Makongoro Nyerere dhidi ya Mapacha watatu (RACHEL) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makongoro Nyerere dhidi ya Mapacha watatu (RACHEL)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Apr 28, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Inasemekani ndiye pekee aliyekuwa na ujasiri wa kuwataja kwa majina huku akimueleza kila mmoja ni kwa nini anahitajika kukaa pembeni.Makongoro Nyerere kwa macho maangavu alikumbushia enzi za baba yake kwa kuwataja kwa majina watuhumiwa wa Ufisadi pasipo kumung'unya maneno ndani ya NEC.

  Makongoro ametimiza wajibu wake na NEC kuonyesha kumuunga mkono na pengine wengine kwenda mbali kwa kusema ni LAZIMA wapishe.Macho ya Watanzania yako kwa CCM kuona utekelezaji wake.Alicho tufunulia Nape ni kuonyesha ni kwa jinsi gani mipango ya kuwatetea hawa mapacha watatu iko mbeleni haya ni dhahiri yameanza kujitokeza kwani ukitizama makala nzima ya Padri Privatus Karugendo imelenga kukichanganya Chama Cha Mapinduzi kwa maana hata wakiondoka hao mapacha watatu bado chama hakiwezi kurudisha imani zaidi ya kufa tu.

  Huu ni wakati wa CCM kuthibitisha kuwa chama ni zaidi ya mtu,kama kweli hawa so called mafisadi wananguvu kubwa ndani ya chama basi CCM itambue kweli Mwisho wake umefika.Vile vile tutabaini NEC ni zao la nani kati ya waliomo na wanaotakiwa kutoka.

  Hofu kwa Kikwete na uswahiba wa hawa mafisadi sioni kama inatija kwani katika siasa mara nyingi wanaofarakiana na kutengana ni wale waliokuwa marafiki (Mseven/Besigye),(Nyrere/Kambona) n.k.Mengi yameanza kuzungumzwa ooooh Lowasa ana nguvu,hivi tangu lini mwizi akawa na nguvu mikononi mwa Askari.Wote wanaomtetea Lowasa etal wanadhihirisha unafiki wao na wasiotakia taifa hili mema.Ifikie mahala LOWASA,AZIZ na CHENGE waseme CCM sio mama yangu wala baba yangu.Wanang'ang'ania humo kuna nini?

  Sote tumuunge mkono Makongoro Nyerere aliyediriki kuwataja na kila mmoja kumuelezea kwa nini anapaswa kukaa kando.Tutambue kuwa shutuma za Wananchi katika Chama zinatosha kumuondoa Mwanachama (huku hakuna sheria ya ushahidi).CCM isiogope kufa kwa sababu ya hawa mafisadi na kama uhai wa chama unategemea hawa mafisadi basi itakuwa imekufa kishujaa.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hana lolote naye mlevi tu huyu...
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yupi sasa ndio mlevi, karugendo, makongo au apolycaripto??:banplease:
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  Unafikiri kufa mchezo? Yesu mwenyewe mwishomwisho nusu akate tamaa mpaka kinjiwa kikaja kumpa moyo. CCM kuinuka labda ibomoke yote nzimanzima then izaliwe upya na jina la ubatizo jipya
   
 5. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ulevi wake hauhisiani na kusimamia hoja na ushajaa wa kutaja majina ya watuhumiwa ili hali wengi walishindwa akiwemo m/kiti wao wa taifa, Bravooooo makongoro, bravoo cha pombe
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwenye red... tumuungeje mkono Makongoro Nyerere?
   
 7. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Mimi akina Mzee Mwinyi wamekuwa butu namna hiyo wanatishwa na akina RACHEL,aheri ya Mzee Pius aliwataja hadharani,ingekuwa Nyerere hao akina RACHEL wala wasingepewa eti siku 90 za nini?hizo siku 90 mnataka wafanye nini?mimi nashindwa kuelewa,Nyerere alimtimua Maalim Aboud Jumbe pale aliponusu tu ukumbini akitoka nchi za nje hakupewa siku 90 na akasahauliwa katika siasa za Tanzania,akina Maalimu Seifu vivyo hivyo,haiwezekani nchi iwekwe rehani na watu watatu kwa ajili ya eti sijui fedha zao,mara mtandao wao una nguvu,mara wameonewa ,jamani kweli nani mjinga nchi hii asiyejuu kuwa akina RACHEL ni wachafu full stop,hakuna jingine,kuyumba kwa CCM kama chama tawala ni kuyumba kwa nchi,hawa akina RACHEL ni nani zaidi hapa Tanzania/mbona tunawapa viburi na sifa za bure,nawaambieni CCM ikidhamiria kuwatosa hao watu watakuwa historia na huo utajiri wao wa wizi utaisha haraka kama walivyoupata haraka,acheni kuwaogopa watu ,ni Mungu tu ndie wakuogopa wote tunapita tu hapa duniani bali Tanzania itakuwepo milele si wote tumeikuta na tutaiacha ,tunakuwa kama tuko visiwa vya Sisily Italy ambako genge la Mafia ndio lilishika huo mji,tusikubali Watanzania watu watatu eti maarufu ndio waiweke rehani nchi,namtakia kila la kheri Raisi wetu Kikwete katika kujivua gamba,dola umeishika wewe hakuna mtu wa kuku blackmail ,Aluta Continua
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sote tunajua CCM ni chama kilichijaa kujuana, favour ism, kuachiana kamba kwa kila kitu!! Ungomvi mkubwa walionao huko ndani unatokana na nani ana haki ya kuachiwa nini na wakati gani!! Haya maungomvi tuliyaona mwaka 2000, hatimaye boyz 2 men wakaibuka kidedea. Undumilakuwili na ulafiwa JK ndo umewafikisha hapa!! A stage which "may avail a new image of CCM" tunataka tuone CCM na CCM B/CCJ or what so wherever...

  Hii ni movie, mimi najvutia pop corn nacheki tu...
   
 9. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makongoro amekosa kurithi busara za marehemu baba wa taifa.
   
 10. M

  Marytina JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ukisoma btn the lines MAKALA ZA raia mwema last wiki utagundua ya kuwa MAKONGORO alimkandia hata JK
   
 11. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mimi sitaki kuamini kuwa eti katika ccm mafisadi ni watatu tu, Tatizo la kwanza nimfumo mzima uko corrupt. Then Mwenyekiti alichea kikao cha baraza la mawaziri lilibariki project ya richmond ambayo rais alielewa vizuri sana huo mshiko jinsi ulivyochotwa. Fedha za epa zimemuweka rai madarakani 2005 sasa nashangaa watu wanang'ang'ana na Lowasa tuuuuuu. tuwe wakweli kama watu waliolamba mshiko wa ufisadi wanaenda na maji basi ccm ijiandane kuwa na viongozi wapya katika ngazi karibu zooote
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Brother ni bora uwe na utamaduni wa kujadili hoja badala ya kujadili maisha binafsi ya mtu. Suala hapa ni hoja alizotoa Makongoro kwenye mkutano ule na kama hoja hizo zina msingi. Sasa wewe unapojadili ulevi wake kwani nani halewi? Kama ni hivyo basi utapuuza wengi na inawezekana na wewe ni mlevi tena mlevi wa pombe za kupuliza lakini hiyo sisi hatuwezi kuiingilia maana haituhusu.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Yeye hapana msimuunge mkono.......ila hoja yake sawa
   
 14. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Sekyuuu! Umenikuna Mkuu!
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nimekumbana na hii kwenye pita pita za kichungaji

  [​IMG]

  Mchezo wa kujivua gamba ndani ya CCM umefikia mahali patamu. Ninapoufikiria, ninapata tu maswali. Makosa majibu, kwani mambo mengi ambayo baadhi ya watu walioko wa upande wa mapacha hao wanadai ndiyo majibu, si majibu wala si hoja. Ni kauli tu za kujitetea. Mwalimu wangu wa Logic alinieleza kuwa ni Fallacies.

  Mfano,
  Mosi, wapo wanaosema: "Si wao tu, wapo wengi hawa wametolewa kafara. Maneno haya hayaelezi kama wao hawasiki, kama yangeleeza hivyo ningesema kuna hoja.

  Pili, wapo wanaosema hata Mukulu wao ni miongoni mwao, hii yaweza kuwa sahihi, lakini haileti majibu kwamba, kama Mukulu naye yumo hastahili kuchukua hatua dhidi yao.

  Tatu, wapo wanaosema kinachofanyika ni vita ya urais 2015, na hii masikioni ni sahihi, lakini haisema kama kilichofanyika dhidi yao ilikuwa stahili yao au wanaonewa.

  Nne, wapo wanaosema mmoja wao atageuka kuwa 'kama' Jacob Zuma wa Afrika Kusini, lakini hawana majibu kama 'madhambi' ya Zuma na mazingira yake yanafanana na madhambi ya huyo pacha, wala kama madhambi ya Zuma yalikuwa na impact ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi wa Afrika Kusini, kama ilivyo madhambi haya.

  Tano, wapo wanaosema wanachafuliwa kwa sababu mbalimbali, lakini hasemi kama bila kuchafuliwa mapacha hawa ni wasafi. Yapo na maswali mengine mengi, ukitaka ongezea.

  Kwa hisani ya http://www.rsmiruko.blogspot.com
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kikwete angemsikiliza Makongoro kwenye mkutano waliofanya Butiama labda sasa hivi suala la kujivua gamba lingekuwa na sura tofauti.
  Mako alishauri wote waliotajwa kwenye kashfa za ufisadi, wakiwepo Chenge, Rostum na Lowassa wajiuzulu au wafukuzwe kwenye chama. Hii ilikuwa 2009, kama nakumbuka vizuri. Alimwambia Lowassa kuwa "hutufai." Lakini Kikwete akawatetea wakati huo na haya ndiyo matokeo yake.
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - National Politics at best, mkuu aliyemuondoa Lowassa U-Waziri mkuu ni nani? Ndiye huyo huyo anayewafukuza chama sasa hivi mjifunze how big politics are played, it is who is behind Makongoro? na sio who is Makongoro anyways katika CCM!

  - Mkulu huenda ana mapungufu katika uongozi, lakini sio games I think he is the best ever! ndio maana hupendelea sana makundi katika uongozi wake angalia kila alikopita utakuta makundi ni raahisi sana kutawala kwa lines za makundi bila watawaliwa kujijua!

  - Divide and rule kwa maneno mengine!

  FMEs!
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Jasusi Butiama mkulu alikuwa occupied sana na muafaka wa Zanzibar, lakini there is one thing he did kule bila makelele wala watu wengi ku-notice, alimuondoa Rostam kwenye uweka hazina wa CCM bila kumfahamisha mapema, tayari alishaweka msingi kuanzia pale, inasadikwia since then jamaa hajawahi kuwa na access naye tena!, it is just politics, alikuwa anasubiri the right time awatose na sasa sio siri anawatosa, sasa hivi utasikia Rostam amekimbia nchi! Watch!

  - Nildokezewa hii na mkuu mmoja aliyekua amekaa next to Rostam, anasema jamaa alihaha haijawahi kutokea, kwa kutoamini, muungwana is very good at political games, hakuna mtu yoyote wa kuwatoa wale mapacha isipokuwa ni yeye tu, sasa tizama alivyoifanya ionekane ni Makongoro!, kama alivyoifanya kule ionekane ni Mwakyembe, sasa uliza aliyemrudisha ubunge Mwakyembe ni nani? Ndio utaelewa hizi siasa za taifa sio mchezo!

  - Kosa kubwa walilokosea mafisadi na they are paying for na kuelekea mwisho wao, ni pale waalipomtoa six kwenye U-Spika kwa kuwatumia Wa-Zanzibari, ndipo walipoanza kujipigilia misumari ya mwishoni kwenye jeneza lao, I mean understand hizi National politiics lini umewahi kuwasikia Wapinzani wakiwalalamikia hawa mapacha? au Mkapa? WHY?


  FMEs!
   
 19. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu nambie kwann wapinzam hawapig kelele kuhusu mkapa na mapacha wa tatu? Pili kwenye listi of shame ya Dk Slaa hawapo?
   
 20. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #20
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Mkuu vipi si na wewe ufanye utafiiti japo kidogo!

  William @ NYc, USA.
   
Loading...