Makonda kufanya mahojianao Clouds kuhusu yanayosemwa juu yake

Kesho ni Jtatu siku ya kazi arekodiwe then mtarusha hiyo interview yake usiku Wa kesho kama recorded interview
 
Kwanini clouds? Redio uhuru na TBC si zipo?


...clouds ni kati ya washauri wa mh. Makonda! Au ulikuwa hujui?

Daah huyo jamaa hiyo nafasi maji marefu kwake. Alitakiwa aachwe kwenye UDC aongeze experience. Anahangaika ku attract attention kwa wateuzi wake

uko sahihi mkuu.

hizi nyazfa za serikali hazihitaji watu wa kukurupuka kama makonda...
zinahitaji utulivu, busara na maono ya mbali.

Makonda afanye kazi na atoe maagizo kupitia mikutano ya ndani ya utendaji... Sio kwenye media kila siku.

Itafikia wakati raia wata mchoka mh. Makonda na kumpuuza....
 
Makonda ni kijana anayejituma ila apunguze kukumbatiana na wasanii maana sasa amekuwa msanii kabisa.
 
Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa Clouds Media ina wafuatiliaji wengi sana. Hivyo ni sahihi kwa RC kutumia media hiyo
Sio kweli. East Africa is the best eductive and entertaining. Haina figisu figisu. Kama ni burudani na sports pekee basi Efm iko vizuri. BE INFORMED!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameujulisha umma wa wana Dsm kuwa kesho saa 6 za mchana atakuwa kwenye studio za Clouds fm kujibu upotoshaji unaofanywa na anaosema wabaya wake kupitia mitandao ya kijamii. Ameeleza hayo kupitia akaunti yake ya instagram.


Maoni yangu; Mh Makonda hana haja ya kwenda media kutoa ufafanuzi wowote, anachotakiwa ni kufanya vitendo zaidi ndio yatakuwa majibu mazuri. Watu hawaridhishwi na matamko hasiyoweza kuyasimamia wala sio wote wanachuki za kiadui. Afanye vitendo zaidi kama boss wake.
Makonda apo ndio unakosea na hapo ndipo kiatu kina pwaya. Unaenda kumfafanulia nani? Wewe nikiongozi wa serikali clouds kunani? Je utetezi wako utabadilisha ushauri aliopewa rais na washauri wake kuhusu wewe? Au umesahau anayekuteuwa anahaki kukupumzisha ili watu walale? Tulia mkuu niliwahi kukushauri kwa maneno haya uteuzi wako waweza leta mabadiliko chanya kwa vijana au fungia vijana nafasi. Tuwe wakweli umeshawaharubia vijana sina uwakika hata uule kama watampa......
 
Huyu jamaa inawezekana kweli nafasi aliyopewa kubwa kuliko umri wake maybe au mkoa ndio tatizo, maana Dar ndio Tanzania
 
Si aje atoe tu hapa hapa jf kwa id yake? Au anaogopa vichwa vya jf vitamshushua?
 
Tuwekeeni ile video alo ongea kuhusu nyumba hadi nyumba
Maana hata magazeti yaliandika
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameujulisha umma wa wana Dsm kuwa kesho saa 6 za mchana atakuwa kwenye studio za Clouds fm kujibu upotoshaji unaofanywa na anaosema wabaya wake kupitia mitandao ya kijamii. Ameeleza hayo kupitia akaunti yake ya instagram.


Maoni yangu; Mh Makonda hana haja ya kwenda media kutoa ufafanuzi wowote, anachotakiwa ni kufanya vitendo zaidi ndio yatakuwa majibu mazuri. Watu hawaridhishwi na matamko hasiyoweza kuyasimamia wala sio wote wanachuki za kiadui. Afanye vitendo zaidi kama boss wake.
Nani aisikilize redio ya wahuni zaidi ya wahuni wenzie
 
Wabaya wake ni yeye mwenyewe.
Nakumbuka wakati niko jeshini kwa mujibu wa sheri, CO wetu alikuwa anatuambia kama wewe ni kiongozi ukiona unataka kutoa amri na haitatekelezeka basi nyamaza maana itakupunguzia heshima kwa wale unao waongoza.
Ndugu yangu Makonda baada ya kupata ujiko amekuwa ni mtu wa matamko ambayo hayatekelezeki,
Anasema malaya Dar waondoke hawambii waende wapi,
Anasema ombaomba waondoke halafu yeye muda huo huo anatokea channel 10 anaomba msaada wa madawati.
Anasema atapita nyumba kwa nyumba kusaka wasio na kazi hakumbuki yeye alisota muda gani bila kazi hadi alipo pata ujiko kwa kumshambulia mzee Warioba.
Asidhani kutumia media sana ndio kumdanganya Mh Rais kwamba yuko busy, bali utendaji ni ku deliver.
 
Back
Top Bottom