Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF | Page 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makonda awaponza Star Tv na Sahara Media mbele ya TEF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurzweil, May 19, 2017.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2017
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 5,198
  Likes Received: 5,169
  Trophy Points: 280
  UAMUZI WA STAR TV NI USALITI KWA TAALUMA YA HABARI
  Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

  Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

  Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

  Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

  Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

  Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

  Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

  Deodatusi Balile
  Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
  Mei 19, 2017

  4db4c219-d817-4d7e-9f11-02c7e4a692e4.jpg
   
 2. M

  Makusudically JF-Expert Member

  #381
  May 20, 2017
  Joined: Feb 3, 2014
  Messages: 1,910
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Ni Wendawazimu kupokea hongo kutoka kwa Gwajima ili kumsusia Rc Makonda.
   
 3. M

  Makusudically JF-Expert Member

  #382
  May 20, 2017
  Joined: Feb 3, 2014
  Messages: 1,910
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Ni Upumbavu na Wendawazimu kuandika barua yenye chuki dhidi ya Rc Makonda bila kuthibitisha kama kweli alishiriki kukivamia kituo cha Clouds Fm akiwa na polisi. Kwanini TEF watoe hukumu kabla ya Tume iliyoundwa na Nape kutoa majibu? Star Tv haina wabdishi makanjanja na wana msimamo unaojitegemea. Big up Star tv na viunga vyake.
   
 4. TBO

  TBO JF-Expert Member

  #383
  May 20, 2017
  Joined: Jan 3, 2014
  Messages: 264
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
   
 5. Matanzia kizebazeba

  Matanzia kizebazeba JF-Expert Member

  #384
  May 20, 2017
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 624
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Uhuru wa Habari afu unawapangia wengine wanachotaka kutangaza??

  Ivi TEF na UTPC ni Regulatory Body ama ni jukwaa na Club tu?? Wanapata wapi mamlaka ya kuwakataza wezao kupractise taaluma yao kwa uhuru ???

  Balile na Meena wanamatatizo na wanatumika vibaya
   
 6. k

  kenyamanyori JF-Expert Member

  #385
  May 20, 2017
  Joined: Feb 9, 2014
  Messages: 723
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 60
  Ni hivi kuanzia hiyo Jumatatu wakimhoji tu hatutaangalia tena Star Tv. Watakoma!
   
 7. M

  Mama BA Member

  #386
  May 20, 2017
  Joined: Aug 4, 2016
  Messages: 26
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 5
  Aombe msamaha kwa lipi? ushasikiliza upande wake wa shilingi? na kama hujasikiliza wawezaje kujudge hao wanaotetea? eti mkuu wa mkoa kavamia, upuuzi wa hali ya tangu lini mkuu wa mkoa akavamia eneo lililo ndani ya mipaka ya utawala wake?
   
 8. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #387
  May 20, 2017
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,531
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Nilikua napendekeza hivi; watu wote MAKINI tungeachana kabisa na kuangalia Start TV pamoja na kusikiliza radio yao ya RFA halafu tuone na yeye Dialo atafanyaje?
  Wafanya biashara kabla ya kupeleka tangazo la biashara kwenye kituo chochote hua wanafanya utafiti wa kujua hiyo TV na au radio inawasikilizaji kiasi gani so kwa mgomo wetu hu ndio Dialo atakapo jua nani zaidi
   
 9. B

  Babati JF-Expert Member

  #388
  May 20, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,845
  Likes Received: 25,105
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu
   
 10. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #389
  May 20, 2017
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,645
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Issue sio kupangiwa mkuu bali walikabaliana kwa umoja wao kwamba waachane na habari za Bashite baada ya kushindwa kuomba radhi kwa kuvamia Cloud media! Na star tv waliridhia haya makubaliano, sasa sijaona mahali wamepangia. Tatizo wabongo hatujui maana ya "agreement" na hatuziheshimu kabisa. Tumesongwa na njaa hadi akilin, hakuna cha msomi na ambaye hajasoma. Be consistent in whatever you are doing, and this is rational.
   
 11. mjingamimi

  mjingamimi JF-Expert Member

  #390
  May 20, 2017
  Joined: Aug 3, 2015
  Messages: 12,718
  Likes Received: 10,569
  Trophy Points: 280
  Sijaona sababu ya wao kujiingiza kwenye ugomvi na makonda na clouds.wakati hao jamaa walikuwa marafiki.siku wakipatana je?
   
 12. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #391
  May 20, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 27,109
  Likes Received: 45,232
  Trophy Points: 280
 13. Mdf

  Mdf Senior Member

  #392
  May 20, 2017
  Joined: May 16, 2017
  Messages: 118
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Hata ukisikiliza upande wa pili,
  Hana la upande mwingine wa shilingi alikosea kama ambavyo binadamu mwingine yeyote anaweza kukosea,hakikuwa kitu cha kawaida pamoja na kuwa ni ndani ya eneo lake la mipaka ya kiutawala.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #393
  May 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,717
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chabusalu, hili la kukubaliana kisha kugeukana nililizungumza kwa kirefu hapa Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent Media Yenye Jeuri Hiyo?.

  Kwenye mambo ya media kuna wamiliki, wahariri, waandishi, watoa habari, watangazaji (advertisers) na walaji wa habari. Very very unfortunately wahariri ambao ndio implementors wa mgomo huo, are not the determinants nini kiandikwe! . Determinants ni wamiliki, na watangazaji wanaoleta pesa za mishahara ya hao wahariri na kugharimia kuiendesha media husika. Editors can't say no to Bashite. Na hili la Star ni mwanzo tuu, wengine wanafuata.

  Paskali
   
 15. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #394
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,146
  Likes Received: 3,546
  Trophy Points: 280
  Nafahamu yote hayo Paskali. Lakini ni "implementors" wa mgomo na "determinants" wa nini kiandikwe walikubaliana kwa pamoja kumtenga Bashite. Na katika hili mimi bado nawaona Startv wanayo hatia, kwa sababu hata kama "advertisers" na hapa niwe wazi tu-yaani serikali imewa influence, walikuwa na nafasi ya kushawishi MOAT na TEF kupunguza au kumaliza msusio huo kabla ya kuamua kufanya ambacho tafsiri yake ni usaliti. Startv walikuwa na nafasi ya kuwa katikati kwa kuwa wao wamejifungamanisha na serikali, na wangeweka mambo sawa ndani kwa ndani.

  Kinachotokea sana ni kibaya zaidi kwa tasnia na Startv. Sisi wengine tunaona Startv wamekula mlungula na tutaendelea kuwaona hivyo hivyo hata milele, na mimi kama mwananchi ambaye natamani kuona media inaheshimika na viongozi wetu wakiwa na adabu kwa kuwa tunawalipa mishahara, baada ya kipindi hicho kurushwa Jumatatu, sitapeleka tangazo langu Startv wala redio Free Africa. Nitaanza kuwachukia mno!
   
 16. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #395
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,146
  Likes Received: 3,546
  Trophy Points: 280
  Uko very low, mkuu. Pumzika tu..
   
 17. Ilisolokobwe

  Ilisolokobwe JF-Expert Member

  #396
  May 20, 2017
  Joined: Jul 29, 2013
  Messages: 1,639
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Kweli wakizUia magazeti yao kusomwa star t✓ watakuwa wamewakomoa
  waache wakimbie na bashite ambaye hatachelewa kuwageukia, hahaha
   
 18. mwengeso

  mwengeso JF-Expert Member

  #397
  May 20, 2017
  Joined: Nov 27, 2014
  Messages: 4,967
  Likes Received: 2,692
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma, wewe uliye very high, angalau hekima inanitawala kutokuamini uzushi
   
 19. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #398
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,146
  Likes Received: 3,546
  Trophy Points: 280
  Rudia kusoma ulichoandika, upumzike halafu urudie tena? Aliyekudanganya kwamba mkuu wa mkoa anaweza akaingia hata chumbani kwako wakati wowote bila utaratibu maalum ni nani? Hivi mkuu wa mkoa kwako ni Mungu? Hata mnayemtetea wakati mwingine anawapuuza sana!
   
 20. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #399
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,146
  Likes Received: 3,546
  Trophy Points: 280
  Hivi watu mnakula maharage gani? nani kawaambia TEF wamezuia wenzao kupractise taaluma yao kwa uhuru? Ni wapi TEF wamewapangia wengine wanachotaka kutangaza? Issue iliyopo ni kuwepo kwa usaliti dhidi ya maamuzi yaliyofikiwa kwa pamoja baina ya TEF, MOAT na clubs. Jamaa zako wa Startv hawajazuiwa, wala TEF hawana mamlaka ya kuwazuia, ila wanaweza kuwatenga, basi! Sasa hapa kitu gani kinasukuma kudai Balile na Meena wanatumika? Unaweza kuthibitisha au ni mahaba tu?
   
 21. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #400
  May 20, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,146
  Likes Received: 3,546
  Trophy Points: 280
  Bora kupokea hongo kutoka kwa Gwajima kuliko kutoka kwa Bashite maana hiyo ni kodi yako mwenyewe!
   
Loading...