Makonda: Wanawake ni moja ya chanzo cha ufisadi

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

1.JPG


Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

Makonda amewaambia wanawake hao kuwa hata katika suala la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya akina mama kwa watoto tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kupunguza changamoto zinazozikabili miji mbalimbali kwa kipindi hiki ambacho kuna changamoto ya usafi.
 
Hapo mkuu wa mkoa ameteleza kidogo ila tumsamehe, nadhani ana nia njema ila jinsi ya kufikisha ujumbe ndiyo ameyumba kidogo, nawaomba ukawa wenzangu tuweke Silaha chini tumpe muda mkuu wa mkoa apate uzoefu wa kutosha
Namuomba Rais a revisit sababu zake za kumteua huyu mkuu wa mkoa. Umefika wakati wakumpangia kazi nyingine.

Wanawake wenzangu mko wapi? Mbona kuna pattern kutokuthaminiwa awamu hii?
 
Namuomba Rais a revisit sababu zake za kumteua huyu mkuu wa mkoa. Umefika wakati wakumpangia kazi nyingine.

Wanawake wenzangu mko wapi? Mbona kuna pattern kutokuthaminiwa awamu hii?
Wanaogopa kutumbuliwa.
 
Nilivyojiambia kuwa 'time will tell' nilidhani angalau watatumia japo miaka miwili kudhihirisha uhalisia wao lakini naona ni chini ya miezi sita upeo wao unadhihirika sasa!
Kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Vipi kuhusu hao wanaotoa zawadi?sitaki kurudi kwenye kisa cha kuku na yai nani wa kwanza ila napenda maswali ya msingi kwa Taifa letu yasipewa majibu myepesi kama hayo ya kusema "wanawake ni chanzo cha ufisadi".......alifanyia uchunguzi wake wapi?kuna ukweli wanaopewa zawadui sana na kupokea zawadi hizo za kifisadi ni wanawake tu au anataka kutujengea hasty generalization?....sikubaliani na jibu jepesi na lenye pendeleo bi nafsi(bias and stereotype).....
 
Makonda anaelewa kuwa kuna wanaume wanaopokea zawadi zinatokana na pesa za ufisadi?
 
God created mankind in his own image,
in the image of God he created them;
male and female he created them. Asisahau hili. Unaposukuma tatizo kwa mwingine ni mhimu kuutambua mchango wako.
 
Ni sahihi kabisa... Mwanamke wa kizungu akimpelekea manoti ya pesa ambayo ana hofu nayo na upatikanaji wake huwa analeta noma. Ila mianawake ya kwetu hata leo ulale na jero kesho urudi na Billion wala hatauliza ulikozitoa zaidi ya kuanza kutumbua ili awakomeshe mashosti zake
 
Kuna ukweli kiasi katika kauli yake.

Ukweli upo mkubwa tu... Mwanamke wa kizungu ukianza kuleta mipesa nyumbani ambayo hajui imepatikanaje lazima akufokee na hii ni kwasababu kule kwao sheria ni ngumu kwenye mambo ya money laundering na kukwepa tax.. Ila huku kwetu mwanamke haulizi umepataje yeye anawaza kutumbua tu
 
Back
Top Bottom