Mimi pia naomba msaada kwenye vigeregere na vigelegele. Nadhani sahihi ni vigeregere lakini sina uhakika wa 100%. Pia kuna swala na suala, wenzetu wa zenj hutumia sana suala na sisi 'wazanzibara' hutumia swala. Je ni sawa kusema suali badala ya swali?
Nadhani neno sahihi katika kumaanisha majambo kuwa...
Mfano suala la lugha linakuwa gumu.
"Majambo" sio neno. Wingi wa jambo ni mambo.
"Suala" sio neno.
By the way, Mama, huwezi kusema "X ndilo jibu ingawa sina uhakika 100%." Sema "nadhani X ndilo jibu, sina uhakika."
"Majambo" sio neno. Wingi wa jambo ni mambo.
"Suala" sio neno.
By the way, Mama, huwezi kusema "X ndilo jibu ingawa sina uhakika 100%." Sema "nadhani X ndilo jibu, sina uhakika."
Kuhani sasa ina maana wazenj wanafanya makosa katika kiswahili kwa kutumia neno hilo? Maana Wazenj wengi wanadai neno sahihi ni 'suala' na siyo 'swala'. Hapo bado hatujagusa maneno yanayotumiwa na wenzetu marikiti, buku, skuli n.k.
Bubu yote tisa, kumi ni maana ya mrefeji na bomba.
Lakini hii ya watu kuchangaya herufi r na l au h na a ndio inayonitia mashaka zaidi.
Mama mimi kusema kweli sina matatizo hayo ya kuchanganya r na l au h na a kama ikitokea ni kughafilika tu, lakini hili la vigelegele huwa linanichanganya. Neno sahihi ni vigelegele ilibidi niingie kwenye kamusi kupata uhakika wa neno sahihi.
Sawa kabisa, na ukishapata hilo neno sahihi tafadhali tujulishe. Natanguliza shukrani.
Mama, neno sahihi ni vigelegele na siyo vigeregere.
Hivi kama mtu anaathiriwa na lugha yake ya asili kwenye ubongo au utamkaji mdomoni pekee....inanishangaza kidogo mtu anatamka masiwa badala ya maziwa lakini pia akiandika huandika masiwa!
Eti 'juice' yaitwaje kwa kiswahili fasaha?
Kitu kama sharubati hivi?
kwa mfano mimi kama mimi mwenyewe binafsi uwaga nafikili akuna hanayejua kua hanakosea adi aambiwe kua hanakosea au hajifunze kujuwa makosa.
haya maneno mara nyingi hukosewa sana kila siku,sasa sijui tuseme ni common mistakes au ni uzembe. Mimi nadhani kuna kauzembe fulani hivi kanako sababisha waandishi wengi kutohoa maneno wasiyo yajua.
Mama ametoa mifano ya baadhi ya maneno ambayo hukosewa mara kwa mara. Hapa ameua ndege wawili kwa jiwe moja. Yaani ametumia maneno hayo hayo yanayokosewa kwa kufikisha ujumbe wake. Au siyo Mama? Au mimi ndio sikuelewa?Sio uwaga ni huwa
sio nafikili ni nafikiri
sio akuna ni hakuna
sio hanayejua ni anayejua
sio kua ni kuwa
sio hanakosea ni anakosea
sio adi ni hadi
sio hajifunze ni ajifunze
Mama, eti ni: "zoea" au "zowea", kama lilivyotumika HAPA, naomba msaada tafadhali.
Je ni Mama pekee anayeweza na kustahili kujibu hilo swali lako?
Unaweza kujibu kwa niaba yake.