Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji kwamba kutokana na mlolongo wa matukio yanayotokea nyumbani ni wazi kwamba vyama vyetu vya upinzani vingetumia fursa hii kujiimarisha na kijipambanua kwa wananchi kama vyama mbadala mbavyo vinaweza kutufikisha huko tunakotaka kwenda.
Bahati mbaya kama Zitto alivyogusia hii dhana ya SWOT analysis, inaonekana vyama vyetu vya upinzani mzani wa internal Weakness(udhaifu) umezidi Opportunities(fursa) zilizopo nje ya vyama vyao, kwa mfano katika hali ya kawaida unategemea nini, mwenyekiti wa taifa wa chama cha upinzani anapoitisha mkutano wenye ajenda ya kuwafukuza wanachama!,au kiongozi anapotuhumiwa kwa kufuja pesa za chama!
Mfano mzuri ni NCCR mageuzi historia inaonyesha wazi kwamba umaarufu wake uliporomoka kwa kufukuzana uanachama, TLP, UDP na vingine vingi, vyama vya upinzani mtaji wake ni wanachama, sasa mnapoanza kufukuzana hata imani ya wananchi kwa vyama vya upinzani inapungua kabisa.Kwa hivyo katika hali ya kawaida ni vigumu kuchukua fursa zilizopo wakati ndani ya vyama bado kuna migogoro isiyoisha.
Lakini pia tusiwakatishe tamaa bado wananafasi ya kujifunza, historia ina mengi ya kutufunza,tujifunze best practice from Ghana, Kenya, Rwanda hata Botswana....
Long live Tanzania.