Castle_Lite
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 4,504
- 9,946
Hivi ni kweli huwa tunachagua exactly au hutokea tu kama Bahati nzuri unapata mwema au Bahati mbaya unapata kipengele!?Kosa la kuchagua mwenza, hili ni pigo la maisha.
Kosa la kuzembea shule.
Hivi ni kweli huwa tunachagua exactly au hutokea tu kama Bahati nzuri unapata mwema au Bahati mbaya unapata kipengele!?
Binafsi naona mwenza hutokea
kuchagua kupo sikuhizi? mbona ni kama wanawake hawakatai, anaweza kuwa na Jose, akija Yusuphu atasema yuko singoKosa la kuchagua mwenza, hili ni pigo la maisha.
Kosa la kuzembea shule.
Kukosea ni sehemu ya maisha na ndio ubinadamu wenyewe
Upo Sahihi bro.
Ila Tuombe Mungu sana atuepeushe na makosa ambayo unajua kabisa ni kosa ila unashupaza shingo.
Au unajua kabisa nikifanya hivi kinaweza kugeuka na kuwa kibaya ila ukakaza Roho na kufanya.
Binadamu ana akili sana lakini binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiriBinadamu wote sio wakamilifu, mara kwa mara tumefanya matendo na tumesema maneno ambayo kwa namna moja yameweza kuleta madhara katika maisha yetu na wenzetu.
Watu wengi wanasema Makosa katika Maisha hayaepukiki, ndio maana kila mtu ameshawah kufanya makosa.
Tuachane na hayo.
Maana Yaliopita sio ndwele , tugange Yajayo.
Tujisamehe, tujifunze na kusonga Mbele.
Lakini pia Tuepuke kufanya tena makosa ambayo tunajua kabisa kuwa ni makosa. Ukijua jambo si sahihi, usilifanye. Hiyo ni kanuni rahisi, lakini yenye uwezo mkubwa wa kuokoa muda, pesa, heshima, mahusiano na hata ndoto na Malengo yako ya Maisha.
Nasema na wewe ambae Leo unaenda kufanya jambo au maamuzi ambayo unajua kabisa sio sawa na kuna kitu ndan mwako kinakukataza, lakin kwasababu ya tamaa, ubishi, hulka za kibinadamu na hasira uliyonayo bado umedhamiria kufanya.
Mungu akakupe ujasiri wa kushinda hiyo vita na Kufanya maamuzi yaliyo Sahihi.
Nikutakie Mapumziko mema ya Weekend.
Kama ni jambo ambalo matokeo yake hayaleti madhara mabaya, ni sawaLakini inatulazimu tufanye baadhi ya mengine kwa ajili ya kijiweka katika position nzuri, Kwa mfano kosa la kudanganya (kusema uwongo wenye faida)
Pole Sana mkuuHuu uzi umeniumiza maana kuna jambo najua sio sahihi na ni kosa mbele ya Mungu na sheria lakini inabidi nifanye tu maana sina namna..
Mungu naomba unisamehe after this😔😔
Binadamu ana akili sana lakini binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri
Binadamu akipata changamoto iliyo sababishwa na yasiyotarajiwa, (uncertainty), huamsha ubongo na kukabiliana na changamoto anapo fanya hivyo anaweza akakutana na ubunifu
Changamoto nyingi tunazo zipata, (kabiliana nazo), husababishwa na binadamu
Binadamu anaweza kujisababishia changamoto kwasababu ya ujinga, uvivu, ulevi, uzembe, ushamba, uroho wa madaraka, upumbavu nitaje hizi tu kwasasa
Binadamu anaweza pia wasababishia wengine changamoto kwa bahati mbaya ama kwa makusudi
Hakika mkuu. Mi Kuna vitu vingine sivichukulii kama dhambi au makosa.Kama ni jambo ambalo matokeo yake hayaleti madhara mabaya, ni sawa
(Kusema uwongo ili kunusuru jambo)