Kwa Sykes Wanarejewa na Kurejewa Katika Historia ya Uhuru wa Tanganyika?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
MUULIZAJI KAULIZA KWA NINI SYKES WANAREJEWA NA KUREJEWA?
''Nauliza hakuna familia nyengine ila ya akina sykes ilo shiriki?
Kugomboa tanganyika naona kila mara tunawarejea hao hao?''

Namjibu:

NYARAKA ZA SYKES KATIKA HISTORIA YA TANGANYIKA

Siku nilipofunguliwa sefu iliyokuwa na nyaraka za Sykes nilipata mshtuko mkubwa usio na kifani.

Historia ya mimi kufikia hapo ni ndefu atakae kuijua inabidi asome kitabu cha Abdul Sykes.

Kwa ufupi nyaraka na kumbukumbu nyingine zinarudi nyuma hadi 1890s.
Ilikuwa kama vile narudi kinyumenyume katika historia.

Nikapewa taarifa kuwa nyaraka hizi zilikataliwa kuwa sehemu ya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika mwaka 1962.

Matokeo yake ikawa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ikawa inasomeshwa bila ya mchango wa akina Sykes.

Baada ya miaka mingi historia hii ikapotea.
1998 nikaandika kitabu kilichochapwa London.

Kitabu hiki kilipindua historia iliyokuwapo.
Kitabu kikatiwa katika Cambridge Journal of African History.

Hapa nyumbani kitabu kikasababisha taharuki kubwa.

Waliosoma kitabu wakauliza iweje mipango ya ukombozi iwe toka 1929 na iliasisiwa na Kleist Sykes na kundi la vijana wa mjini akina Mzee bin Sudi lakini historia imewafuta?

Waliposoma historia ya Abdul Sykes hali ikawa mbaya zaidi.

Prof. Haroub Othman akamkabili Mwalimu na hoja kuwa lazima na yeye Mwalimu aeleze historia yake kwa kuwa tayari historia ya Tanganyika imepata mashujaa wengine.

Bahati mbaya Waislam ndiyo wakawa wametawala historia ya ukombozi wa Tanganyika.

Mjadala huu umetawala mitandao ya kijamii na kila FM Station, Online TV na AZAM TV, TBC 1 wamenihoji si mara moja.

Pandora's Box imefunguka.

Hakika ni historia ya kipekee ukisoma mswada alioacha Kleist Sykes kabla hajafa 1949 anavyoeleza uhusiano wa jeshi la Wazulu lililoingia Tanganyika likiongozwa na Hermann von Wissmann.

Mswada huu uko Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam toka 1968.
Vita na Abushiri na Mkwawa.

WW I watoto wa hawa Wazulu wanapigana na Waingereza chini ya von Lettow Vorbeck 1914 - 1918.

Wajukuu wanapigana na Wajerumani WW II KAR Burma Infantry 1939 - 1945.
1950 Abdul Sykes na Kenyatta Nairobi mipango ya kupambana na Waingereza.

Yote haya kwa ushahidi wa nyaraka nyingine kutoka Rhodes House Oxford.
1953 Abdul Sykes anamuweka Nyerere madarakani.

1954 wanaunda TANU.
1955 Nyerere anaacha kazi anakwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Tanganyika hii hakuna ukoo wenye historia kama hii.
Kila siku mimi ni kuulizwa maswali kuhusu historia hii.

Na kila siku napata wanafunzi wapya.
Kitabu kinakwenda sasa toleo la 5.

Mwaka wa 2011 nilimzungumza Abdul Sykes Northwestern University, Evanston, Chicago, Illinois katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

Hiki ndicho chuo kinaongoza ulimwengu mzima katika African History.
Mhadhara wa kwanza ulikuwa University of Iowa, Iowa City.

Baada ya hapo nikamzungumza Abdul Sykes Zentrum Moderner Orient, Berlin.
Hii ni taasisi kubwa Ujerumani katika utafiti wa historia.

Nilitoa paper: "Tanzania A Nation Without Heroes."

Namshukuru Allah.

Nakushukuru sana ndugu yangu kwa swali hili kwani bila ya kupata changamoto ubongo una kawaida ya kusinzia.

Nitatumia hizi ''notes'' hapa In Shaa Allah kuwasomesha wanafunzi wangu wapya.

Historia ya Kleist Sykes ipo katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press, New York 2011.

HIstoria ya Kleist Sykes ipo katika kitabu hicho hapo chini ''Modern Tanzainians,'' East African Publishing House, 1973.

1672603739909.png

1672603787561.png

1672603815124.png
1672603859922.png

1672603880586.png
 
Mzee Mohammed binafsi naamini haikuwa Nyerere binafsi alie edit history ya Tanganyika...

Wewe binafsi ulienda Ujerumani ukakuta history ya mashujaa wa Majimaji..na baadae ukakuta imebadilishwa...majina Yao halisi yamefutwa......

Kilichotokea history ya Tanzania na Tanganyika kimetokea Africa nzima..

Wakoloni wali edit history na wakaacha "vibaraka wao"wasimamie "their version"of history...
Binafsi Hadi namaliza Primary nilikuwa sijui kulikuwa na watumwa walipelekwa Marekani.... history ya utumwa ilikuwa inawataja waarabu with hate....na inawasafisha wazungu kuwa walikuja kuleta dini na ustaarabu..... Africa nzima history imejaa upotoshaji...ukienda Ethiopia...utakuta waislam wanalalamika haya haya ya kufutwa history Yao ..hata Kenya mchango wa waislam kupigania Uhuru umefuta Kwa history...

Kina Ibn Batuta hawapatikani kwenye history za mashuleni..
 
Ni kweli kabisaaa
 
Hakuna sehemu ambayo Kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anasema Wazungu hawakufanya ukoloni. Hakuna somo Hilo.

Mgogoro uliopo ni baadhi ya watu kutaka kuwaona WAARABU ni watu SAFI na kuwaondoa kwenye UKATILI wa KIKOLONI kuwa hawakuhusika na ukoloni.

Pili,Tanganyika watu hawakuoigania UHURU kwa matabaka matabaka.

Kila aliyeweza kwa nguvu na mali zake aliunganisha nguvu kuhakikisha Ukoloni unaondoka. Kuanzia Vyama vya wafanyakazi, chiefs, wasomi, wanavyuo nk.

Mwisho wa siku, hata huyo Nyerere mwenyewe hakupewa huo Uhuru kwa faida yake mwenyewe. Kila kitu kimebaki kiwa mali ya umma.

Anyway,na Mimi ngoja nianze kuandika KITABU Cha Namna watu wa MARA na Kanda ya Ziwa kwa Ujumla walivyomwaga damu zao kupigania nchi hii,na Leo wametelekezwa.
 
Mzee Mohammed binafsi naamini haikuwa Nyerere binafsi alie edit history ya Tanganyika...

Wewe binafsi ulienda Ujerumani ukakuta history ya mashujaa wa Majimaji..na baadae ukakuta imebadilishwa...majina Yao halisi yamefutwa......

Kilichotokea history ya Tanzania na Tanganyika kimetokea Africa nzima..

Wakoloni wali edit history na wakaacha "vibaraka wao"wasimamie "their version"of history...
Binafsi Hadi namaliza Primary nilikuwa sijui kulikuwa na watumwa walipelekwa Marekani.... history ya utumwa ilikuwa inawataja waarabu with hate....na inawasafisha wazungu kuwa walikuja kuleta dini na ustaarabu..... Africa nzima history imejaa upotoshaji...ukienda Ethiopia...utakuta waislam wanalalamika haya haya ya kufutwa history Yao ..hata Kenya mchango wa waislam kupigania Uhuru umefuta Kwa history...

Kina Ibn Batuta hawapatikani kwenye history za mashuleni..
Kabisaaa. Kitu kingine duniani kwote mashujaa wa ukombozi huwa hawatajwi woteee baba wa taifa hua ni mmoja tuui.

Leo South Africa unaweza dhani Mandela alikua peke yake,kenya unafikiri kenyatta alikua pekee.

Ukweli mchunguuu ni kua anae andika historia huandika yampendezayo tuu.
 
Tunachokitaka ndo hicho mnachokisema: yaani historiabitajwe kwa uhakika na ikiwa watu wanafichwa isiwe kwa nia mbaya na kwa kuchafuliwa. Ila shida ya Dunia hii inawatukiza watu wa itikadi flani wawe mahero na inawafunika watu hisiyo wataka kisa siyo watu wa itikadi hiyo.
Kuna barua ya Nyererebiliyotumwa kwenda kwa Askofu wa Bukoba Ask. Rugambwa akimwambia kuwa ๐’‚๐’Ž๐’†๐’Ž๐’„๐’‰๐’‚๐’ˆ๐’–๐’‚ ๐’Ž๐’Ž๐’๐’‹๐’‚ ๐’˜๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’„๐’‰๐’–๐’๐’ˆ๐’‚๐’‹๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐‘ฒ๐‘ฒ๐‘ฒ๐‘ป ๐’Œ๐’–๐’Ž๐’‘๐’‚ ๐’–๐’๐’๐’ˆ๐’๐’›๐’Š ๐’”๐’†๐’“๐’Š๐’Œ๐’‚๐’๐’Š๐’๐’Š ๐’”๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’Š ๐’Ž๐’‹๐’–๐’›๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐’”๐’Š๐’‚๐’”๐’‚, ๐’ƒ๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’Š ๐’Ž๐’˜๐’†๐’๐’š๐’† ๐’–๐’‹๐’–๐’›๐’Š ๐’๐’‚ ๐’Š๐’Ž๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’–๐’ƒ๐’˜๐’‚ ๐’‹๐’–๐’– ๐’š๐’‚ ๐’–๐’Œ๐’“๐’Š๐’”๐’•๐’.

Sasa mambo hayendi hivyo mnapochanganyika na watu flani lazima mfuate misingi inayotakiwa siyo itikadi flani za kidini, huu ni udini lakini nyinyi wenyewe mpaka leo mnasema Nyerer hakuwa na Udini, tukiyataja sisi mnainuka hamkubari mnabaki kusema sisi ndo tunaleta udini. Sisi tunatetea Waislaam si kwa kuwa ni wenzetu bali kwa kuwa waliotetea wakristo nao walotetea wenzao.

"๐™€๐™ฃ๐™ฎ๐™ž ๐™ฌ๐™–๐™ฉ๐™ช ๐™๐™–๐™ ๐™ž๐™ ๐™– ๐™จ๐™ž๐™จ๐™ž ๐™ฉ๐™ช๐™ข๐™š๐™ ๐™ช๐™ช๐™ข๐™—๐™š๐™ฃ๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐™—๐™–๐™—๐™– ๐™ข๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™ข๐™– ๐™ข๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™–. ๐™ƒ๐™–๐™ ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ข๐™—๐™ค๐™ง๐™– ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™ช ๐™Ÿ๐™ž ๐™ข๐™˜๐™๐™– ๐™ข๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™ช ๐™ฉ๐™ช" Al Hujurat

Mwislamu hawezi kuwa mbaguzi kwa itikadi za kuficha ukweli na kuuzika na akaushikiria uwongo ulotiwa mkazo kwa kuusambaza.
 
Mzee Mohammed binafsi naamini haikuwa Nyerere binafsi alie edit history ya Tanganyika...

Wewe binafsi ulienda Ujerumani ukakuta history ya mashujaa wa Majimaji..na baadae ukakuta imebadilishwa...majina Yao halisi yamefutwa......

Kilichotokea history ya Tanzania na Tanganyika kimetokea Africa nzima..

Wakoloni wali edit history na wakaacha "vibaraka wao"wasimamie "their version"of history...
Binafsi Hadi namaliza Primary nilikuwa sijui kulikuwa na watumwa walipelekwa Marekani.... history ya utumwa ilikuwa inawataja waarabu with hate....na inawasafisha wazungu kuwa walikuja kuleta dini na ustaarabu..... Africa nzima history imejaa upotoshaji...ukienda Ethiopia...utakuta waislam wanalalamika haya haya ya kufutwa history Yao ..hata Kenya mchango wa waislam kupigania Uhuru umefuta Kwa history...

Kina Ibn Batuta hawapatikani kwenye history za mashuleni..
The Boss,
Hakika.
 
Tunachokitaka ndo hicho mnachokisema: yaani historiabitajwe kwa uhakika na ikiwa watu wanafichwa isiwe kwa nia mbaya na kwa kuchafuliwa. Ila shida ya Dunia hii inawatukiza watu wa itikadi flani wawe mahero na inawafunika watu hisiyo wataka kisa siyo watu wa itikadi hiyo.
Kuna barua ya Nyererebiliyotumwa kwenda kwa Askofu wa Bukoba Ask. Rugambwa akimwambia kuwa ๐’‚๐’Ž๐’†๐’Ž๐’„๐’‰๐’‚๐’ˆ๐’–๐’‚ ๐’Ž๐’Ž๐’๐’‹๐’‚ ๐’˜๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’„๐’‰๐’–๐’๐’ˆ๐’‚๐’‹๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐‘ฒ๐‘ฒ๐‘ฒ๐‘ป ๐’Œ๐’–๐’Ž๐’‘๐’‚ ๐’–๐’๐’๐’ˆ๐’๐’›๐’Š ๐’”๐’†๐’“๐’Š๐’Œ๐’‚๐’๐’Š๐’๐’Š ๐’”๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’Š ๐’Ž๐’‹๐’–๐’›๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐’”๐’Š๐’‚๐’”๐’‚, ๐’ƒ๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’Š ๐’Ž๐’˜๐’†๐’๐’š๐’† ๐’–๐’‹๐’–๐’›๐’Š ๐’๐’‚ ๐’Š๐’Ž๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’–๐’ƒ๐’˜๐’‚ ๐’‹๐’–๐’– ๐’š๐’‚ ๐’–๐’Œ๐’“๐’Š๐’”๐’•๐’.

Sasa mambo hayendi hivyo mnapochanganyika na watu flani lazima mfuate misingi inayotakiwa siyo itikadi flani za kidini, huu ni udini lakini nyinyi wenyewe mpaka leo mnasema Nyerer hakuwa na Udini, tukiyataja sisi mnainuka hamkubari mnabaki kusema sisi ndo tunaleta udini. Sisi tunatetea Waislaam si kwa kuwa ni wenzetu bali kwa kuwa waliotetea wakristo nao walotetea wenzao.

"๐™€๐™ฃ๐™ฎ๐™ž ๐™ฌ๐™–๐™ฉ๐™ช ๐™๐™–๐™ ๐™ž๐™ ๐™– ๐™จ๐™ž๐™จ๐™ž ๐™ฉ๐™ช๐™ข๐™š๐™ ๐™ช๐™ช๐™ข๐™—๐™š๐™ฃ๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐™—๐™–๐™—๐™– ๐™ข๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™ข๐™– ๐™ข๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™–. ๐™ƒ๐™–๐™ ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ข๐™—๐™ค๐™ง๐™– ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™ช ๐™Ÿ๐™ž ๐™ข๐™˜๐™๐™– ๐™ข๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™ช ๐™ฉ๐™ช" Al Hujurat

Mwislamu hawezi kuwa mbaguzi kwa itikadi za kuficha ukweli na kuuzika na akaushikiria uwongo ulotiwa mkazo kwa kuusambaza.
Aya ya mwisho katika andiko lako, huwa ni ya maneno zaidi kuliko vitendo. Bahatimbaya sana wote tumenaswa kati huo mtego wa DINI yangu/yetu.
 
Me naomba kuuliza huyu msanii wa bongo flava Dully sykes huo ni pia ni ukoo wake....
Trouble...
Dully ni mjukuu wa Abdul Sykes mtoto wa Ebby Sykes.
Nakuwekea hapo chini picha ya Ebby ni marehemu.

Mimi na Ebby tulipishana siku moja kuzaliwa na tumekuwa marafiki toka udogo wetu kama baba zetu walivyokuwa marafiki.

1672660290074.jpeg
 
Tunachokitaka ndo hicho mnachokisema: yaani historiabitajwe kwa uhakika na ikiwa watu wanafichwa isiwe kwa nia mbaya na kwa kuchafuliwa. Ila shida ya Dunia hii inawatukiza watu wa itikadi flani wawe mahero na inawafunika watu hisiyo wataka kisa siyo watu wa itikadi hiyo.
Kuna barua ya Nyererebiliyotumwa kwenda kwa Askofu wa Bukoba Ask. Rugambwa akimwambia kuwa ๐’‚๐’Ž๐’†๐’Ž๐’„๐’‰๐’‚๐’ˆ๐’–๐’‚ ๐’Ž๐’Ž๐’๐’‹๐’‚ ๐’˜๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’„๐’‰๐’–๐’๐’ˆ๐’‚๐’‹๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐‘ฒ๐‘ฒ๐‘ฒ๐‘ป ๐’Œ๐’–๐’Ž๐’‘๐’‚ ๐’–๐’๐’๐’ˆ๐’๐’›๐’Š ๐’”๐’†๐’“๐’Š๐’Œ๐’‚๐’๐’Š๐’๐’Š ๐’”๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’Š ๐’Ž๐’‹๐’–๐’›๐’Š ๐’˜๐’‚ ๐’”๐’Š๐’‚๐’”๐’‚, ๐’ƒ๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’Š ๐’Ž๐’˜๐’†๐’๐’š๐’† ๐’–๐’‹๐’–๐’›๐’Š ๐’๐’‚ ๐’Š๐’Ž๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’–๐’ƒ๐’˜๐’‚ ๐’‹๐’–๐’– ๐’š๐’‚ ๐’–๐’Œ๐’“๐’Š๐’”๐’•๐’.

Sasa mambo hayendi hivyo mnapochanganyika na watu flani lazima mfuate misingi inayotakiwa siyo itikadi flani za kidini, huu ni udini lakini nyinyi wenyewe mpaka leo mnasema Nyerer hakuwa na Udini, tukiyataja sisi mnainuka hamkubari mnabaki kusema sisi ndo tunaleta udini. Sisi tunatetea Waislaam si kwa kuwa ni wenzetu bali kwa kuwa waliotetea wakristo nao walotetea wenzao.

"๐™€๐™ฃ๐™ฎ๐™ž ๐™ฌ๐™–๐™ฉ๐™ช ๐™๐™–๐™ ๐™ž๐™ ๐™– ๐™จ๐™ž๐™จ๐™ž ๐™ฉ๐™ช๐™ข๐™š๐™ ๐™ช๐™ช๐™ข๐™—๐™š๐™ฃ๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐™—๐™–๐™—๐™– ๐™ข๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™ข๐™– ๐™ข๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™–. ๐™ƒ๐™–๐™ ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ข๐™—๐™ค๐™ง๐™– ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™ช ๐™Ÿ๐™ž ๐™ข๐™˜๐™๐™– ๐™ข๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™ช ๐™ฉ๐™ช" Al Hujurat

Mwislamu hawezi kuwa mbaguzi kwa itikadi za kuficha ukweli na kuuzika na akaushikiria uwongo ulotiwa mkazo kwa kuusambaza.
Hivi hizi dini mnazozipambania kila siku mngefanya hivi kupambania mila na desturi za mwafrika si tungekua mbali sana. Kwanini bado mnapenda utumwa? Je babu zenu hawakuwa na dini zao zilizowafaa?
 
Wewe kanisa lako ni lipi?
 
Hivi hizi dini mnazozipambania kila siku mngefanya hivi kupambania mila na desturi za mwafrika si tungekua mbali sana. Kwanini bado mnapenda utumwa? Je babu zenu hawakuwa na dini zao zilizowafaa?
Hatupambanii Dini, tunqpambania Uhalisia na ukweli. Ukijikuta unatetea kuabudiwa jiwe na mti na mizimu wakati mizimu ni ya watu walioshindwa kujirudishia uhai walipotaka kufa, vipi wakusaidie wewe. Huo ndo uafrika na ndo imani za waafrika ATR, naanzaje kutetea vitu visivyo na ukweli?
 
Back
Top Bottom