Castle_Lite
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 3,299
- 6,379
Binadamu wote sio wakamilifu, mara kwa mara tumefanya matendo na tumesema maneno ambayo kwa namna moja yameweza kuleta madhara katika maisha yetu na wenzetu.
Watu wengi wanasema Makosa katika Maisha hayaepukiki, ndio maana kila mtu ameshawah kufanya makosa.
Tuachane na hayo.
Maana Yaliopita sio ndwele , tugange Yajayo.
Tujisamehe, tujifunze na kusonga Mbele.
Lakini pia Tuepuke kufanya tena makosa ambayo tunajua kabisa kuwa ni makosa. Ukijua jambo si sahihi, usilifanye. Hiyo ni kanuni rahisi, lakini yenye uwezo mkubwa wa kuokoa muda, pesa, heshima, mahusiano na hata ndoto na Malengo yako ya Maisha.
Nasema na wewe ambae Leo unaenda kufanya jambo au maamuzi ambayo unajua kabisa sio sawa na kuna kitu ndan mwako kinakukataza, lakin kwasababu ya tamaa, ubishi, hulka za kibinadamu na hasira uliyonayo bado umedhamiria kufanya.
Mungu akakupe ujasiri wa kushinda hiyo vita na Kufanya maamuzi yaliyo Sahihi.
Nikutakie Mapumziko mema ya Weekend.