Makonda apiga marufuku maandamano Dar

Makonda apiga marufuku maandamano Dar

hivi dezo ya nauli za waalimu ilishia wapi!?
mashoga!?
kukagua kila nyumba kusaka wasio na kazi!?
eeeeeeh kabla sijasahau na kupaka nyumba rangi viliishja wapi.....

rais ameruhusu kila mtu kufanyia mkutano jimboni kwake.... nimkumbushe tu kua jiji la dar lipo chin ya UKAWA na yy yupo chin yao...
#Mwambie Aache Kukurupuka kana boss wake#
 
Sasa kama hauwezi kumshitaka Raisi wa JMTZ ni kwa nini unasema kavunja Sheria? Hivi huko Chuoni mnaelewa mnachofundishwa au mnakariri tu? Kama huwezi kumshitaki mtu ina maana hiyo Sheria haimuhusu ni rahisi kihivyo tu!

Mlipo wawekea kinga hawa Watawala WATUKUFU SANA mlijua ni mfumo gani mnaoujenga kwa baadae pindi Raia watakapo kuwa na uwezo au ujasiri wa kuhoji na kutenda..Lakini unafikiri Tanzania itaendelea kuongozwa na CCM wakati wote ?..
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda amepiga marufuku maandamano ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Makonda amesema kuwa kufuatia kauli ya Rais,yeye anaitekeleza.

Makonda amesema kuwa kauli ya Rais ni moja ya mambo aliyoapa kuyatii na kuyatenda. Amesema kuwa hataruhusu wala kukubali kufanyika maandamano yakifanyika mkoani mwake.
Makonda ameanza...

Maoni yangu: Kama Mwanasheria sifurahishwi na kuwekwa kando kwa Sheria zinazoruhusu na kuratibu mikutano ya kisiasa na maandamano. Serikali naiomba ifanye tathmini njema juu ya sakata hili.Where are we heading?

Chanzo: Habari,Channel Ten usiku huu
Wanasheria wa Tanzania baadhi yenu mna matatizo
Haupaswi kusema hufurahishwi,chukua hatua nenda mahakamani kaombe tafsiri ya sheria
Huo uanasheria ni wa kugonga fomu za mikopo ya finca tu?
Cc Pasco
 
Mlipo wawekea kinga hawa Watawala WATUKUFU SANA mlijua ni mfumo gani mnaoujenga kwa baadae pindi Raia watakapo kuwa na uwezo au ujasiri wa kuhoji na kutenda..Lakini unafikiri Tanzania itaendelea kuongozwa na CCM wakati wote ?..

Hata kama TanZania haitaongozwa na CCM siku zote lk chadema chini ya Lowasa na Mbowe hawezi kuja kuongoza TanZania kamwe!
 
Akili ndogo inapotawala akili kubwa ni hatari kuliko zinka bora waende Dodoma
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda amepiga marufuku maandamano ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Makonda amesema kuwa kufuatia kauli ya Rais,yeye anaitekeleza.

Makonda amesema kuwa kauli ya Rais ni moja ya mambo aliyoapa kuyatii na kuyatenda. Amesema kuwa hataruhusu wala kukubali kufanyika maandamano yakifanyika mkoani mwake.
Makonda ameanza...

Maoni yangu: Kama Mwanasheria sifurahishwi na kuwekwa kando kwa Sheria zinazoruhusu na kuratibu mikutano ya kisiasa na maandamano. Serikali naiomba ifanye tathmini njema juu ya sakata hili.Where are we heading?

Chanzo: Habari,Channel Ten usiku huu
Hivi ulitegemea makonda aseme nini?ni MTU wa kukurupuka katika media aonekane
 
Huyu naye anakurupuka kama kawaida yake alimwambia ana uwezo wa kuzuia maandamano ni nani?

Makonda ni moja ya wateule wa JPM walioshindwa tayari mpaka sasa! 'Like daddy like son' Kazi yake ni kukurupuka. Yaani huyu jamaa ni mtalaamu wa "copy&paste"

Tangu apewe uDC na sasa uRC ni myu wa matamko yasiyo na mashiko!

Sijui nini hasa kinachomfanya ajione superior na kujifanya yuko karibu sana na JPM! Nakumbuka. alipoingia tu madarakani akaanza na uhakiki wa silaha akafaulu kiasi, akaja na nauli bure kwa waalimu akadoda,akaja na Shisha, hola...!akaja na ombaomba patupu na ....!!!

Sasa sielewi kwanini Mteuzi wake hajamyumbua jipu????
 
Subiri utajua kuwa anao huo uwezo au hana
Wakukurupuka mwenzako huyo wewe kwenye kifungu gani cha katiba kinasema mkuu wa mkuu ana uwezo wa kuzuia maandamano?
 
Huyu alipewa kazi kubwa kuliko uwezo wake ndo maana amekuwa mtu wa kutoa matamko bila utekezaji
Makonda ni moja ya wateule wa JPM walioshindwa tayari mpaka sasa! 'Like daddy like son' Kazi yake nj kukurupuka kama babske JPM. Yaani huyu jamaa ni kiazi na mtalaamu wa "copy&paste"
Tangu apewe uDC na sasa uRC ni myu wa matamko yasiyo na mashiko!
Sijui nini hasa kinachomfanya ajione superior na kujifanya yuko karibu sana na JPM! Nakumbuka. alipoingia tu madarakani akaanza na uhakiki wa silaha akafaulu kiasi,akaja na nauli bure kwa waalimu akadoda,akaja na Shisha, hola...!akaja na ombaomba patupu na ....!!!
Sasa sielewi kwanini Mteuzi wake hajamyumbua jipu????
 
Nina ushauri wa Bure kwa Serikali ya CCM, kwa kuwa wao ndio wenye wabunge wengi, ni heri wangeitisha bunge la katiba ili kuifanyia katiba marekebisho kwa kuondoa sheria zote zinazotoa haki sawa kwa wapinzani, na badala yake waingize matamko yao ili yapitishwe kuwa sheria. Hii itawasaidia kuendesha nchi kwa kufuata katiba na wala si matamko tu. Na kwenye hilo Bunge lao wanaweza ongeza wadau wengine watakaochangia ili kuiboresha zaidi, mfano: wakuu wa mikoa, makamanda wa polisi, n.k.
 
Hivi zawad alizo waaidi wenyeviti na mabarozi wa serikali za mitaa kashawapa au miezi mitatu haijafika? Boda boda, gari na pesa taslimu kwa wenyeviti washindi kashawapa au hajapatikana mshindi???!!!
 
Huyu si ndiye yule anayewaogopa mashoga kwa kuwa wanataka kummaliza? Naye kaamua kukurupuka leo.
Kwa dar kachemka maana ukawa kila wilaya yenye mbunge ikiamua kufanya mkutano na wananchi wake itabidi aumwe kizunguzungu tu
 
Makonda nilishamwambia tatzo kutojua wajibu wake hiv kazi ya mkuu wa mkoa ni kuzuia
Shisha,
maandamano
Ushoga,
Au ni kutojua majukumu yako??

Acha kujitoa ufahamu lasivyo Katavi inakuusu
Mkuu kwa kweli nazipenda sindano zako kumuelekezea makonda
 
Back
Top Bottom