Makunganya hakupigania Uhuru, alipigania biashara yake ya Utumwa

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Huo ni muhtasari wa kile ambacho Profesa Elias Jengo wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (Fine & Performing Arts) ambaye pia ni mchoraji mahiri, atakizungumzia wakati wa maonyesho ya kazi za sanaa kuhusiana na Historia ya vita ya ukoloni dhidi ya utawala wa Wajerumani.

Maonyesho hayo ambayo yameratibiwa kufanyika Jioni ya leo ktk ukumbi wa Makumbusho ya Taifa - Posta Dar es salaam, yatatoa historia hiyo tamu kupitia michoro, filamu fupi, vitu, mpangilio wa ukumbi pamoja na maelezo ya tafiti mbalimbali.

Mnaoweza kufika mje tuungane, msioweza kufika msubiri hapa hapa nije kuwapa uhondo..
 
Bila shaka hapo historia imesahihishwa! Makunganya na yule mwenzake wa Tanga (jina nimelisahau), walivyokuwa front-liners kumkimbiza mjerumani kumbe ni kwa sababu binafsi? Mmmh..

Hapa patakuwa hapatoshi!

Fanya mambo mkuu basi, kumeshakucha!
 
weka ushahidi tuupime
 
Bila shaka unamzungumzia Abushiri (na Bwana Heri). Ni kweli watawala wengi wafanyabiashara waliwapinga wakoloni (rejea pia mifano ya watawala kama Machemba wa Wayao, kusini mwa Tanzania; Samori Toure, Nana Olum wa Itsekiri, Jaja wa Opobo na wengineo).

Hawa walipiana na wakoloni siyo tu kwa sababu binafsi za kibiashara kama ambayo unashawishika kuamni kirahisi. Ukweli ni kwamba, katika picha mkubwa zaidi, walikuwa wakitetea pia maslahi maana ya jamii zao zilizowapa dhamana.Kiujumla, walikuwa wanapinga "foreign interference in their own affairs" iwe katika maendeleo ya kiuchumi, kisiasa au kiutamaduni. Nadhani tusijaribu kurahisisha mno jambo hili.
 
Back
Top Bottom