apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Inasemekani ndiye pekee aliyekuwa na ujasiri wa kuwataja kwa majina huku akimueleza kila mmoja ni kwa nini anahitajika kukaa pembeni.Makongoro Nyerere kwa macho maangavu alikumbushia enzi za baba yake kwa kuwataja kwa majina watuhumiwa wa Ufisadi pasipo kumung'unya maneno ndani ya NEC.
Makongoro ametimiza wajibu wake na NEC kuonyesha kumuunga mkono na pengine wengine kwenda mbali kwa kusema ni LAZIMA wapishe.Macho ya Watanzania yako kwa CCM kuona utekelezaji wake.Alicho tufunulia Nape ni kuonyesha ni kwa jinsi gani mipango ya kuwatetea hawa mapacha watatu iko mbeleni haya ni dhahiri yameanza kujitokeza kwani ukitizama makala nzima ya Padri Privatus Karugendo imelenga kukichanganya Chama Cha Mapinduzi kwa maana hata wakiondoka hao mapacha watatu bado chama hakiwezi kurudisha imani zaidi ya kufa tu.
Huu ni wakati wa CCM kuthibitisha kuwa chama ni zaidi ya mtu,kama kweli hawa so called mafisadi wananguvu kubwa ndani ya chama basi CCM itambue kweli Mwisho wake umefika.Vile vile tutabaini NEC ni zao la nani kati ya waliomo na wanaotakiwa kutoka.
Hofu kwa Kikwete na uswahiba wa hawa mafisadi sioni kama inatija kwani katika siasa mara nyingi wanaofarakiana na kutengana ni wale waliokuwa marafiki (Mseven/Besigye),(Nyrere/Kambona) n.k.Mengi yameanza kuzungumzwa ooooh Lowasa ana nguvu,hivi tangu lini mwizi akawa na nguvu mikononi mwa Askari.Wote wanaomtetea Lowasa etal wanadhihirisha unafiki wao na wasiotakia taifa hili mema.Ifikie mahala LOWASA,AZIZ na CHENGE waseme CCM sio mama yangu wala baba yangu.Wanang'ang'ania humo kuna nini?
Sote tumuunge mkono Makongoro Nyerere aliyediriki kuwataja na kila mmoja kumuelezea kwa nini anapaswa kukaa kando.Tutambue kuwa shutuma za Wananchi katika Chama zinatosha kumuondoa Mwanachama (huku hakuna sheria ya ushahidi).CCM isiogope kufa kwa sababu ya hawa mafisadi na kama uhai wa chama unategemea hawa mafisadi basi itakuwa imekufa kishujaa.