Historia ya Kupigania Uhuru wa Tanganyika Katika Miji ya Kigoma na Ujiji 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,410
31,040
HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA KIGOMA UJIJI

Utangulizi

Ndugu yetu mmoja siku chache zilizopita aliturushia picha ya nyumba ya Suleiman Kagobe akaeleza kuwa nyumba hiyo ndipo alipofikia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950.

Wengi tulivutiwa na historia hiii khasa kwa kuona kuwa mbele ya nyumba hiyo kulikuwa umejengwa mnara kama kumbukumbu ya historia hii.

Watu wakaandika kutaka kupata historia zaidi ya Suleiman Kagobe.

Mimi nikaandika na kumtwisha mzigo huu Hamisi Hababi afanye hima atuletee historia iliyokamilika.

Hapo chini ni historia kamili ya mzalendo na mpigania uhuru wa Tanganyika Sheikh Suleiman Kagobe kama ilivyoandikwa na ndugu yetu Hamisi Hababi na yeye kama alivyoelezwa na Mzee Brambath Ali Kiyola.

Mzee Brambath Ali Kiyola pichani hapo chini alishiriki harakati nyingi za TANU Kigoma wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika wakati huo akiwa kijana mdogo katika TANU Youth League.

Karibuni.

"Nyumba hiyo iliyopo kwenye picha ni nyumba ya marehem Sheikh Suleiman Kagobe, ambaye ndio baba wa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe, Mzee Omar Suleiman Kagobe na M'baya Suleiman Kagobe, pamoja na dada zao watatu.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ni miongoni mwa warithi wa elimu ya Dini ya Kiislam kutoka kwa baba yake na baadae alikwenda kusoma kwa Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy Zanzibar.

Sheikh Mtumwa aliporudia Kigoma alikuwa kapata maarifa mengi ya dini na dunia.

TAA ilipoanzishwa Kigoma Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe akachaguliwa kuwa rais wa kwanza wa TAA Kigoma akiwa katika uongozi na Saadan Abdu Kandoro.

Nyumba ya kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe tangu baba yao Sheikh Suleiman akiwa hai ilikuwa mojawapo ya Zawiyatul Qadiriyya Ujiji.

Katika Tanganyika Khalifa wa Qadiriyya alikuwa Sheikh Muhammad Ramiyya wa Bagamoyo.

Qadiriyya ilikuwa na nguvu kubwa Pwani ya Afrika ya Mashariki hadi Bara Tabora, Kigoma, Ujiji hadi Upare, Moshi na kupanda Machame Nkuu Kilimanjaro.

Hii ni historia inayohitaji muda wake maalum kuihadithia; kote huko bendera ya Qadiriyya ilipepea.

Qadiriyya chini ya uongozi wa Sheikh Hassan bin Ameir ina historia ya pekee katika kueneza Uislam na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wanazuoni maarufu kutoka Dar es Salaam, Mombasa, Tanga na Zanzibar walifika Ujiji katika Zawiyya iliyokuwa nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe kusomesha.

Miongoni mwa wanazuoni wa kukumbukwa kufika na kufundisha Ujiji ni Sheikh Al Amin bin Ali Mazrui kutoka Mombasa, Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy.

Nyumba hii ilisomesha dini kwa ukamilifu wake wote na haikubaki nyuma katika medani ya siasa za kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndiye mtu aliyekuja na kadi za kwanza za TANU na alikabidhiwa Dar es Salaam na Sheikh Hassan bin Ameir azifikishe Kigoma na Ujiji.

Kadi hizi zilianza kuuzwa majumbani kwa siri na Bi Mwanzige bint Khamis Kazukamwe.

Kwenye harakati za kudai uhuru, nyumba hii ikawa ndiyo ikifikiwa na wageni mbalimbali kutoka kila upande wa Tanganyika.

Ugeni mashuhuri ambao hautosahaulika ni ule wa uongozi wa TANU Makao Makuu, New Street Dar es Salaam ukiongizwa na Rais wa TANU Julius Nyerere, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Sheikh Suleiman Takadir na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU Bi. Titi Mohamed.

Katika ziara hii ya kukumbukwa ni hotuba ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir ambaye katika hotuba yake ya Ujiji Sheikh Suleiman Takadir alikuwa akinukuu aya mbalimbali za Quran Tukufu.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa hodari wa kutoa hotuba kama hizi.

Ziara ya pili nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ilikuwa ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alipokuja kuifanyia kampeni TANU iliyotishiwa uimara wake na baadhi ya masheikh waliokuwa UTP wakiongozwa na Sheikh Omar Kakolwa na Sheikh Mussa Rehani.

UTP ilikuwa ikifadhiliwa na mfanyabiashara mkubwa Gullamhusein Rajabali Ladak na nduguze Kamrudin Rajabali Ladak na Sadrudin Rajabali Ladak.

Familia hii ya Kiasia ilkuwa na ushawishi sana katika jamii ya Waafrika wa Kigoma na Ujiji wakati huo.

Kwenye ziara hii ndiyo Sheikh Hassan Bin Ameir alimshawishi Sheikh Mussa Rehani na Sheikh Omar Kakolwa kuhama UTP na kuingia TANU na Sheikh Mussa Rehani akakabidhiwa kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji.

Kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika na mbio zake, kati ya mwaka 1962 mpaka 1963, Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe alihamia Ukerewena na hapo nyumbani akamuacha mdogo wake Mzee Omar Suleiman Kagobe.

Serikali na chama cha TANU waliamua kuweka kumbukumbu ya historia hii kwa kujenga mnara huo unaoonekana pembeni mwa nyumba na ungalipo mpaka sasa.''

1684686761177.png

1684686898095.png
 
Mimi sio mtabili, ila kwenye huu uzi lazima dini ya mnyaazi mungu imeingizwa na kupambwa kwa kuonesha ilihusika kupigania uhuru wa bendela.
 
Ni ukweli ndugu zetu waislamu walikua kinara kudai uhuru kuliko wa imani nyingine kutokana hawakua wanufaika wa utawala wa muingereza ukilinganisha na wa imani tofauti.
Na hali ingekua kinyume chake kama waislamu wangekua ndiyo wanufaika. Ni kanuni rahisi za kiulimwengu na watu wake. Hakuna ghiliba wala haja ya kumrushia maneno mzee wetu nguli Mohamed Said.
Andiko zuri, historia adhimu.
 
Dr.
Ahsante sana.
 
Mbona inafahamika sana labda kama kuna wasomaji humu ambao hawakwenda shule kwa hio inakua hawajui.
Since time colonial african resistance was mainly in coastal areas. Sehem zote alizokaa mishionari hazikua na resistance ya ukolon.na kwa kanun rahis za kilimwengu lazima asiye nufaika hana la kupoteza katika mapambano.
Ukiona history inavyosema pioneers weng walikua ni watu waliojiajiri niliona mfano dodoma mmoja wao alikua fundi cherehen,the same to Lindi nadhan walikua madobi.
Na white collar job hakuna hata mmoja aliye champion harakat except mwalimu ambaye nae ilibidi aache kaz ili aingie mapambano.therefore 85% ya uhuru lazima tutaona majina ya aina fulan hilo halikwepeki.
 
Julaibibi,
Kabla Mwalimu Nyerere hajafahamiana na Abdul Sykes alipokuwa akija Dar es Salaam kutoka Pugu alikuwa anakwenda Temeke kwa Joseph Kasella Bantu kama mwenyeji wake.

Harakati zilipopamba moto Mwalimu akawa akija Dar es Salaam anafika kwa Abdul Sykes nyumbani kwake au ofisni kwake Kariakoo Market Abdul alipokuwa akifanyakazi kama Market Master.

Hapo Kariakoo ndiko Nyerere alipofahamiana na watiu wengi wa mjini kama Mshume Kiyate, Shariff Abdallah Attas kwa kuwataja wachache na hawa wote ndiyo walikuja kumuunga mkono ndani ya TANU.
 
Back
Top Bottom