Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,903
- 3,139
Utamaduni wa kuwajibisha viongozi wanaofanya ubadhirifu, ufisadi na rushwa umeanza kubaki kama hadithi za kusadikika tu kwenye nchi yetu; hakuna tena mihimili yenye nguvu, mathalani mahakama zenye uwezo wa kuamua, kuheshimiwa na kutekekelezewa matakwa yake.
Miaka michache mbeleni, tutakuwa na aina ya kundi la watu wenye nguvu ambao wanaamini wanaweza kufanya jambo lolote, liwe takwa la kisheria au lah! bila kupokea uwajibikaji kutoka kwa mamlaka zozote ndani ya nchi, tutaanza kushuhudia miungu watu ambao wapo juu ya sheria.
Kwenye nchi hii, miaka michache ijayo mentalities za watu kuhusu dhana ya uongozi zitabadilika kabisa, watu watahisi nchi inatawaliwa kwa utashi tu, na si sera, kanuni na sheria zilizopo. Na jambo linaloshangaza zaidi ni kuona kundi fulani la watu wanatetea hali hii kwa sababu tu ya kulinda narratives za chama na serikali wanayoamini ina nguvu kuliko kundi la miungu watu hawa.