Makosa ya Rais Magufuli wakati mwingine unashindwa hata kumhurumia, the Man is So naive!

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Rais Magufuli, si mbaya kwa kila hali...mimi Binafsi alinisaidia kupata kazi, ya heshima tu, kabla ya tukio Lile la September 7, 2017 juu ya Uhai wa Lissu, NILICHUKIA.

Kwa hiyo Huyu Jamaa hufanya makosa ambayo mtu wa pembeni Unaona kabisa anaelekea kuiingiiza nchi kwenye migogoro ambayo itatuchukua muda mrefu mno kuitatua...kwa sababu mengi ya maamuzi yake kwa kweli kila mwenye utimamu wa akili anaona yanarisk si tu Amani na Utulivu wa nchi, bali hata Urais wake anaojidai nao sana, na wala adui yake si Chadema kama anavyoelekea kuamini yeye; Kuna siku ADUI yake watakutana barabarani

Hivi Imagine hadi WHO wanalazimika kumwandikia barua kuwa mwenendo wake katika kushirikiana na Viongozi wenzake kukabili janga hili hauwapendezi, hivi haoni hicho Kivuli kinachomnyemelea?

Kenya wanamlaumu, na Hakika na nchi majirani wengine akiwemo Kagame Wataanza kumlaumu punde, maana Sasa Tanzania ndo itakuwa nchi Kinara wa kusambaza Wadudu hawa kwa jirani zake...Corona Virus ni Ukungu mbaya ambao haujui mipaka ya nchi.

Siamini kama hiki Kiburi ni cha heri, pengine Mungu ana jambo kubwa sana anataka atufanyie Watanzania, lakini tutaipata Heri hiyo baada ya kupoteza raia wetu kwa Maelfu.

Kama Corona Virus wanaweza kuuangamiza mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu? Wacha tuone

IMG_20200403_183606.jpg
 
Siamini kama hiki Kiburi ni cha heri, pengine Mungu ana jambo kubwa sana anataka atufanyie Watanzania, lakini tutaipata Heri hiyo baada ya kupoteza raia wetu kwa Maelfu.
Hii ndiyo hoja ya kweli ndiyo maana ya umuhimu wa kutubu na kumshukuru Mungu ili mapenzi yake yatimie.
 
ivi Imagine hadi WHO wanalazimika kumwandikia barua kuwa mwenendo wake katika kushirikiana na Viongozi wenzake kukabili janga hili hauwapendezi, hivi haoni hicho Kivuli kinachomnyemelea?
Tafadhali tuwekee hapa, this is good and very important
 
Wewe binafsi na familia yako unachukua hatua gani ya kujinga kuambukizwa au kuambukiza majirani, ndugu zako, na marafiki wanaokutembelea, wafanyakazi wako/wenzako, nk?

Je, nchi ikiingia kwenye "lockdown" bidhaa mhimu (chakula na nishati ya kupikia km kuni/mkaa, mafuta ya taa, nk) watu watapataje?

Je, hata kama Serikali itaweka utaratibu wa kusambaza hayo mahitaji mhimu, huoni kuna uwezekano wa kusambaza virusi hivyo wakati wa kuandaa, kupakia, kusafirisha na matumizi yake?

Je, umezingatia uwezo wa kaya mojamoja wa kununua na kuhifadhi mahitaji mhimu?

Je, WaTz ambao kipato chao ni chs kila siku kudamka na kwenda kuhemea, ataishije wakati na baada ya "lockdown"?

Ubinafsi usisukume kufanya maamuzi yanayogusa maisha ya kila siku ya WaTz walio wengi.
 
Mkuu siyo yeye bali uwezo wake mdogo.kama unakumbuka mke wake tu alikataa kumpigia kampeni,waroho wa madaraka na wenye makaburi yao wakaamua kumsukumizia kwenye madaraka makubwa sasa acha tukipate cha moto
 
Kila nchi inatumia mbinu zake binafsi kukabiliana na corona kulingana na hali halisi ya mfumo wa maisha.

Kuna watu wachache kwenye mitandao ya kijamii wanalazimisha "total lockdown" ili nchi ivurugike.
Tukumbuke asilimia kubwa ya watanzania vipato vyao vinategemea kazi za kila siku.

Lockdown inaweza kusababisha vifo vingi hata mara 1000 ya vifo vya corona.

Tuchukue tahadhari, tunawe mikono kila wakati.
Mungu Ibariki Tanzania. TUTASHINDA.
 
Back
Top Bottom