Makonda kufanya mahojianao Clouds kuhusu yanayosemwa juu yake

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,679
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameujulisha umma wa wana Dsm kuwa kesho saa 6 za mchana atakuwa kwenye studio za Clouds fm kujibu upotoshaji unaofanywa na anaosema wabaya wake kupitia mitandao ya kijamii. Ameeleza hayo kupitia akaunti yake ya instagram.


Maoni yangu; Mh Makonda hana haja ya kwenda media kutoa ufafanuzi wowote, anachotakiwa ni kufanya vitendo zaidi ndio yatakuwa majibu mazuri. Watu hawaridhishwi na matamko hasiyoweza kuyasimamia wala sio wote wanachuki za kiadui. Afanye vitendo zaidi kama boss wake.
 



Wewe ndie hamnazo kwelikweli! mchawi wa Makonda ni Makonda mwenyewe, na kwa mwendo huu Makonda kutoboa 2020, itakuwa muujiza labda JPM aamue kwa makusudi kabisa kufunga macho na kuziba masikio kabisa!
Makonda anachokosea ni kujiona anaweza kuigeuza Dar single handedly; jambo ambalo sio kweli kabisa, uwezo huo hana na kamwe hatakaa aweze kuwa nao!
Makonda is choping off more than he can chew! ameanzisha vitu vingi sana kwa wakati mmoja, badala ya kupanga vipaumbele na kuvisimamia kwa awamu na kufanya tathmini ya ufanisi wake kabla ya kuanza na jambo jingine!! he is stretching himself too thin.

mtu anapochagua kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ni lazima ama mafanikio yake yatakuwa kiduchu au hamna kabisa. Makonda atoe tathmini ya ufanisi wa jambo lolote kati ya yote aliyoyaanzisha ndio umma utajenga imani kwamba kweli sasa dar imepata jembe!

Kuanzia usafi wa jiji, machangudoa, mashoga, bunduki, ujambazi, ufisadi, panya road, nauli bure kwa walimu, ukosefu wa ajira kwa vijana, migogoro ya ardhi nk nk!

Vinginevyo anguko la Makonda limeshaanza kuonekana japo kwa mbali.
 
Uko sahihi mkuu, akiongea wakazi wa jiji wanajua kiongozi wao kaonge, sio huyu analazimisha tusikie kaongea.
Kabisa aisee, na watu walikua wanatii tena kwa amani zote (walikua wana afiki) na kila mtu alikua huru ...
Kuna haja sana ya jamaa kuiga mfano wa mzee, na ukizingatia kwamba busara za wazee ni za muhimu sana pia.
 
Kuna vijana wengi wa CCM hawampendi Makonda, wanatamani ashindwe katika mengi sana, wao kila siku wanamuombea mabaya lakini, Makonda anafanya vizuri, Kuna baadhi ya ma groups ya WhatsApp ya watu wa CCM, kazi yao kumuombea mabaya Makonda, ila naona God hapokei dua zao, maana nazani wanasubiri ashindwe tu wasema tulishasema
 
Nadhani kazi anazidanya vizuri. Ila hili la kuongea kwenye media ni hatua nzuri pia kwani biashara ni matangazo
 
Daah huyo jamaa hiyo nafasi maji marefu kwake. Alitakiwa aachwe kwenye UDC aongeze experience. Anahangaika ku attract attention kwa wateuzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…