Makongoro Nyerere ametumwa na nani?

Makongoro Nyerere ametumwa na nani?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
Hakuna kipindi ambacho CCM imeingia katika Uchaguzi Mkuu ikiwa na makundi hatarishi na pia matatizo ya kiutawala kama uchaguzi Mkuu ujao.

Ujio wa Abdulrahman Kinana kama Katibu Mkuu kwa kiasi kikubwa umekichelewesha chama kumeguka vipande vipande kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Wataalam wa kisiasa wanaendelea kujiuliza maswali mengi kuhusu hatima ya makundi na uhasama unaorutubika kila siku ndani ya CCM.

Udhaifu wa viongozi wakuu wa chama umesababisha baadhi ya wanachama kufanya watakacho kwa kukiuka kanuni, maadili na taratibu za chama mpaka kufikia hatua ya kutaka kumuondolea Rais Kikwete kofia ya Mwenyekiti wa CCM-Taifa.

Kuibuka kwa Makongoro Nyerere katika kundi la wanachama ambao wanaomba kuteuliwa kuwa wagombea Urais wa Tanzania kumeufanya uwanja wa siasa ndani ya CCM kubadilika hasa ikichukuliwa kuwa, hakuna mwanaCCM ambaye alikuwa akiongea na kusikilizwa kwa makini na wanachama wa CCM kuhusu kile kilichokua kinaendelea ndani ya CCM.

Makongoro amewashambulia vikali baadhi ya watia nia kama Edward Lowassa, Mwigulu Nchemba na Stephen Wasira kama ndiyo baadhi ya wale wanaleta maradhi ndani ya CCM pamoja na kwamba CCM bado ni chama bora nchini.

Pamoja na mambo mengine, Makongoro aliwatuhumu kwa kuja na Ilani yao ya uchaguzi badala ya kusubiri Ilani ya CCM itakayopitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM-Taifa.

Alisema ndani ya chama hicho kumekuibuka pia genge la watu wachache ambao utajiri wao ni wa shaka na umejijenga kwa fedha chafu.

"Ndani ya chama tawala wamekuwapo ‘vibaka' wachache… unajua kibaka ni kibaka tu hata kama kapewa gari la Serikali lina bendera ya taifa mbele atabaki kuwa kibaka tu. Hawa ndiyo wanaotuvurugia chama na hawamheshimu Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete'', Makongoro alisema.

Makongoro ameamua kuchukua jukumu la viongozi wakuu wa CCM ili kupambana na makundi yanayohatarisha uwepo wa CCM katika uwanja wa siasa.

Sauti ya Makongoro ukiichunguza kwa makini ni kama sauti ya mtu aliaye nyikani!

Kwa sauti hii, ni nani amemtuma Makongoro ili kupambana na wanachama anaowaita ni vibaka wanaosababisha baadhi ya viongozi wa CCM kuishi maisha ya kusukumwa kwa upepo wa makundi yanayomilikiwa na watoa fedha.

Je, inawezekana sauti ya Makongoro ni sauti ya viongozi wakuu wa CCM?


Makongoro atauweza mfupa uliowashinda viongozi wakuu wa CCM?.
 
Huyu Makongoro wala haonekani kama yuko serious.
Ngosha;

Muonekano wake hauonyeshi seriousness kwenye kazi anayoiomba.

Kutokuwa serious ndiyo kumenipa shauku ya kufahamu aliyeko nyuma yake.
 
Naona anaweza kushinda na ameshashinda. Siku zote majizi na mafedhuri km lowasa na genge lake ni lazima yashindwe
Mkuu;

Kitu gani kinakufanya udhani ameshinda kabla hata ya mchakato kumalizika?
 
Kinana ni kiboko ametumia mbinu kali sana ya kuwajaza wagombea Urais kutokea kwenye chama chake ili kuwachanganya wengi na kufikiri kuwa CCM kuna mparaganyiko.

Yeye huyooooo yuko mikoani anasafisha njia na kufunika mashimo. Nyinyi hangaikeni na hawa wagombea.

Hapo sasa!
 
Kutibu jipu unaanza kulipasua na kulisafisha.
Muafaka ni CCM kugawanyika makundi mawili (CCM Asili na CCM Maslahi/Mafisadi), kundi linalotetea wananchi litapeta wakati huo huo la pili likitoswa!
 
Hajatumwa ila ni shinikizo la la wazee wa ccm ambao wao jina nyerere ndio kila kitu.
Hivo kupambana na ukawa bora watumie jina nyerere . Wanafikiri kuwa watu watadhani amerudi..kwao ni kurudi ikulu bila kujali kama anaweza au hawezi
Bila kujali kuwa hana sifa yoyote ya urais.
Kwanza nilupo muona kachuchuma mbele ya padre mzungu sina imani kabisa..tutarudi kule kule serikali kukabidhiwa vatikano
 
Mkuu,asante kwa hoja shirikishi.
Kwa maoni yangu Makongoro hajatumwa, katika hali mbaya ambayo CCM inapitia ni rahisi tu kwa mwanachama yoyote kuamua kuingia kwenye kinyang'anyiro.
Makongoro anabebwa na jina la Nyerere na si vinginevyo, anaweza asipewe ridhaa ya chama kugombea kwenye uchaguzi mkuu ila uwepo wake na hoja zake zinaonekana wazi kuwa na mlengo wa kuzungumza kile ambacho wengine wameshindwa.

Uwepo wake ni hasara kwa baadhi ya wagombea ambao "wamebebeshwa" tuhuma za ufisadi na faida kwa wale ambao wanajitanabaisha kama watu "wasafi".
Anaposimama kuzungumza kama kiranja wa CCM inawezekana ni kwa sababu kubwa mbili.
Mosi, mwenyekiti wa chama amepoteza uwezo wa kukemea na kusimamia maadili ya Chama
Mbili, huu ni wakati wa liwalo na liwe. ..the end justify the means. .
CCM wakipita salama wataponya majeraha, wakisambaratika wapo watakaolaumiwa. ..
 
Hajatumwa ni haki yake ya kikatiba kuomba kugombea uongozi.
Pili hata mtu wa kawaida anaona madudu yaliyopo ccm na taifa kwa ujumla, ameamua kupambana na hayo madudu maana WATANZANIA WENGI mmezoea kukaa kimya na kunung'unika tu bila kusema chochote.Basi Makongoro Charles Nyerere ameamua kupambana bila woga.
 
Makongoro ni sehemu kubwa ya mkakati wa viongozi wakuu wa CCM kumchomoa Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha urais. Lowassa won't make it; mark my words.
 
Na wewe ni nani kakutuma? je,unweza ukakubali kutumwa? mbona haujauliza wengine nani kawatuma?.Sisi wanyonge tunamtaka yeye na yeye anatutaka sisi.Mungu kamtuma.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kinana ni kiboko ametumia mbinu kali sana ya kuwajaza wagombea Urais kutokea kwenye chama chake ili kuwachanganya wengi na kufikiri kuwa CCM kuna mparaganyiko.

Yeye huyooooo yuko mikoani anasafisha njia na kufunika mashimo. Nyinyi hangaikeni na hawa wagombea.

Hapo sasa!
Mkuu;

Ni kweli CCM haijafika kwenye mparanganyiko lakini kuna makundi hatarishi ambayo yanakisukuma chama kuparanganyika.
 
Kutibu jipu unaanza kulipasua na kulisafisha.
Muafaka ni CCM kugawanyika makundi mawili (CCM Asili na CCM Maslahi/Mafisadi), kundi linalotetea wananchi litapeta wakati huo huo la pili likitoswa!
Mkuu;

Kwa hiyo Makongoro ameanza kulipasua jipu?

Kama ni hivyo, nani atalisafisha?
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Cku zote aliyezama ajui niwakat na mda gan mwokoaji anakja kumwokoa ndo ilivyo kwa hyu jmaa weng wetu atujajua kama ndo anataka kulinsuru taifa letu makongoro mkombozi wa wanyonge sbr utaona
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Back
Top Bottom