DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema endapo atashinda uchaguzi na kuingia bungeni, ataweka nguvu kubwa katika kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030.
Makonda amesema anatarajia kutumia nafasi hiyo kuhakikisha uwajibikaji unazingatiwa serikalini na vijana wa Tanzania wananufaika na matunda ya maendeleo yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
“Niwahakikishie kule bungeni moto utawaka, nitapiga spana watu mpaka kitaeleweka. Tunataka haki na kila mtu awajibike kwa nafasi yake ili kila kijana wa Tanzania afurahie matunda ya Taifa lake,” amesema Makonda Jumatano, Oktoba 9, 2025, alipokuwa akizungumza na wakazi wa Lamadi, mkoani Simiyu.