Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 16,958
- 7,512
"Kwa upande wake, Nyerere alisema akifanikiwa katika kinyanganyiro hicho, ataanza kushughulika na kukiimarisha chama ili kiweze kurudi katika misingi yake"
SWALI:
Makongoro anataka kugombea uraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi?
Nauliza hivyo kwakuwa toka awali ajenda yake kubwa ni kuleta nidhamu ndani ya chama na kukirudisha kwa wananchi. Sijawahi kumsikia akisema atafanya nini kwa watanzania akiwa Rais, ila namsikia na kumkariri atafanya nini akiwa mwenyekiti wa chama.
Tatizo la watanzania sio chama, ni mmonyoko wa maadili, rushwa, ufisadi, uwajibikaji, na uwazi ndani ya serikali. Mengine ni huduma mbovu za kijamii (elimu, afya, maji, n.k). Sasa ajaribu kujikita kuelezea atashughulikia vipi matatizo kama hayo yanayowakabili watanzania.
NB: Ikumbukwe kuwa sio lazima Rais anayetokana na CCM awe mwenyekiti pia wa CCM, ni utamaduni tu uliojengeka ndani ya Chama.
CC: Zakumi
Mkuu kama umesikia basi ulitakiwa kuona ambavyo kwa pamoja vingekurahisishia kufikia hitimisho sahihi kwa kutumia zile njia tano (senses) za ufahamu, bahati mbaya wewe ulisikia tu. Facts;
1. C.M.N Hakusoma ilani yake zaidi ya kutangaza nia yake.
2.Hakuwa anaomba watanzania wamchague bali alikuwa anakiomba chama chake kimpitishe. Alikuwa anaongea na chama chake.
3.Mpaka sahivi hajasema ilani itakuwaje kwani ilani atakayoisimamia haitengenezwi na yeye bali ilani inatengenezwa na chama na inabaki kuwa ni mali ya chama.
4.Chochote alichokisema yeye alikuwa anaongea na chama chake kupitia wanachama wake. Sisi kusema hatujasikia atafanyaje hiki ama mbona hatujamsikia kuhusu kile ni kutokuelewa Maelezo yake aliyosema kwamba ahadi si za mtu, chama kupitia ilani yake ndo kinahaidi na atakayepitishwa ndo atatakiwa kuifata ilani ya chama na si ile yake, na akauliza hivi, itakuwaje nitangaze yangu hapa alafu kwenye ilani ya chama iwe tofauti itakuwaje?.
Sasa kama alikuwa anaongea na chama chake sisi kumbe inatuhusu nini? yeye kama kaona chama chake hayo ndo matatizo ya msingi katika chama chao sie inatuhusuje
? .Tusubiri siku chama kikimpitisha hapo sasa ndo atakuja kwetu watanzania akiletwa na chama ili asimame atwambie sasa, ni nini anataka kuifanyia nchi yetu, huo ndo utaratibu na si kurukaruka tu ilmradi umepewa maiki uongee