Makundi hatarishi kwa Uhai wa CHADEMA

Makundi hatarishi kwa Uhai wa CHADEMA

So ipi ni best option? Nilikwambia sasa ni CUF nikimaanisha upepo wa kumuunga mkono Magu sasa umehamia CUF unashauri nini?

Halafu hilo neno kwamba haipo kama zamani si zuri kutolewa na mtu mwenye exposure tena ya Russia kama wewe!! Ukitaka kila kitu kiwe kama zamani itabidi nawewe urudi hatua ya kutambaa!!

Amka kijana majira yanabadilika na mambo pia hubadilika!!

Mkuu upepo wa kumuunga mkono magu tunajua jinsi unavyofanya kazi,kwanini watu ambao wapo kwenye chama ambayo ipo kwenye muunganiko wa ukawa wamwunge mkono?

ningependa tujikite kwenye hoja na siyo personality mkuu
 
Mkuu chadema inatakiwa ijipange upya,mikakati yake sasa hivi hamna nguvu

Mkuu nimeona hoja zako na zina mashiko na kila mtu anajua hilo tatizo. Sasa ule uchaguzi wa juzi kulikuwa na haja gani ya ccm kutumia ukatili wa kiwango kile tena kwa kushirikiana na polisi? Unadhani hayo makosa ya cdm ndio yanaipa ccm uhalali wa kufanya ukatili kiasi kile? Je kile kitendo cha rais kupokea madiwani waliopatikana na rushwa mbele ya hafla ya kijeshi, kuna uwezekano wa vyama vya upinzani kupambana tena na hicho kikundi cha kijeshi kinachoitwa ccm? Hii kununua wapinzani ndio udhaufu huo wa upinzani unaousema?
 
Subiri wale wenye mihemko waje watakutukana mpaka basi hapa ....ngoja Babati na Salary slip waje uone watakavyokunanga......


Hao watu wameshakua sikio La kufa
hivi ni vitu ambavyo viko wazi,je ni wangapi wametepuuzwa kwenye kusimamishwa katika uchaguzi kwa ajili ya waliohamia?
 
Dr.Slaa alipokuwa katibu mkuu chadema mbona mikakati na mbinu mpya ilikuwa inapatikana?

Dr. Slaa angekuwepo leo na zile siasa zake angekuwa kashapigwa risasi muda mrefu sana. Mazingira yale sio haya.
 
Dr.Slaa alipokuwa katibu mkuu chadema mbona mikakati na mbinu mpya ilikuwa inapatikana?

Viol,

Mkuu, achana kabisa na Kichwa Dr. Slaa, that guy is talented and a genius.

Ndiyo maana, katika vyeo vya uteuzi hakika bnafsi, I was so happy and proud for the uteuzi wa Balozi , Dr. Slaa.

Hadi dunia liishe na Kristo Yesu arudi hakuna Kichwa kama Dr. Slaa kitakachotokea kwa awamu ya upinzani nchini Tanzania.

Sasa hivi upinzani hawajitambui yaani, ni aibu.
 
Mkuu upepo wa kumuunga mkono magu tunajua jinsi unavyofanya kazi,kwanini watu ambao wapo kwenye chama ambayo ipo kwenye muunganiko wa ukawa wamwunge mkono?

ningependa tujikite kwenye hoja na siyo personality mkuu
Sasa kwa akili yako wanamuunga mkono kwa kweli au ghilba? Halafu mbona unatwist mada umeanza na Chadema nimekupa ya CUF unarudi na UKAWA!!

Au upo kwenye project nawewe?
 
hivi ni vitu ambavyo viko wazi,je ni wangapi wametepuuzwa kwenye kusimamishwa katika uchaguzi kwa ajili ya waliohamia?

Kama watu waliotoka vyama vingine kupewa cheo ni tatizo ndio watu wanahama mbona hatuoni wanaccm wakihama kwa kina mama Anna Mghwira, Kitila Mkumbo, Juliana Shonza kupewa vyeo huko ccm? Hoja dhaifu, kinachoendelea sasa ni siasa za kibabe na kikatili dhidi ya wapinzani na wale wenye moyo mwepesi wanahongwa ili kuhama. Hakuna nje ya hili.
 
Dr. Slaa angekuwepo leo na zile siasa zake angekuwa kashapigwa risasi muda mrefu sana. Mazingira yale sio haya.
Kwanza amesahau hata enzi za Dr slaa tumewahi pigwa kata tatu kwa chopa tatu nchi nzima kama utakumbuka mkuu!!

Huyo kijana bado hajajua hali halisi ya nchi hii au ana agenda yake anashindwa atoke nayo vipi
 
Dr. Slaa, is a genius and talented.

Yaani, Tanzania TANU/ CCM ni Nyerere na Chadema / UKAWA ni Dr. Slaa, baada ya hao watu kuondoka kwenye siasa na uongozi huo wa vyama tumebakia tunatapatapa.
 
Mkuu nimeona hoja zako na zina mashiko na kila mtu anajua hilo tatizo. Sasa ule uchaguzi wa juzi kulikuwa na haja gani ya ccm kutumia ukatili wa kiwango kile tena kwa kushirikiana na polisi? Unadhani hayo makosa ya cdm ndio yanaipa ccm uhalali wa kufanya ukatili kiasi kile? Je kile kitendo cha rais kupokea madiwani waliopatikana na rushwa mbele ya hafla ya kijeshi, kuna uwezekano wa vyama vya upinzani kupambana tena na hicho kikundi cha kijeshi kinachoitwa ccm? Hii kununua wapinzani ndio udhaufu huo wa upinzani unaousema?
Tatizo bado ni hakuna mikakati,hivi unakumbuka 2010 dr Slaa alivyopanga maandamano nchi nzima?yalikuwa yalete madhara makubwa kama siyo mbinu za kiintelijensia kumleta babu wa loliondo,wafuasi na waandamanaji wakaacha maandamano wakaona heri wafuate tiba,mbinu ya kususia bunge kaleta dr slaa hadi saa chadema na ukawa wwanatumia hawana njia nyingine?
 
Kosa ambalo CHADEMA ilifanya ni kuweweseka na watu wa kuja kiasi kwamba walitoa damu yao na kupigania chama kupuuzwa.

Wahamiaji wengi walithaminiwa kwa vyeo vyao walipokuwa serikalini au walipokuwa CCM,CHADEMA na UKAWA,walipowapiga chini wagombea wao wa urais ndani ya chama ambao walijenga chama kwa mda mrefu na kuwasimamisha ambao walikuwa upande wa pili wa chama walitegemea nini?

Waliwaza tu kwa upeo mfupi kwamba Lowasa atashinda,je asiposhinda CHADEMA na ukawa bila Lipumba na Slaa itafika wapi?


Wapingaji wa ufisadi wanamsimamisha mgombea urais waliyempigia kelele 2008 kwa ufisadi na kumnadi kwa wananchi! Sawa tunataka mabadiliko ila kwani hakuna ambaye angefaa ukawa wamsimamishe kama mgombea???

CHADEMA ilipata wabunge wengi chini ya ukatibu wa Dr.Slaa,hao wote,Lisu,Mnyika,Sugu,Lema,Nassari,Wenje,Mdee, etc walikomaa kisiasa na kulelewa na Dr.Slaa.

Hata chama ingefeli uchaguzi mkuu na mgombea ni mtu halisi ambao ni wapanga mikakati Wa zamani bado hata chama ingeshindwa wafuasi wangekuwa na imani.Chama ina mikakati gani sasa hivi na wafuasi wana spirit gani ,imeonekana kutetea maslahi tu,warembo wanakuja toka upande wa pili wanawekwa kwenye listi ya viti maalum.

Wote waliokimbia upande wa pili kwa kuumizwa au hasira wamekuja huku wameingia hadi chumbani now wameona kila kitu wanarudi kule.

CHADEMA ilitakiwa iwasimamishe watu kama kina Dr.Slaa waliotoa damu yao Arusha siyo hao ambao hawana sera wanapanda jukwaani halafu wanasema "zungusha ngumi,zungusha ngumi,mabadiliko lowasa,lowasa mabadiliko,Peoplesss power" halafu wanaondoka.


Mimi kama mfuasi leo utanishawishi nini?niingie barabarani nipigwe mawe kwa maslahi yako kisa mwañaharakati uchwara ?

Mtu anajituma jimboni miaka 5 hadi 10 anajenga chama,anajulikana halafu katika kupitsha majina ya wagombea ubunge au udiwani mnakuja kumsimamisha mamluki aliyekimbia kwao ili apate maslahi .

Kama chama ina uchungu na waliopigania 2020 imsimamishe Lissu,kuwa mgombea urais siyo hao wazungusha ngumi video ichukuliwe.

CHADEMA ijikite kuwajenga vijana waliopigania chama na kuwaweka kwenye misingi mizuri ya uongozi kama kina John Heche.

Kama kweli CHADEMA ina nia thabiti iwaandae vijana na wazee waliokuwa wametumia Nguvu zao ndani ya chama na siyo kuwavunja moyo,bila hivo hata wabunge wote watawakimbia,uchaguzi utarudiwa na watasimama kwa upande wa CCM,mawakala wa upinzani watawekwa ndani na wabunge wa CCM watashinda,sijui hizo Nguvu ya harakati hata bungeni mtapata wapi.




Ahsante sana Mjaluo!

.....Mwingine.....
 
Kwanza amesahau hata enzi za Dr slaa tumewahi pigwa kata tatu kwa chopa tatu nchi nzima kama utakumbuka mkuu!!

Huyo kijana bado hajajua hali halisi ya nchi hii au ana agenda yake anashindwa atoke nayo vipi

Halafu wote wanaokuja kuua hii aibu ya ccm kununua wapinzani na ule ukatili waliofanya juzi kwenye uchaguzi ili kushinda wanaishia kusema sijui Mbowe ni Mugabe, mara enzi za Slaa cdm ilikuwa inakubalika. Mbona enzi hizo haikuwahi kuchukua nchi na ccm ilikuwa inajisifu inashinda kwa kishindo na kukubalika!?
 
Tatizo bado ni hakuna mikakati,hivi unakumbuka 2010 dr Slaa alivyopanga maandamano nchi nzima?yalikuwa yalete madhara makubwa kama siyo mbinu za kiintelijensia kumleta babu wa loliondo,wafuasi na waandamanaji wakaacha maandamano wakaona heri wafuate tiba,mbinu ya kususia bunge kaleta dr slaa hadi saa chadema na ukawa wwanatumia hawana njia nyingine?

Toa mbinu mpya ambaya unadhani inaweza kutumika kwa sasa kwenye mazingira mtu anapigwa risasi mchana kweupe na wengine wanatoweka bila maelezo ya kueleweka. Enzi hizo za kina Slaa kulikuwa na mikutano ya hadhara, leo hii hata mikutano ya ndani watu wanakamatwa. Enzi za JK sio kwamba aliwatendea haki sana wapinzani, lakini wangalau alikuwa anakubaliana na siasa za ushindani. Sasa hivi mwenyekiti wa ccm hawezi siasa za ushindani, na wala hawezi kujenga hoja. Katika mazingira hayo ndio unaona haya yanayotekea ya ukatili dhidi ya upinzani na kuwanunua waoga na wachumia tumbo kuuongopea umma kwamba anakubalika. Msitoe uchambuzi ambao tunaona kabisa uko ndani ya unafiki na huku mkikwepa uhalisia wa siasa za sasa hapa nchini.
 
Dr. Slaa, is a genius and talented.

Yaani, Tanzania TANU/ CCM ni Nyerere na Chadema / UKAWA ni Dr. Slaa, baada ya hao watu kuondoka kwenye siasa na uongozi huo wa vyama tumebakia tunatapatapa.
Mkuu hebu hata tafakari,plan b ya vyama vya upinzani kujikwamua kwenye hili ni lipi?
 
Halafu wote wanaokuja kuua hii aibu ya ccm kununua wapinzani na ule ukatili waliofanya juzi kwenye uchaguzi ili kushinda wanaishia kusema sijui Mbowe ni Mugabe, mara enzi za Slaa cdm ilikuwa inakubalika. Mbona enzi hizo haikuwahi kuchukua nchi na ccm ilikuwa inajisifu inashinda kwa kishindo na kukubalika!?
Kwa mtazamo wako grafu ya CHADEMA au upinzani inapanda au inashuka?
 
Dr. Slaa angekuwepo leo na zile siasa zake angekuwa kashapigwa risasi muda mrefu sana. Mazingira yale sio haya.
asingepigwa maana nguvu ya upinzani ungeongezeka
 
Halafu wote wanaokuja kuua hii aibu ya ccm kununua wapinzani na ule ukatili waliofanya juzi kwenye uchaguzi ili kushinda wanaishia kusema sijui Mbowe ni Mugabe, mara enzi za Slaa cdm ilikuwa inakubalika. Mbona enzi hizo haikuwahi kuchukua nchi na ccm ilikuwa inajisifu inashinda kwa kishindo na kukubalika!?
Ndio maana hadi Leo watu weusi tunauzwa kama wanyama huko Libya!! Akili zetu zipo imara ktk ngono si fikra!!

Fikiria mtu anaongea ya Dr Slaa enzi za ushindi wa kura Milioni mbili na wabunge 5 na enzi hizi ambapo chadema imekamata robo tatu ya miji mikubwa nchini

Chadema chini ya Slaa haikuwahi kuwa na jiji la DSM Leo chadema inaongoza DSM halafu mtu analeta alinacha za enzi hizo!!

Watanzania tu mazezeta mno linapokuja suala la critical thinking!!
 
Mkuu hebu hata tafakari,plan b ya vyama vya upinzani kujikwamua kwenye hili ni lipi?
Vyama ni watu sio machine!! Ukiwa mtu wa upinzani wewe plan B yako ni ipi tuanzie hapo!!
 
Back
Top Bottom