Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Yaani hiyo ni kabisa, na wanaisubiria kwa hamu sana.
Kwa akili zenu mmewaona watanzania viraza wasiojitambua km Bashite???

Waulizeni bongo movie watz wamewanyoosha.

Watz tunalilia watz wenzetu waliofukuzwa kazi kisa vyeti fake lakini Makonda yupo na hajafanywa lolote.

Lkn Makonda ni nani??? Mkuu wa Mkoa wa Tanzania???.

Watz si cheep to that extent , by the way buriani star TV.
 
Star tv wanaonyesha kujielewa na kutokubali kuburuzwa kijinga. Vyombo vingine vinaskilizia star tv akishafanya basi nao wanafanya
 
Hapa ni bihashara nyie nuneni au zima TV yako , cc tuna imani na Makonda wengine acha upuuzi wenu
Yani tuzime TV kwa sababu ya star TV??? Ngachoka!!! TV ambayo imedoda km TBC, .

Mshauri aende azam tv, ITV, Chanel ten labda tutazima tv zetu lkn sio star tv
 
- Hahaha Ndugu najua unasoma hapa, naomba kukuhakikishia kuwa umedanganywa na huenda hujui kinachoendelea, halafu punguza chuki kwa RC hajakukosea chochote zaidi tu ya kurubuniwa kwako na wanaomchukia kwa sababu yupo karibu na Rais. Hao wanasiasa waliokurubuni huko waliwahi pia kukurubuni na kumbu kumbu zake zipo humu JF toka ulipokuwa unasoma London/UK, jana nimeona matusi uliyomrushia mwananchi mmoja huko kwenye Group lako la Watsap ambaye umemtukana sana kwa sababu ya kumuunga mkono RC, WHY? Mkuu RC wewe binafsi amekukosea nini hasa cha kukufanya wewe kutukana matusi ya ajabu vile?

- Kwa nini unasema Uongo kwenye huu waraka wako kama ule uongo uliousema kuwa RC alikukimbia ofisini kwake? Uongo wa kitoto ambao sikutegemea mtumzima msomi kama wewe unaweza kujiingiza nao, Ofisi ya RC ina Milango Miwili mmoja wa kuingilia na mwingine kutokea kwa pembeni kwa hiyo hakuna Mlango wa nyuma kama ulivyodai ulikuwa ni uongo wa kitoto sana, na besides ili umfikie RC ofisini kwake ni lazima upitie Getini ujiandikishe wamuulize Secretary wake ndio uruhusiwe kupanda juu kwa Secretary wake usubiri amfahamishe RC kuwa upo ndio uruhusiwe kuingia kumuona, sasa kama RC alikuwa hataki kuwaona na Tume yako hivi kweli alihitaji kuwaruhusu mfike mpaka ndani ya ofisi yake ndio akimbie? Huoni kuwa ni uongo wa kitoto wakati unajua kabisa siku mliyopanga kwenda kumuona ndiyo siku Bosi wake Waziri wa Tamisemi alimpitia na kwenda naye Ilala Machinga Complex, sasa wewe uliendaje kumuona RC ambaye hakuwepo ofisini I mean WHY UNADANGANYA?

- Leo again umeibuka na uongo mpya kwamba eti kuna "Wpambe wa RC wanaojaribu kuwaomba Waandishi wamuandike" ...hahahahah kwanza naomba kucheka sana kwa sababu binafsi nimefuatwa na kundi la Waandishi walionifahamisha kwamba wana mpango wa kuachana na mgomo wako na kuanza kumuandika kwenye magazeti yao 5 makubwa hapa mjini, na wakaniomba nimfahamishe RC ili awakatie mzigo hahahahaha niliwacheka sana nikawaambia kwamba HAITAKUJA KUTOKEA NEVER maana kwa maneno mengine walichokitaka inaitwa "BLACKMAIL" niliwauliza so mligoma ili mje mdai pesa kumuandika? hahahahahahha

- Mkuu wewe, ni mtu unayetakiwa kuheshimika na jamii kwa usomi na kazi yako lakini kwa kukubali kutumiwa na Wanasiasa umejiharibia sana na kwa muda mrefu sasa, I mean hizi Chuki zako na wanaokutuma zitawasaidia nini hasa mbele ya Wanasiasa ambao hubadilika kila siku? Majuzi Lowassa alikuwa adui namba moja wa Wanasiasa wa CCM wanaokutuma leo ni Rafiki yao mkubwa kwa siri tunajua sana. So how can you trust your life kwa Wanasiasa wa namna hiyo ambao Mange alikuwa adui yao mkubwa leo ni Rafiki yao mkubwa mpaka wanampa habari nyingi za uongo kama za Kinana au mnadhani hatufahamu? Tunajua sana ila tunajiuliza mnachopigania ni nini hasa wakati Uchaguzi ulishaisha Mwaka 2015?

- Nikukumbushe tena hakuna Mwandishi aliyeombwa kwa kushawishiwa kupewa rushwa ili amuandike RC hapana, ila kuna Mjumbe wa hilo Baraza lako aliyemtishia sana Muandishi atakayemuhoji RC Jumatatu hahahahaha naomba kukuambia kwamba huo muungano wenu ni wa wachawi hauwezi kudumu ndio maana tulisema it is about time tu mtavurugana wenyewe kwa wenyewe, kwa sababu magazeti sasa hivi hayauzi na tunajua kuna Wanaowalipa kufidia hasara lakini hata wao wanawalipa kwa taabu sana hahahahaha anyways nakuomba usijiaminishe sana kuandika kama unawaongoza Waandishi wote HAPANA, maana wengi wanahangaika na njaa na huu mgomo. Wewe na wanaokutuma mlishashindwa siku nyingi na mtashindwa tu maana hamna sababu ya msingi ya mgomo na hakijaharibika kitu cause slogan yetu ni ile ile "KAZI JUU YA KAZI yaani BAMPA TO BAMPA". Halafu jitahidini basi Jukwaa lako na Wanasiasa wanaokutuma mfanye kitu cha msingi kwa jamii kama RC anavyofanya, Jengeni Mahospitali tu kusaidia Wananchi ili tujue kwamba umoja wenu ni wa nguvu kama ulivyosema sio wa kujitokeza kutaka kumchagulia Rais viongozi wake hahahahaha

- By the way hii interview itafanyikwa Jumatatu Saa Moja na Nusu Asubuhi, Tarehe 22/5 unakaribishwa sana kuhudhuria au kuangalia kwenye Luninga wa Star TV, otherwise nimejifunza kwamba kumbe kupigana na Wauza Madawa ya Kulevya sio mchezo maana majibu yao ndio haya tunayaona kwa macho yetu sio tena kwa kusimuliwa! Nakukumbusha sana kwamba mgomo wakomunawaumiza sana Waandishi wa Habari wasiolipwa Mishahara kwa muda unaotakiwa, wasiokuwa na pensheni wala Bima za afya, jitahidi basi kuwapigania kwenye hayo na hilo Baraza lako msiishie kumgomea RC tu!

- Kuhusu mnaouita "UVAMIZI WA CLOUDS" naomba kusema tena na tena nimeamua kuunyamazia kwa sababu Mmiliki wa Clouds ni rafiki yangu waa karibu sana ndio maana sipendi kugusa hiyo ishu, ambayo ninajua ilivyopangwa kwenye vikao huko Dodoma na washiriki wote wa hivyo vikao tunawajua, ni aibu tupu kwa watuwazima kutishiana nyau kwa ishu ambazo mnajua kabisa kuwa ni uongo wa kitoto sana ila endeleeni kuwadanganya wasioelewa.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

- Le Mutuz Nation
Kumbe Lemutuz
 
SWALI KWA KINA BALILE: NI KWELI KWAMBA UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI?

Mpendwa Mr. Deodatus Balile,

Salaam sana.

Nafahamu wewe ni mchambuzi makini.
Mimi ni mchambuzi makini pia.
Ninaandika haya kama mdadisi huru.


Kimsingi, nina maswali machache kwako kama Makamu Mwenyekiti pamoja na viongozi wenzako kuhusu mkakati wa smart sanctions mnaoutekeleza:

1. Unakumbatia maadili ya kimachiaveli. Kuna lengo zuri (kumwadhibu mkosaji) lakini zinatumika mbinu haramu (kuwanyima umma habari kamili katika mfumo wa 5W and 1H). Unasemaje kuhusu hili?

2. Unaifundisha jamii kuamini katika sera ya jino kwa jino, falsafa ya kukomoana. Bashite akifanya mabaya habari zake zinaandikwa (mfano alipoitwa Bungeni Dodoma), akifanya mazuri habari zake haziandikwi. Unayo maoni gani hapa?

3. Unaifundisha jamii undumila kuwili. Unamtumia mtu pale unapoona anakufaa, na kumtelekeza pale unapoona humwitaji. Kwa nini mnafanya hivo?

4. Una harufu ya kisiasa. Sasa Media sector inaonekana kuungana dhidi ya state organs, pasipo sababu za msingi. Kwa nini tunashindwa kuwa objective? Kwa mfano ktk ripoti yako kwa Nape unaandika "Makonda alivamia Clouds TV Studio." Ulishindwaje kufanya utafiti kidogo ili ujielimjishe kuhusu maana ya neno "vamia," angalau kwa kusoma Kamusi ya Kiswahili Sanifu? Huoni kwamba ulifanya siasa kwa kutumia utata wa kimisamiati?

5. Unakosa uhalali kisheria. Nikikupiga ngumi wewe, unayo locus standi ya kunishitaki mahakamani, lakini jirani yako hana locus standi hiyo. Clouds walitendewa isivyo, lakini Clouds sio media sector yote. There is a difference between a whole thing and its parts. You are confusing the two illogically. Wanasheria wenu wameshindwaje kuwashauri hapa? Au nao wanafanya siasa katika sheria?

Hebu nisaidie kuniondolea utata huo hapo juu, kwa kutoa majibu yasiyo na makona.
Kama hamwezi kufanya hivyo, basi hebu badilini mkakati wenu wa smart sanctions.


Asante.
 
Dhambi ya Unafki ni dhambi mbaya sanaz hata mafarisayo na masadukayo Yesu aliwakemea kwa dhambi ya Unafki.

Unafki huu kufanywa na Star TV sio jambo la kushangaza maana Star TV ni vibaraka wa chama tawala.

Mungu tusaidie kutuondolea dhambi ya Unafki.
 
Kufuatia kitendo cha Kituo cha Luninga cha Star Tv kuamua kuisaliti Tasnia ya Habari nchini Tanzania kwa kuanza kushirikiana na Bashite ili kurusha habari zake, Vita dhidi ya Chombo hicho kutoka kwa wadau mbalimbali hapa nchini imeanzishwa rasmi mitandaoni, mbinu mbalimbali zitatumika, na kwa kuanzia tu, haya yanaanza kufanyika mara moja
mitandaoni.

[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]continentalDecorder
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]starTv
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]radiofreeAfrica
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]kissFm
 
Kufuatia kitendo cha Kituo cha Luninga cha Star Tv kuamua kuisaliti Tasnia ya Habari nchini Tanzania kwa kuanza kushirikiana na Bashite ili kurusha habari zake, Vita dhidi ya Chombo hicho kutoka kwa wadau mbalimbali hapa nchini imeanzishwa rasmi mitandaoni, mbinu mbalimbali zitatumika, na kwa kuanzia tu, haya yanaanza kufanyika mara moja
mitandaoni.

[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]continentalDecorder
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]starTv
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]radiofreeAfrica
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]kissFm
KATAA CHAMA CHA CCM
 
Sijawahi kusikilizaga wala kufuatilia vyombo hivyo vya habari maana niliskia vimebase zaid kanda ya ziwa hata habari zao ni za butimba maswa bukombe igate nyehunge lamadi nk
 
Mtu unaanzisha kampeni wakati huna hata Redio au Television achilia mbali king'amuzi (decoder).

Hii inaitwa ni furahisha genge la wajinga!

Hii kampeni ya kuikataa Vodacom iliishia wapi?

LINK>>Vodacom kukubali kutoa ushahidi dhidi ya Lema ni dharau kubwa kwa Watanzania

Nilisikia kuna mwingine alianzisha kampeni ya kuchoma kadi za CCM! Sijui kampeni yake imefikia wapi?

Tanzania kuna ujinga mwingi sana!
 
Kufuatia kitendo cha Kituo cha Luninga cha Star Tv kuamua kuisaliti Tasnia ya Habari nchini Tanzania kwa kuanza kushirikiana na Bashite ili kurusha habari zake, Vita dhidi ya Chombo hicho kutoka kwa wadau mbalimbali hapa nchini imeanzishwa rasmi mitandaoni, mbinu mbalimbali zitatumika, na kwa kuanzia tu, haya yanaanza kufanyika mara moja
mitandaoni.

[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]continentalDecorder
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]starTv
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]radiofreeAfrica
[HASHTAG]#KATAA[/HASHTAG]kissFm
Huo ukaskazini wenu ulishawashinda siku nyingi. Bado kidogo mtaanzisha [HASHTAG]#KATAAwasukumaKilimanjaro[/HASHTAG]..... Nyambaffffffg
 
Back
Top Bottom