Makonda awaonya Wastaafu wanaowashwa washwa! Awaelekeza kulea Wajukuu zao...

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,245
103,948
Uenezi CCM, Paul Makonda amesema sio utaratibu kwa Wastaafu kila siku kuongeaongea huku akiwashauri Wastaafu wakishapumzika watulie na walee Familia zao na kwamba kama watahitajika kwa ajili ya kazi wataitwa.

Akiongea Jijini Dodoma leo Makonda amesema “Kuna tofauti kubwa kati ya tuliokuja Mjini kwa kuungaunga na wale tuliowakuta Mjini, tuliokuja kwa kuungaunga tumepigana vita mapori mengi sana, ndio maana hata ukiulizwa hivi Makonda ni nani hata Baba yake humjui kwasababu tumepiga vita vingi sana, niwaombe tu mliopo ndani ya CCM na nje ya CCM huyu Dkt. Samia ndiye Rais wetu ameletwa na Mungu kwa mapenzi yake Mungu tumpe nafasi ya kufanya kazi”

“Sikuweza kusema kipindi cha miaka yote ile kwasababu sikuwa na nafasi yoyote na Mimi utaratibu wangu ukipewa nafasi unapewa kazi uliyopewa ukimaliza unapumzika, huwezi kupewa kazi umemaliza umepumzika wewe ni Mstaafu lakini kila siku upo kwenye microphone, huo sio utaratibu”

“Ukishaitwa Mstaafu tulia lea Familia yako wakikuona wa maana watakuita kama walivyomuita Makonda, huwezi kuwa Mstaafu halafu kutwaa, aah, aah, na Wastaafu Nchi hii wanaheshimika sana na Mimi nimejifunza kutoka kwao, nakumbuka Marehemu Mzee Mkapa alipostaafu siku moja nimeenda nyumbani kwake nikamuuliza Mzee vipi mbona uko kimya sana akasema unataka nifanye nini?, nikamwambia Mzee unajua akasema hapana Mimi nimemaliza wajibu wangu”

“Kwahiyo tumuache Rais Samia afanye kazi , tusilipelipe Watu mitandaoni wamtukane, kama una pesa kuna Bodaboda wanahitaji pikipiki, Mamantilie wanahitaji mitaji, Wavuvi wanataka boti, kama unawapenda wape hao badala ya kuwapa Watu hela wamtukane Rais wetu na ndio maana waliposikia Makonda ameteuliwa wamepiga kelele nyingi kwasababu wanajua nawajua na hofu yao ni kuwajua, walitamani waendelee kukaa kwenye maficho wasijulikane lakini Mungu ni mwema ninawafahamu”

My Take
Watu kama Samia wasio na maono ndiyo huzoa wateule kama hawa ambao hata akili ndogo ya kujua haki ya mtu kikatiba hana. Kwa hiyo Nyerere na Mkapa ni wajinga waliostaafu wakaandika vitabu tena wakikosoa?
 
Uenezi CCM, Paul Makonda amesema sio utaratibu kwa Wastaafu kila siku kuongeaongea huku akiwashauri Wastaafu wakishapumzika watulie na walee Familia zao na kwamba kama watahitajika kwa ajili ya kazi wataitwa...
Mwambieni aendelee kubwabwaja na kuomba aombewe huko kwa makanisa na misikiti kama yule aliyeenda ! Litampata la kumpata! Aendelee kuwaona wengine mapoyoyo!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom