GE2025 Makonda: Nililishwa Sumu nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ilikuwa nife mwaka 2024

GE2025 Makonda: Nililishwa Sumu nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ilikuwa nife mwaka 2024

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda, amekiri kuwahi kulishwa sumu hali iliyomsababishia kulazwa hospitalini na kutoonekana hadharani.

Makonda amefichua siri hiyo leo Jumapili, Septemba 21, 2025, wakati wa ibada katika Kanisa la Mbingu Duniani lililopo Njiro - Arusha, akisema si mara yake ya kwanza kulishwa sumu na kwamba amenusurika kifo mara kadhaa.

"Kuna kipindi nilipotea nikaanza kutafutwa, na wengine mlinitafuta kwa nguvu kubwa huyu yuko wapi. Ukweli nilikuwa naumwa, nililishwa sumu, Yasingekuwa maombi ya Watanzania na Mungu kumuinua Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia matibabu yangu nilitakiwe nife mwaka jana," amesema Makonda.


Soma >> Mtoto pendwa kapatwa na nini? Yuko hoi kwa Madiba, inadaiwa ni sumu
 
Mbona hajasema alivamia ofisi ya watu 4 usiku
20250920_104435.jpg
 
Back
Top Bottom