Makonda: Sitamsaliti Hayati Magufuli hata niwekewe bastola

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,753
15,227
Katibu mwenezi wa CCM Taifa bwana Paul Makonda akiwa analia kwenye kaburi la Hayati Magufuli wilayani Chato ameapa hatakuja kumkana wala kumsaliti Hayati Magufuli hata kama atawekewa bastola kichwani.

Makonda amesema Magufuli ni role model wake katika kulipenda na kulitumikia taifa lake mpaka kufa.

Katibu mwenezi huyo amewataka wanaomchafua Magufuli kwa mabaya wajaribu kuyataja na mazuri yake.

===
Paul Makonda ambaye ni Katibu mwenezi wa CCM amesema hatukuja kumsaliti Magufuli hata akiwekewa bastola kichwani. Amesema Magufuli alikuwa ni mwalimu wake, rafiki na mshauri.

Makunda amesema hayo baada ya kutoka Chato alipoenda kuzuru kaburi la aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Aidha amesema wanaotaka kumgombanisha Rais Samia na Magufuli hawatoweza kwa kuwa uteuzi wa Makonda kwa nafasi ya uenezi wa chama ni kielelezo tosha cha kuwa Samia hana chuki na Magufuli.
 
Back
Top Bottom