Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurzweil, May 19, 2017.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,894
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI
  Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

  Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

  Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

  Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

  Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

  Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

  Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

  Deodatusi Balile
  Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
  Mei 19, 2017

  4db4c219-d817-4d7e-9f11-02c7e4a692e4.jpg
   
 2. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2017
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 21,415
  Likes Received: 13,206
  Trophy Points: 280
  Vipi? Ina maana wanaweza kuwazuia wasirushe matangazo yao?
   
 3. Dr Simba

  Dr Simba JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2017
  Joined: Apr 27, 2016
  Messages: 800
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 180
  Kunkuchaaa! !!!!
   
 4. kirakapacha

  kirakapacha JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2017
  Joined: Jan 10, 2015
  Messages: 928
  Likes Received: 1,000
  Trophy Points: 180
  Bashite ni nani?
  Jawabu: Mkuu wa mkoa wa Tanzania.
   
 5. Nichumu Nibebike

  Nichumu Nibebike JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2017
  Joined: Aug 28, 2016
  Messages: 6,279
  Likes Received: 10,070
  Trophy Points: 280
  Nadhani maelezo yamejitosheleza. Aliyeandika barua hii anaonekana kweli ana weledi wa kutosha katika tasnia ya uandishi wa habari...
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2017
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  gooood hawa mabazazi wamezidi :D:D:Dtupo pamoja nanyi tusikubali huu ushuzi utapakae tunanyanyaswa why why why?
   
 7. mjingamimi

  mjingamimi JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2017
  Joined: Aug 3, 2015
  Messages: 11,317
  Likes Received: 9,110
  Trophy Points: 280
  Acheni kuwapangia watu.au mliwasaidia kununua maspika?
  Kama wameamua waacheni.
   
 8. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2017
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  sahara media ilimdHalilisha LowasSa kwenye kipindi cha kampein, na inatumika kisiasa ni ya anthony dialo naona anatafuta kiky japo nyota yake imezimika.......
  zile pangaboi zake ziko wapi ? ndege uchwara sijui aliziokota wapi tehetehe
   
 9. chilumendo

  chilumendo JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2017
  Joined: Oct 26, 2013
  Messages: 1,970
  Likes Received: 1,481
  Trophy Points: 280
  kinachutusumbua watanzania hasa tunapopigania haki ni ukosefu wa umoja ndiyo ugonjwa wetu ulipo
   
 10. ng'ombo

  ng'ombo JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2017
  Joined: Dec 1, 2014
  Messages: 361
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 180
  BURZKB3lSmT.jpg
   
 11. Bonny

  Bonny JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2017
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 10,144
  Likes Received: 18,077
  Trophy Points: 280
  Arusha watch it una uhuru lakin not to that extent
   
 12. c

  chige JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2017
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 5,873
  Likes Received: 9,893
  Trophy Points: 280
  Kipindi kinachovuta audience kubwa kwa Star TV and RFA ni pamoja na kipindi cha Kutoka Magazetini!!

  Kama ndivyo, endapo Star TV wataendelea na programu yao na Daudi Albert Bashite, basi wamiliki wa vyombo vya habari wapige marufuku magazeti yao kusomwa na Star TV na RFA. Aidha, wakataze waandishi wao kushiriki mijadala ya kila asubuhi inayoendeshwa na Star TV ambayo mara kwa mara huwa inaalika watu wa media zingine.
   
 13. Faru fausta

  Faru fausta JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2017
  Joined: Apr 29, 2017
  Messages: 220
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60
  Tulikwambia Hakuna kuandika habari Za BASHITE
   
 14. Topintz

  Topintz Senior Member

  #14
  May 19, 2017
  Joined: Aug 2, 2013
  Messages: 158
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 180
  Kwakweli hamna namna, nawapongeza TEF. Maana ungekua unafiki Star Tv washirikiane na adui wa TEF,station nyingine zikaze kamba alaf viongozi wa TEF wakae kimya tu. Bwana DAB alipewa sharti dogo tu la kuwaomba msamaha wanahabari, kama kashindwa kulitekeleza inaonesha anawadharau na haon umuhimu wa kufanya ivo. Kwa wanaomtetea na hapa wana mtindio wa ubongo.
   
 15. kirikou1

  kirikou1 JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2017
  Joined: Nov 8, 2016
  Messages: 2,891
  Likes Received: 3,527
  Trophy Points: 280
  huyo bashite ana media ya TBC y asiitumie hiyo tena bure kbs :eek:
   
 16. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,999
  Likes Received: 37,701
  Trophy Points: 280
  Wasije tu wakamteka.
   
 17. M

  MENGELENI KWETU JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2017
  Joined: Oct 23, 2013
  Messages: 6,075
  Likes Received: 12,281
  Trophy Points: 280
  Safi Kabisa..
   
 18. B

  Babati JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,030
  Likes Received: 24,169
  Trophy Points: 280
  TBC, Star Tv, Uhuru na Mzalendo hivi siyo vyombo vya habari isipokuwa ni vituko vya habari.
   
 19. Nyama ya Zamba

  Nyama ya Zamba Member

  #19
  May 19, 2017
  Joined: Nov 11, 2016
  Messages: 97
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 25
  Daaah,mkuu umelenga mlemle.Huyu bashite amejaa dharau na lugha za maudhi wamnyoooshe kabsa.Asante sana TEF
   
 20. MBIIRWA

  MBIIRWA JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2017
  Joined: May 24, 2013
  Messages: 2,176
  Likes Received: 4,107
  Trophy Points: 280
  Bashite kila akijaribu kusimama anakula za uso kutoka kwa wanahabari mpaka akae na anavyopenda kuuza sura. Gambo kifungo kinanukia ndio maana polisi waliwapa lifti wanahabari pale Luck vicent..
   
Loading...