Makundi hatarishi kwa Uhai wa CHADEMA

Makundi hatarishi kwa Uhai wa CHADEMA

Kosa ambalo CHADEMA ilifanya ni kuweweseka na watu wa kuja kiasi kwamba walitoa damu yao na kupigania chama kupuuzwa.

Wahamiaji wengi walithaminiwa kwa vyeo vyao walipokuwa serikalini au walipokuwa CCM,CHADEMA na UKAWA,walipowapiga chini wagombea wao wa urais ndani ya chama ambao walijenga chama kwa mda mrefu na kuwasimamisha ambao walikuwa upande wa pili wa chama walitegemea nini?

Waliwaza tu kwa upeo mfupi kwamba Lowasa atashinda,je asiposhinda CHADEMA na ukawa bila Lipumba na Slaa itafika wapi?

Wapingaji wa ufisadi wanamsimamisha mgombea urais waliyempigia kelele 2008 kwa ufisadi na kumnadi kwa wananchi! Sawa tunataka mabadiliko ila kwani hakuna ambaye angefaa ukawa wamsimamishe kama mgombea???

CHADEMA ilipata wabunge wengi chini ya ukatibu wa Dr.Slaa,hao wote,Lisu,Mnyika,Sugu,Lema,Nassari,Wenje,Mdee, etc walikomaa kisiasa na kulelewa na Dr.Slaa.

Hata chama ingefeli uchaguzi mkuu na mgombea ni mtu halisi ambao ni wapanga mikakati Wa zamani bado hata chama ingeshindwa wafuasi wangekuwa na imani.Chama ina mikakati gani sasa hivi na wafuasi wana spirit gani ,imeonekana kutetea maslahi tu,warembo wanakuja toka upande wa pili wanawekwa kwenye listi ya viti maalum.

Wote waliokimbia upande wa pili kwa kuumizwa au hasira wamekuja huku wameingia hadi chumbani now wameona kila kitu wanarudi kule.

CHADEMA ilitakiwa iwasimamishe watu kama kina Dr.Slaa waliotoa damu yao Arusha siyo hao ambao hawana sera wanapanda jukwaani halafu wanasema "zungusha ngumi,zungusha ngumi,mabadiliko lowasa,lowasa mabadiliko,Peoplesss power" halafu wanaondoka.

Mimi kama mfuasi leo utanishawishi nini?niingie barabarani nipigwe mawe kwa maslahi yako kisa mwañaharakati uchwara ?

Mtu anajituma jimboni miaka 5 hadi 10 anajenga chama,anajulikana halafu katika kupitsha majina ya wagombea ubunge au udiwani mnakuja kumsimamisha mamluki aliyekimbia kwao ili apate maslahi .

Kama chama ina uchungu na waliopigania 2020 imsimamishe Lissu,kuwa mgombea urais siyo hao wazungusha ngumi video ichukuliwe.

CHADEMA ijikite kuwajenga vijana waliopigania chama na kuwaweka kwenye misingi mizuri ya uongozi kama kina John Heche.

Kama kweli CHADEMA ina nia thabiti iwaandae vijana na wazee waliokuwa wametumia Nguvu zao ndani ya chama na siyo kuwavunja moyo,bila hivo hata wabunge wote watawakimbia,uchaguzi utarudiwa na watasimama kwa upande wa CCM,mawakala wa upinzani watawekwa ndani na wabunge wa CCM watashinda,sijui hizo Nguvu ya harakati hata bungeni mtapata wapi.
 
Mkuu sasa ni CUF au upo too obbsesed na Chadema?

Then hiki kinachonendelea ni harakati za frustrated man kuzima anguko kuu linalomjilia....

Kwanza umeona hostel za watoto wetu zinavyoota nyufa? Hebu twende kwanza tukaokoe uhai wa watoto wetu achana na hizi abracadabra
 
Kaka karibu Mbozi nikupe dada yangu bure kabisa....We have to look The party and politics in 3D
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkuu sasa ni CUF au upo too obbsesed na Chadema?

Then hiki kinachonendelea ni harakati za frustrated man kuzima anguko kuu linalomjilia....

Kwanza umeona hostel za watoto wetu zinavyoota nyufa? Hebu twende kwanza tukaokoe uhai wa watoto wetu achana na hizi abracadabra
sipo CUF na sipo obsessed na chadema,ila chadema siyo kama ya zamani
 
Hakika, nimeamini kuwa "Huwezi ukaupaka upepo rangi"

CCM nao, wanarudia kosa lilelile la CDM yaani, soon litaanza kuwatesa.
 
Subiri wale wenye mihemko waje watakutukana mpaka basi hapa ....ngoja Babati na Salary slip waje uone watakavyokunanga......

Hao watu wameshakua sikio La kufa
 
sipo CUF na sipo obsessed na chadema,ila chadema siyo kama ya zamani
So ipi ni best option? Nilikwambia sasa ni CUF nikimaanisha upepo wa kumuunga mkono Magu sasa umehamia CUF unashauri nini?

Halafu hilo neno kwamba haipo kama zamani si zuri kutolewa na mtu mwenye exposure tena ya Russia kama wewe!! Ukitaka kila kitu kiwe kama zamani itabidi nawewe urudi hatua ya kutambaa!!

Amka kijana majira yanabadilika na mambo pia hubadilika!!
 
Mkuu chadema inatakiwa ijipange upya,mikakati yake sasa hivi hamna nguvu
Unajua hoja Chadema wanazo ila shida ni kuweza kuzijustify hoja hizo ziendane na uhalisia ndio tatizo.....
 
Hakika, nimeamini kuwa "Huwezi ukaupaka upepo rangi"

CCM nao, wanarudia kosa lilelile la CDM yaani, soon litaanza kuwatesa.
mkuu kwa ccm hamna madhara kama chadema
 
Kama mtoto anakimbia kisa kaja mgeni kalia sahani yake huyo dogo alikua hasara ktk familia
 
CDM walishapoteza Net work. Kwa sasa hawana la kufanya.
Kwa hakika kabla ya 2020 tutashuhudia anguko kuu la chama hiki.
 
Back
Top Bottom