Makonda: Wengi sana walinishauri nisihudhurie kwenye msiba, ila nimetimiza wajibu

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mkuu wa mkoa wa Dar amesema watanzania wengi wana kasumba ya kuvisha taswira jambo fulani,amesema kuna watu wengi sana walikuwa wanamuambia asihudhurie kwenye msiba na waandishi wa habari wakatengeneza mazingira wanayoyajua wao ili kuleta uadui kati yake na wafiwa, lakini ametimiza wajibu wake, ameasa watu wasipende kuwa na maneno mengi na kusingizia watu mambo, msikilize zaidi hapa.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar amesema watanzania wengi wana kasumba ya kuvisha taswira jambo fulani,
amesema kuna watu wengi sana walikuwa wanamuambia asihudhurie kwenye msiba na waandishi wa habari wakatengeneza mazingira wanayoyajua wao ili kuleta uadui kati yake na wafiwa, lakini ametimiza wajibu wake, ameasa watu wasipende kuwa na maneno mengi na kusingizia watu mambo, msikilize zaidi hapa

Makonda katika hali ya ubinadamu unategemea kweli wakupende ndugu zake na Kabwe? Common sense dictates that anyway! Umekwenda sawa lakini sidhani kama walifurahia ujio wako. Mwanadamu yuko hivyo, hata hakimu akitoa hukumu against mtu, yule mtu hawezi kumpenda hakimu pamoja na kuwa anatimiza wajibu wake, ila hawezi kumdhuru hakimu kama kamhukumu katika haki!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar amesema watanzania wengi wana kasumba ya kuvisha taswira jambo fulani,amesema kuna watu wengi sana walikuwa wanamuambia asihudhurie kwenye msiba na waandishi wa habari wakatengeneza mazingira wanayoyajua wao ili kuleta uadui kati yake na wafiwa, lakini ametimiza wajibu wake, ameasa watu wasipende kuwa na maneno mengi na kusingizia watu mambo, msikilize zaidi hapa.

makonda anapenda sana sifa, asingeacha kwenda kutafuta SIFA.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar amesema watanzania wengi wana kasumba ya kuvisha taswira jambo fulani,amesema kuna watu wengi sana walikuwa wanamuambia asihudhurie kwenye msiba na waandishi wa habari wakatengeneza mazingira wanayoyajua wao ili kuleta uadui kati yake na wafiwa, lakini ametimiza wajibu wake, ameasa watu wasipende kuwa na maneno mengi na kusingizia watu mambo, msikilize zaidi hapa.

AMESEMA TUSIWE NA MANENO MENGI MBONA YEYE KAONGEA SANA
 
Watu wanashindwa kutofautisha majukumu na ubinadamu, wanadhani ukuu wa mkoa ni umakonda, hawajui kuwa muda wowote hiyo nafasi inaweza kuchukuliwa na mtu asie na jina la makonda na Makonda akawa na nafuu. Yalikuwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kazi na sio uadui au hisia binafsi za Makonda dhidi ya marehemu.
 
Watanzania lipi jema kwetu?mtu akiwa mwizi tunapiga kelele...lakini akitajwa hadharani akafukuzwa lawama pia..mwizi ni mwizi tu..awe marehemu au mzima.kufa hakukuondolei dhambi zako ila kinakusogeza kwenye kiti cha hukumu.maana hakuna tena muda wa kutubu..tatizo letu tunaangalia nani kafunga goli ndio tushangilie ushindi..
 
Mheshimiwa Makonda,kuna mambo matatu yanaleta FITINA kubwa kwenye jamii pindi yanapojiri.Nayo ni MARADHI,KIFO na SHEREHE.Mambo haya huleta fitina na sintofahamu kubwa kijamii,hasa jamii ambayo IKO MBALI NA MWENYEZI MUNGU.Kwa hiyo nikupe pole kwa yaliyokukuta lakini si wewe si wa kwanza kukuta.
 
Kutumbuliwa sawa, lakini ubinadamu ndugu zake hawawezi kukupenda. Mimi nisingelikwenda, ningelituma mwakilishi tu
Ndio maana kuna wengine wanapata uongozi na wengine hawapati kwani sifa moja ya Uongozi ni Ujasiri. Unadhani asingeenda ndio ingetafsiriwaje. Kuwa alimuonea? Inawezekana njia aliyotumia haikuwa sahihi lakini je marehemu ( RIP) tuhuma hizo si za kweli? basi nadhani tumuombee tu lakini tukumbuke Mh. Makondo yuko kwenye wadhifa mgumu sana unaotaka ujasiri!
 
Ukiona unatumia muda mwingi sana kwenye media kutafuta balance, maana rahis ni kwamba HUKUBALIKI inabidi hata aliyekuchagua ajiulize, what went wrong? utumishi wa umma ni utumishi wa watu, huwez kufanya kazi na watu wasiokukubali.
Bora upangiwe kazi za kitaalamu kutegemea proffession yako, ikiwa ushawish kwa watu umepungua.
Ni mtazamo tu, usikasirike sana mzee haya mawazo tu!
 
Ndio maana kuna wengine wanapata uongozi na wengine hawapati kwani sifa moja ya Uongozi ni Ujasiri. Unadhani asingeenda ndio ingetafsiriwaje. Kuwa alimuonea? Inawezekana njia aliyotumia haikuwa sahihi lakini je marehemu ( RIP) tuhuma hizo si za kweli? basi nadhani tumuombee tu lakini tukumbuke Mh. Makondo yuko kwenye wadhifa mgumu sana unaotaka ujasiri!
Ujasiri wa kujitoa ufahamu? Tuma mwakilishi, unakuwa kituko kwenye kadamnasi. Jaji akimhukumu mkosaji kufa akanyongwa, pamoja na kuwa umetenda haki kama jaji, katika ubinadamu, ndugu wa mnyongwa hawawezi kukupenda. Usiende kwenye msiba na ndio maana Majaji wanapewa ulinzi kwa sababu pamoja na kutimiza wajibu kwa haki uliyemhukumu kunyongwa hawatakupenda (pamoja na kuwa labda hawezi kukudhuru) ubinadamu uko hivyo!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar amesema watanzania wengi wana kasumba ya kuvisha taswira jambo fulani,amesema kuna watu wengi sana walikuwa wanamuambia asihudhurie kwenye msiba na waandishi wa habari wakatengeneza mazingira wanayoyajua wao ili kuleta uadui kati yake na wafiwa, lakini ametimiza wajibu wake, ameasa watu wasipende kuwa na maneno mengi na kusingizia watu mambo, msikilize zaidi hapa.

Tokea nione ile video ya Makonda kule bandarini anatafuta mabehewa ya sukari. Sijawahi kuona lofa kama huyu mtu hata shule sijui kasoma wapi kwa sababu hata train of thought hana.
 
Back
Top Bottom