Maktaba Imepokea Kitabu Cha Rajabu Ibrahim Kirama

Maktaba Imepokea Kitabu Cha Rajabu Ibrahim Kirama

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,494
Reaction score
33,052
MAKTABA IMEPOKEA KITABU CHA RAJABU IBRAHIM KIRAMA

Rajabu Ibrahim Kirama ndiye aliyeuingiza Uislam Uchaggani kiasi cha zaidi ya miaka 150 iliyopita.

Katika maajabu ya Allah alipofariki watoto wake walihifadhi nyaraka zake zote ambazo zinafika umri wa miaka 100.

Nyaraka hizi zilihifadhiwa Machame Kijiji cha Nkuu alipozaliwa na kukulia Rajabu Ibrahim Kirama.

Mwanae mkubwa Salim Rajabu ndiye aliyezihifadhi nyaraka hizi za baba yake kwenye nyumba yake darini ndani ya gunia.

Nyaraka hizi zimenifikia mimi zikiwa katika hali nzuri kabisa na ndizo nilizotumia kuandika kitabu cha maisha ya Mzee Rajabu Ibrahim Kirama: "Rajabu Ibrahim Kirama Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislamu."

Mzee Rajabu ameishi zaidi ya miaka 100 na kufariki mwaka wa 1962.

Soma kitabu hiki ukutane na wanazuoni wakubwa waliokutana na Rajabu Ibrahim Kirama wakati wa kuusimamisha Uislam Uchaggani masheikh kama Sayyid Omar bin Sumeit, Sheikh Hassan bin Ameir.

Hawa wametoka Zanzibar kumfuata Rajabu Ibrahim Kirama, Machame.

Utasoma pia harakati za Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika, Machame na ushirikiano wao na Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika, Dar es Salaam chini ya Mwalimu Juma Mwindadi na Mwalimu Adam Issa.

Kitabu hiki kina mengi.
Si cha kukosa.

1750622892233.jpeg



View: https://youtu.be/UY1MpKd2cOk
 
Umefanya Kazi kubwa Sana.Sllah akujaalie umri mrefu
 
Utaratibu wa kukipata upoje?
Nyiluka,
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro bei Shs 10,000.00.

Kipo pia Mkuki na Nyota (Tanzania Publishing House) Samora Avenue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom