Mkuu samahani nimepotia conservations zako na Mayala napata picha kuwa kama unachuki na upande wa Makonda badala ya kutafuya fairness itakayokuongoza ktk kuwalaumu Start tv.Nafahamu yote hayo Paskali. Lakini ni "implementors" wa mgomo na "determinants" wa nini kiandikwe walikubaliana kwa pamoja kumtenga Bashite. Na katika hili mimi bado nawaona Startv wanayo hatia, kwa sababu hata kama "advertisers" na hapa niwe wazi tu-yaani serikali imewa influence, walikuwa na nafasi ya kushawishi MOAT na TEF kupunguza au kumaliza msusio huo kabla ya kuamua kufanya ambacho tafsiri yake ni usaliti. Startv walikuwa na nafasi ya kuwa katikati kwa kuwa wao wamejifungamanisha na serikali, na wangeweka mambo sawa ndani kwa ndani.
Kinachotokea sana ni kibaya zaidi kwa tasnia na Startv. Sisi wengine tunaona Startv wamekula mlungula na tutaendelea kuwaona hivyo hivyo hata milele, na mimi kama mwananchi ambaye natamani kuona media inaheshimika na viongozi wetu wakiwa na adabu kwa kuwa tunawalipa mishahara, baada ya kipindi hicho kurushwa Jumatatu, sitapeleka tangazo langu Startv wala redio Free Africa. Nitaanza kuwachukia mno!
Labda nami nikuulize tu hizo adhabu za TEF zimetajwa ktk kanuni gani za miungano yao?
Na je hizo adhabu zina ukomo wa kuanza kutumikia na kumaliza adhabu yako?
Kama adhabu alopewa Makonda haizingatia hayo napenda nikuambie tu hao TET + MOAT waliendeshwa na mihemko ya wenye nguvu ktk vyama vyao bila kujali Principles of natural justice.
Huenda star tv wame review uamuzi wao na kuchukua maamuzi mapya ambayo sioni shida kwa sbb wao ni wanadamu wanapaswa kuwa dynamic.
Ona Gambia walikuwa wanachama wa ICC lkn miezi 3 kabla uchaguzi wao walijitoa uanachama wa ICC sembuse ktk jambo hili la kibiashara mtu aache kuangalia maslahi yake.
Ndio muono wangu huo wakuu Chabusalu + Mayala.