke miguu na vitabu kwenye maji. Kama huna elimu, nenda shule ili ustahili position yako hata evening class. Kama mshahara hautoshi, fanya kazi za ziada ama tafuta kazi ingine fastaaa! There is no, absolutely no reason to give in to sexual harrassment just becoz you need money or a job. Hata kama ni maskini kiasi gani, hailipiii!
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  lara 1, usimpongeze alietoka familia duni kujiuza ili afaulu mtihani ama maisha. My friend wa olevel alifukuzwa kwao baada ya kumkataa baba wa kambo. Alisomeshwa kwa michango ya wanaume kuanzia makondakta wa mabasi na by the time anafika chuo wafanya biashara nao wakawa donors wake. Kasoma kifahari sana, hela nje nje. Nilikutna nae few months before kumaliza chuo, sikumtambua. Hiv imemtandika kisawasawa. Nilisikia alipomaliza chuo she was sick ilibidi chuo kiandae mtu wa kumpeleka kwao. She was the best student, graduu walimgongea brass band, hopefully alitabasamu akiwa kaburini. She died. Baada ya kuhangaika kusoma na yote, na gpa ya first class!!!
  Bible inasema, itamfaa nini mtu aje apate ulimwengu wote. Nae mwenyewe aje apTe hasara ya nafsi yake?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Hili unalosema ni kweli, afu limeendana na INJILI ya leo!!! LOL! Unachosema ni kweli endapo tu mtu atdhibiti tamaa mpaka mwisho!!! na kuishi katika neno mpaka mwisho! Tatizo siku hizi mtu chuo, mshika dini, akimaliza KIUPEPO CHA UNEMPLOYMENT kikimpausha kidogo basi anaanza kuwa CHARITABLE kwa vikongwe vya jiji hili! Sasa si bora angenza zamani?, Kweli wadada turidhike na TUJASIRIEMALI NA SIO KUJASIRIAMIILI. Kama wanaume wanapata kihalali hata sie tunaweza kupata kihalali!!! LOL!
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Room mate wangu wa chuo alikuwa anasema nikitembea na lecturer ni kwa sababu nimemtamani na sio kwa ajili ya marks. It is not worth it! I agreed with her.

  Na siemi hivi kwa sababu mie mtakatifu, no! Chagua dhambi ili hata shetani asikucheke (za epa zikinipitia sicheki nazo wallah! Ila za mwili mhhh!)Kuna mdada alitembea na boss bot, akapata kazi. Yule jamaa akapata WB job, akasepa. Kumbe mmama alieshika kiti aliijua story. Dada alipigwa vijembe, akachukua sebbatical leave akaenda phd uk ati kwa kujilipia. Akachemsha after a year akarudi, mmama boss akakomaa huwezi futa likizo. Ilibidi aache kazi ili ppf zimtoe. She is still jobless miaka 7 sasa, sijui siku zote anategemeaga gstring?
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Huku kwetu ukifunguka wasipokuua bahati yako. Umeona MBILIA anavyojishauri manake mtuhumiwa ni hakimu, haki mbinguni tu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. majany

  majany JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hii ya degree za chupi ipo saaaana.....kuna dada mmoja(naomba nimuhifadhi) alikua ni fundi kwenye hiyo part,na kwa sasa ni lecturer kwenye chuo flan...huwez amini kama haya mambo yapo!!!ahsante sana mkuu Mtambuzi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  imenigusa sana
   
 20. m

  mbukoi JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2014
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 253
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii post ina comment za kujenga sana. Hope MMU itarudi kwenye misingi hii ili kujitofautisha na majukwaa ya watoto.
   
Loading...