zitto binafsi anafahamu kuwa yeye, mbowe na slaa kila mmoja anapambana kikamilifu ili kuhangaikia uteuzi wa kugombea uraisi katika uchaguzi mkuu ujao, lakini anaelewa ni jinsi gani inabidi apambane na ubanguzi mkubwa wa ukabila na ukanda.mwaka 2015, kazi inayofanywa kwa kutumia ushawishi wa kisiasa na kifedha. anafahamu kuwa kamati kuu ya chadema imerudikwa na watu wanaotoka kilimanjaro ili wawe na nguvu, wale ambao kuna wengine ni wafanyabiashara wakubwa wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hichi katika mkoa huo, philemon ndesasamburo. viongozi wengine wanaotoka kilimanjaro ni pamoja mbowe, mkurugenzi wa habari na uenezi john mnyika, mbunge wa kawe halima mdee, mbunge wa ilemela hayness kiwia, mkurungenzi wa fedha na utawala anthony komu na mkurugenzi wa bunge na halmashauri john mrema
Kundi hilo pia linasaidiwa na wabunge kama akina peter msingwa [iringa mjini] ezekieli wenje [nyamagana] joseph mbilinyi [mbeya mjini] joshua nasari [ arumeru mashariki] vincent nyerere [ musoma mijini] saidi arfi [mpanda mjini] mbunge wa zamani wa arusha mijini godbless lema.
SOURCE: gazeti la sauti huru