Makonda kufanya mahojianao Clouds kuhusu yanayosemwa juu yake

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameujulisha umma wa wana Dsm kuwa kesho saa 6 za mchana atakuwa kwenye studio za Clouds fm kujibu upotoshaji unaofanywa na anaosema wabaya wake kupitia mitandao ya kijamii. Ameeleza hayo kupitia akaunti yake ya instagram.


Maoni yangu; Mh Makonda hana haja ya kwenda media kutoa ufafanuzi wowote, anachotakiwa ni kufanya vitendo zaidi ndio yatakuwa majibu mazuri. Watu hawaridhishwi na matamko hasiyoweza kuyasimamia wala sio wote wanachuki za kiadui. Afanye vitendo zaidi kama boss wake.
 
Habari wadau;

Kuna kundi la wanufaika wa uhalifu,matapeli,mashoga na wanufaika wake kwa kushirikiana na nyumbu na viongozi wao, wameanzisha propaganda chafu za kumdhihaki mkuu wetu bora ambaye anasafisha jiji lililokuwa limegeuzwa dampo la kiila aina ya uozo. Kuna watu maisha yao yote yalikuwa ni udalali na utapeli, Watanzania tujiulize hivi wewe kama ni mtu mwema makonda kafanya lipi baya? Rc makonda anamakusudi ya dhati ya kuliweka jiji safi na kwa hilo nauhakika atafanikiwa, asigeuke nyuma kamwe. Ana mpango wa dhati wa kuwasaidia vijana kupata ajira na kuwatengenezea fursa mbalimbali, Je atawezaje Pasipo kuwa na Takwimu ya wasio na ajira? Wapinzani wanajuwa kabisa endapo atafanikiwa yote anayoyafanya, ni dhahili kabisa upinzani utakuwa umekufa. Watuambiye ni nani anafaa mwingine zaidi ya makonda? Eti sasa hivi wanasema bora ya aliyekuwa mkuu wa mkoa MECKY SADICK , Jiulize alipokuwepo mbona walimponda? Waogopeni hao wanafiki Makonda tunamwamini ataendelea kuziba mianya ya waharifu bila uwoga. Naomba mtambue kwamba Wapenda uharifu,wakwepa kodi na Mashoga hawapendezwi na utendaji wa Mkuu wetu mtukufu; MAKONDA GO! GO! GO! Wengi tukonyuma yako.

WALIOZOEA VYA KUNYONGA SASA HIVI VYA KUCHINJA KWAO NI HARAMU NI WA KUPUUZWA



Wewe ndie hamnazo kwelikweli! mchawi wa Makonda ni Makonda mwenyewe, na kwa mwendo huu Makonda kutoboa 2020, itakuwa muujiza labda JPM aamue kwa makusudi kabisa kufunga macho na kuziba masikio kabisa!
Makonda anachokosea ni kujiona anaweza kuigeuza Dar single handedly; jambo ambalo sio kweli kabisa, uwezo huo hana na kamwe hatakaa aweze kuwa nao!
Makonda is choping off more than he can chew! ameanzisha vitu vingi sana kwa wakati mmoja, badala ya kupanga vipaumbele na kuvisimamia kwa awamu na kufanya tathmini ya ufanisi wake kabla ya kuanza na jambo jingine!! he is stretching himself too thin.

mtu anapochagua kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ni lazima ama mafanikio yake yatakuwa kiduchu au hamna kabisa. Makonda atoe tathmini ya ufanisi wa jambo lolote kati ya yote aliyoyaanzisha ndio umma utajenga imani kwamba kweli sasa dar imepata jembe!

Kuanzia usafi wa jiji, machangudoa, mashoga, bunduki, ujambazi, ufisadi, panya road, nauli bure kwa walimu, ukosefu wa ajira kwa vijana, migogoro ya ardhi nk nk!

Vinginevyo anguko la Makonda limeshaanza kuonekana japo kwa mbali.
 
Uko sahihi mkuu, akiongea wakazi wa jiji wanajua kiongozi wao kaonge, sio huyu analazimisha tusikie kaongea.
Kabisa aisee, na watu walikua wanatii tena kwa amani zote (walikua wana afiki) na kila mtu alikua huru ...
Kuna haja sana ya jamaa kuiga mfano wa mzee, na ukizingatia kwamba busara za wazee ni za muhimu sana pia.
 
Kuna vijana wengi wa CCM hawampendi Makonda, wanatamani ashindwe katika mengi sana, wao kila siku wanamuombea mabaya lakini, Makonda anafanya vizuri, Kuna baadhi ya ma groups ya WhatsApp ya watu wa CCM, kazi yao kumuombea mabaya Makonda, ila naona God hapokei dua zao, maana nazani wanasubiri ashindwe tu wasema tulishasema
 
Makonda anatakiwa kujipanga vizuri na kufanya kazi kwa vitendo. Aache kuchosha watu na matakamko yake ya kipuuzi kila kukicha. Dar es Salaam ndio mji mkuu wa biashara Tanzania, anatakiwa kulitambua hilo na kufanya kazi zinazoendana na hadhi ya jiji na sio huo utoto anaofanya.
Nadhani kazi anazidanya vizuri. Ila hili la kuongea kwenye media ni hatua nzuri pia kwani biashara ni matangazo
 
Daah huyo jamaa hiyo nafasi maji marefu kwake. Alitakiwa aachwe kwenye UDC aongeze experience. Anahangaika ku attract attention kwa wateuzi wake
 
Back
Top Bottom