Makonda: Wanawake ni moja ya chanzo cha ufisadi

Makonda: Wanawake ni moja ya chanzo cha ufisadi

Hahahaa naona hata mbwembwe za wadada pale mlimani city wikiend zimepungua sana tangia JPM atue magogoni!!
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

1.JPG

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

Makonda amewaambia wanawake hao kuwa hata katika suala la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya akina mama kwa watoto tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kupunguza changamoto zinazozikabili miji mbalimbali kwa kipindi hiki ambacho kuna changamoto ya usafi.

Tena yamekuwa hayo. Kwa stahii hii nimeanza kumkubali Makonda
 
Huyu katoka chama kile na anauzoefu na serikali iliyopita huenda anamaana yake!
 
Vipi kuhusu hao wanaotoa zawadi?sitaki kurudi kwenye kisa cha kuku na yai nani wa kwanza ila napenda maswali ya msingi kwa Taifa letu yasipewa majibu myepesi kama hayo ya kusema "wanawake ni chanzo cha ufisadi".......alifanyia uchunguzi wake wapi?kuna ukweli wanaopewa zawadui sana na kupokea zawadi hizo za kifisadi ni wanawake tu au anataka kutujengea hasty generalization?....sikubaliani na jibu jepesi na lenye pendeleo bi nafsi(bias and stereotype).....
At times huwa najiuliza kuhusu uwezo wa kufikiri wa huyu mtu nakosa jibu. Kweli alienda hata shule zaidi ya secondary?
 
Leviticus unajiuliza juu ya hoja ya Makonda au Mimi niliyechangia?
 
Ukweli upo mkubwa tu... Mwanamke wa kizungu ukianza kuleta mipesa nyumbani ambayo hajui imepatikanaje lazima akufokee na hii ni kwasababu kule kwao sheria ni ngumu kwenye mambo ya money laundering na kukwepa tax.. Ila huku kwetu mwanamke haulizi umepataje yeye anawaza kutumbua tu
Naona mmeamua kumuunga mkono. Mnashindwa vipi kuthamini wanawake? Mafisadi wanakuwa driven na tamaa, tamaa ya kuwa na pesa! Assuming huyo fisadi ni mwanaume basi atataka kuwa na gari la maana, nyumba nzuri hata 10, safari za huku na kule, casino na kuhonga mwanamke au mwanaume kutegemea mlengo wake. Na wanaume bila shaka dau lao ni kubwa.

Na sikubaliani na yeye kwa vile tumeona watu wanaotuhumiwa au tunaowatuhumu kwa ufisadi miongoni mwao kuna wanawake. Makonda asi generalize. Wanawake wengi wa Tanzania ndio tunabeba nyumba zetu kwa kufanya kazi halali. Kama tungekuwa wachunaji, Magufuli asingekuta kitu.

Rekebisheni kauli zenu. Hiko sio kitu cha kujivunia wala mzaha!

Hata wanawake wenye longtime commitment na anayekuelewa lazima atahoji, chances lazima atmdanganywa na kumuaminishwa kwamba amepata kihalali.
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

1.JPG

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

Makonda amewaambia wanawake hao kuwa hata katika suala la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya akina mama kwa watoto tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kupunguza changamoto zinazozikabili miji mbalimbali kwa kipindi hiki ambacho kuna changamoto ya usafi.
Wanawake hawa wanaokesha kitafuta kuni za kupikia ili familia ipikiwe chakula?
Wanawake hawa wanaoshinda shambani na watoto migongoni ili familia iwe na kipato.
Wanawake ambao baada ya kushinda shambani na kurudi nyumbani na mzigo wa kuni kichwani na mtoto mgongoni.
Wanawake hawa wanaolala chini hospitalini wakati wa kujifungua.
Wanawake hawa wanaohangaika kupata karo na sare ya watoto wao kwa kupika na kuuza pombe.
Wanawake hawa wanaoamka alfajiri na kulala usiku wa giza ili kutunza familia.
Labda kuna wanawake wa nchi au sayari nyingine ambao anawazungumzia.
Mwamamke wa kitanzania angekuwa kisababishi cha rushwa asingekuwa na dhiki zote hizi.
 
Hapa napo Kikgwa ngala amuombe Nape aombe samahani kwa wanawake, hii si sawa kabisa, haaa! wanawake ndio wanasababisha uchafu?ina maana yeye halei watoto wake? Au babake hakuhusika na malezi yake? kweli huyu jamaa sijui amefikiria kw akiungo gani, hata angetumia masaburi asinge kashifu wanawake.
 
Wanawake hawa wanaokesha kitafuta kuni za kupikia ili familia ipikiwe chakula?
Wanawake hawa wanaoshinda shambani na watoto migongoni ili familia iwe na kipato.
Wanawake ambao baada ya kushinda shambani na kurudi nyumbani na mzigo wa kuni kichwani na mtoto mgongoni.
Wanawake hawa wanaolala chini hospitalini wakati wa kujifungua.
Wanawake hawa wanaohangaika kupata karo na sare ya watoto wao kwa kupika na kuuza pombe.
Wanawake hawa wanaoamka alfajiri na kulala usiku wa giza ili kutunza familia.
Labda kuna wanawake wa nchi au sayari nyingine ambao anawazungumzia.
Mwamamke wa kitanzania angekuwa kisababishi cha rushwa asingekuwa na dhiki zote hizi.
Umeongea vyema sana, mwanamke huyu ambae anaombwa rushwa ya ngono ili apte ajira, mwanamke ane kesha mtoto akiumwa, mwanamke ane lia kuomba Mungu baraka kwa nchi yake. Eti Makonda nae kiongozi?! maajabu.
 
Akili za kushikiwa ndivyo zilivyo, kama huna cha maana cha kuongea ni bora kukaa kimya kuliko kukurupuka na kuongea pumba.
 
Kila akisemacho mtu kwani lazima iwe ishu ya kujadiliwa? mambo mengine ni sehemu ya maongezi tu jamani.
 
Jamani ninashauri hawa viongozi waandaliwe hotuba
Wasiwe wepesi kuzungumza na watu wakiwakuta wamejikusanya wawapungietu kisha wapite.Madaraka yanaendana na umri ,uzoefu na busara.Hayo mambo yasipokuepo uongozi wa mtu huingia doa sugu
 
Namuomba Rais a revisit sababu zake za kumteua huyu mkuu wa mkoa. Umefika wakati wakumpangia kazi nyingine.

Wanawake wenzangu mko wapi? Mbona kuna pattern kutokuthaminiwa awamu hii?
Nena uko sahihi. Katika dunia ya leo kauli hiyo ni mashambulizi ya wazi dhidi ya wanawake. Ni udhalilishaji wa wazi kwa wanawake. Ni mashambulizi ya wazi dhidi ya wote wanaotetea haki sawa kwa makundi yote. Na bahati mbaya kabisa kauli hii inatolewa na mtu ambaye anapaswa kuwa mtetezi wa wanawake.

Hivi RC hajui kama kuna wanaume wanafaidi pesa za kifasadi kutoka kwa wanawake mafisadi? Ni wakati wa wanawake kusimama na kuungana pamoja kupinga udhalilishaji huu wa wazi!
 
Naona mmeamua kumuunga mkono. Mnashindwa vipi kuthamini wanawake? Mafisadi wanakuwa driven na tamaa, tamaa ya kuwa na pesa! Assuming huyo fisadi ni mwanaume basi atataka kuwa na gari la maana, nyumba nzuri hata 10, safari za huku na kule, casino na kuhonga mwanamke au mwanaume kutegemea mlengo wake. Na wanaume bila shaka dau lao ni kubwa.

Na sikubaliani na yeye kwa vile tumeona watu wanaotuhumiwa au tunaowatuhumu kwa ufisadi miongoni mwao kuna wanawake. Makonda asi generalize. Wanawake wengi wa Tanzania ndio tunabeba nyumba zetu kwa kufanya kazi halali. Kama tungekuwa wachunaji, Magufuli asingekuta kitu.

Rekebisheni kauli zenu. Hiko sio kitu cha kujivunia wala mzaha!

Hata wanawake wenye longtime commitment na anayekuelewa lazima atahoji, chances lazima atmdanganywa na kumuaminishwa kwamba amepata kihalali.

Huyo fisadi uliyemwongelea hana mke?? Kwanini mke akiona kuna mipesa michafu inaingia asitoe taarifa kwa vyombo vya usalama au asimwonye mmewe?? Wewe mkeo akiwa anakuja na mipesa nyumbani na kubadilisha magari mbona unashupaza shingo kwa kudhani anahongwa.. Tena unampiga mpaka stop au kumfanyia hila aache kazi akae nyumbani
 
Back
Top Bottom